Kariakoo Derby: Simba SC 2 - 2 Yanga SC | Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara - Uwanja wa Taifa Dar

Kariakoo Derby: Simba SC 2 - 2 Yanga SC | Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara - Uwanja wa Taifa Dar

Refa ameshindwa kubalance mchezo wakati anajua hii ni game kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sheria ya mpira wa miguu inayosema kazi ya Refa ni kubalance mchezo...ataamua kulingana na sheria 17 za mpira wa miguu kuhusu ile penalt its clear penalt tena alipaswa atoe card coz yule bek alkua last man

地那天刚才妇产科☆
 
Umepanick mkuu. Bongo hamna GIF ningekuwekea kukuonyesha kosa la refa. Rafu ilichezwa mbali na eneo hatari
GIF zipo Telegram tunazitumia sanaaa.
Nenda Azam tv Facebook washaweka tayari ulete ukiona clip haikupi support edit kabisa
 
Offside ile nayo ya Nchimbi nayo mwamuzi huwezi mlaumu?Wakati Nchimbi hakuwa offside.

Ndio timu yetu haikucheza mpira mzuri lakini refa katunyonga mara mbili.
Kwani offside si nimesema kachapia? Au umejibu kihisia kuliko uhalisia wa maandishi?
 
Kwa mwaka huu wa fedha, wazee wa kujimwambafai, SSC wamesajili wachezaji wa nje wengi sana kwa mantiki ya kuongeza ufanisi katika timu.

Lakini kitu kimoja naona wazee hawa wa kujimwambafai wanajisahau ni kushindwa katika bench la ufundi kuwatumia hawa wachezaji wanaosajiliwa kila siku.

Mchezaji kama Kahata, Deo Kanda, Kagere, Ajibu, Beno na wengine bado hawajaweza kutumika vizuri. Na katika hili ni vyema mkaacha kumpangia Kocha na kuwa na influence juu ya nani acheze au asicheze.

Kocha aone mwenyewe uwezo wa wachezaji na awapange based on their abilities. Haka katabia kakumpangia Kocha I am told kapo sana pale Msimbazi.

Aidha, kwa upande wa Goli kipa nina shangaa na nitazidi kuendelea kushangaa kwa Mchezaji kama Aishi Manula kuendelea kuwa goli kipa namba moja wa wazee wa kujimwambafai.

It gives me a thought as in why huyu kijana Beno, goli kipa namba mbili wa Simba ni moja kati ya magoli kipa bora sana ambao benchi la ufundi la Simba limeamua kuendelea kumuweka Kando na kuendelea kumchezesha Manula ambae uwezo wake unatia mashaka sana sana sana.

Na hata kina Matola waliliona hili na kuamua kumchukua Kaseja aliyesaidia sana Taifa Stars kupiga japo hatua chache mbele.

Kijana Huyu wa kipogolo amekuwa akifungwa magoli ya kizembe ( excuse me for my language) mara nyingi na ninashindwa kuelewa kuna shida gani katika bench la ufundi kiasi cha kushindwa kuliona hili.

Kijana Beno aliyefanya kazi nzuri sana kule Msumbiji katika hatua za awali kabisa za michuano ya Klabu Bingwa Africa ambapo aliweza kulinda lango lake vyema pamoja na mikiki ya wazee wa Msumbiji.

Kadhalika, marudiano yaliyopigwa taifa na wazee wa kujimwambafai kutolewa nje ya michuano hiyo huku Aishi Manula akiwa goli kipa katika mechi hiyo, na kama kawaida yake aliitia hasara SSC ambayo mpaka leo bado mashabiki wa SSC hawaamini katika yale yaliyotokea taifa.

Naendelea kusisitiza tena, SSC wazee wa kujimwambafai wasipoliangalia hili kwa makini basi ipo siku watalia kilio cha mbwa koko, wuu wuu wuu.

kwasababu goli kipa mwenye uwezo yupo kwanini hapangwi? mnamuweka mtu ambaye hayupo attentive kwenye mipira ya adhabu ndogo ndogo tu, non sense.

Benchi la ufundi kuna shida gani?msikimbilie kufanya mausajili tu bila ya kufanya allocation vyema ya wachezaji wenu;

Fanyeni usajili wa goli kipa wa maana; tokeni kwenye hiyo comfort zone yenu; mpira ni biashara na ni kazi kama kazi nyingine. Hapana mchezo mchezo.

Mnatumia nguvu sana kwenye mausajili usajili bila ya kuwa na strategy ya ku utilize hizo man power zenu.

Manula anatakiwa awe anaingia Sub; you guys need to accept this bitter truth kama kweli mnataka changes na kuweka fantasy pembeni. Otherwise; the struggle will be real.

Mwisho, mkitaka kufika mbali hakikisheni safu ya ulinzi inakuwa imara huku mkiweka golikipa mwenye weledi na uwezo na anayetambua thamani ya kazi badala ya kuendelea kutumia wachezaji na magolikipa wanaoshinda kwa waganga kupata nafasi.
Lazima mu create ushindani wa golikipa; yaani mtu asijimilikishe nafasi, matokeo yake ni uzembe katika kazi.

Hakuna uchawi katika mpira, ni kujitahidi kufanya kazi.

PERIOD.
————————-
On date, 4th January 2020.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom