Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Mkuu, uchuuzi wa kitapeli si mzuri. Kwa eneo kama Kariakoo hauoni impact kwa haraka sababu watu ni wengi na kila siku kuna watu wapya wa kutapeliwa ila si jambo zuri kibiashara.Bro hujui how things work. Biashara zote dunian zinafanyika online na wakat mwingine huwez kuwa na watu wote online so unakuta una mawinga kama 50 kila mtu ana wafuasi elfu 4 tuseme na wanakuja dukan kupiga picha kuposti so ndani ya nusu saa kila Winga anakuja huyu anataka pcs 30 huyu kumi huyu 20 na wanakuja kuchukua mizigo kupelekea wateja huko walipo so yeye anapata cha juu na wewe unapata chochote kitu. Ndivyo mfumo wa biashara ulivyo dunian lazima awepo mtu wa kati anaerahisisha kazi zako ziaende. Kwa mtu ambae amesafir anajua hasa viwandani. Biashara ni agent mzee. Na hiyo ya dukan kusubirishwa ni kawaida kkoo mi tangu naanza biashara vijana wanafanya hivyo miaka hiyo we umestuka leo na hata wagen wanajua. Kwa mfano mimi biashara yangu ni groups za whatsp za wateja wangu kutoka congo zambia Zimbabwe kenya malawi Rwanda Burundi comoro msumbiji nk. So mzigo ukitoka natoa sampo store narusha kwenye whatsp kila mtu anaweka order humo humo kutoka hizo nchi na wanaingiza mizigo kwenye account yako unawatumia mizigo yao. Simpo mzee life ishabadilika kaka. Mimi naweza kuuza mizigo nikiwa hukuhuku china ikawafuata wateja walipo na wakaniingizia mpunga wangu kwenye account tu. So usikariri maisha mzee pinduka maisha na yenyewe yanavyopinduka waache wenye kibarua cha kulaumu walaumu kila mtu apigane vita vyake. Ukiona umestuka ujue kuna mwingine ni mtaji, biashara ni mchezo wa sanaa kuna wakati unafungwa na kuna wakat unafunga.
Unaweza kuwa na duka lako, ukawa na bei elekezi kwa mawinga wako wanaowaleta wateja hapo dukani. Utauza mno maana hutategemea wapitaji wapya bali wapya na wanaopita na kurudi.
Kwa wale wanaopost online na wanawapelekea wateja sawa ila kwa hawa wanaokuja na mteja dukani jitahidi uwe na bei elekezi kwa wateja wako.