Wabongo kitu pekee tunacho weza kufanya kwa weledi wa hali ya juu basi huwa ni KULALAMIKA, KULIA LIA na KUKOSOA
Tz hakuna kiwanda cha nguo, viatu, simu, kompyuta, simu, tv, radio nk nk....... Lakini wanao leta hizo bidhaa ambazo ni muhimu na za lazima kwenye maisha unawaita HAWANA UMUHIMU WOWOTE
Badala tuchangamkie fursa ya kujenga viwanda sisi tunalia lia eti katiakoo hai hamasishi ukuaji wa viwanda Tz
Sasa sijui ulitaka Chalamila apige marufuku uagizaji bidhaa nje?
Mkuu swala la uchumi halipo hivyo, nchi inanunua kwa wingi nje bidhaa ambazo haizalishi
Kama tunataka hivyo tujenge kwanza viwanda vyetu
BTW unajua ni kiasi gani serikali inakusanya kwa mwaka pale kariakoo?
Unadhani ni kwa nini kariakoo ni “mkoa maalumu”wa kikodi?
Angalia tu sakata la sukari lilivyo
Serikali inalinda viwanda vya ndani kwa kudhibiti uagizaji sukari nje lakini bado viwanda vinasuasua tu
Ukweli ni kwamba Kariakoo ni MUHIMU sana kwenye kuchangia pato kwasababu hatuna viwanda mbadala vya kuzalisha bidhaa zinazoagizwa
Ni kazi ngumu sana kutuelewa Wabongo huwa tunataka nini haswa