Kariakoo haihamisishi ukuaji wa viwanda vya ndani, Kariakoo ni Dumping site ambako asilimia 100 ya products zinazo uzwa pale ni Made in nje.
Ni wajinga pekee ndio wanaoweza kuamini kwamba soko lenye asilimia 100 ya bidhaa za nje ya nchi lina umuhimu sana kwa uchumi wa nchi kuliko, Kilimo, kuliko Madini, kuliko Uvuvi na kulilo utalii.
Kariakiakoo ni makao makuu ya kituo uapnde wa Tanzania cha kupromote products za nje hasa kupromote viwanda vya China na kupelekea China kutoa ajira zaidi kwa wachina.
Huwa nashangaa sana tunapo aminishwa kwamba kariakoo ndio roho ya uchumi wa nchi, yaani sehemu inayo promote viwanda vya China inaweza vipi kuwa roho ya uchumi wa nchi?
Kariakoo ni Dumping site ya products low qualities kutoka nje ya nchi.
Kama angalau asilimia 40 ya bidhaa za kariakoo ni made in Tanzania hapo kungekuwa na logic ila asilimia 100 then wajinga sisi tunaaminishwa kwamba pale ndio uchumi wa nchi ulipo?
Vipi huko wanako enda kuchukua bishaa?
Kariakoo ni kituo moja wapo cha kuua viwanda vya ndani.
Nchi inamalizwa na siasa za kijinga sana.
Wabongo kitu pekee tunacho weza kufanya kwa weledi wa hali ya juu basi huwa ni KULALAMIKA, KULIA LIA na KUKOSOA
Tz hakuna kiwanda cha nguo, viatu, simu, kompyuta, simu, tv, radio nk nk....... Lakini wanao leta hizo bidhaa ambazo ni muhimu na za lazima kwenye maisha unawaita HAWANA UMUHIMU WOWOTE
Badala tuchangamkie fursa ya kujenga viwanda sisi tunalia lia eti katiakoo hai hamasishi ukuaji wa viwanda Tz
Sasa sijui ulitaka Chalamila apige marufuku uagizaji bidhaa nje?
Mkuu swala la uchumi halipo hivyo, nchi inanunua kwa wingi nje bidhaa ambazo haizalishi
Kama tunataka hivyo tujenge kwanza viwanda vyetu
BTW unajua ni kiasi gani serikali inakusanya kwa mwaka pale kariakoo?
Unadhani ni kwa nini kariakoo ni “mkoa maalumu”wa kikodi?
Angalia tu sakata la sukari lilivyo
Serikali inalinda viwanda vya ndani kwa kudhibiti uagizaji sukari nje lakini bado viwanda vinasuasua tu
Ukweli ni kwamba Kariakoo ni MUHIMU sana kwenye kuchangia pato kwasababu hatuna viwanda mbadala vya kuzalisha bidhaa zinazoagizwa
Ni kazi ngumu sana kutuelewa Wabongo huwa tunataka nini haswa