Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Kariakoo hakuna machimbo tena, kwa atakayepuuza sitaongea tena

Umasikin ni mbaya sana aisee. Nyie ndio mkiona mtu kanunua range rover mnamlaumu kwa kununua gari inayotumia mafuta. Mzee ukiona unanunua kitu kwa kubagain ujue hali yako ni mbaya pambana mkuu.
Tajiiiiriii
 
Ukosefu wa ajira ndo umeleta hawa inzi saiv nchi hii ukiwa na hela unashindwa kuenjoy kwa kununua vitu vizur kisa hawa inzi wanajiita mawinga hapo kariakoo mm nilitoka bila kununua chochote nikasema hebu nipite na hapo karume yaani balaa la soko la karume kipindi hiko kabla halijaungua lilikuwa mbada wa kariakoo na hao inzi hawakuwepo.Saiv karume kumejaa vibaka wanaosumbua watu, unakuwa unanunua huku unalinda mali mfukoni maana sio kwa hao nzi waliokuzunguka.Napo pia niliishia kushangaa nikapanda gari nikaondoka🤗.Mjini daslam kumevamiwa vijana wakimaliza chuo hawataki kurudi makwao. Goli moja mawinga 7 au 8 yaani ni viroja🥱

Alafu ni nani aliyewaambia kuwa mm nimetoka nyumbani nakuja mjini alafu ww inzi mmoja unajifanya tour guide( dalali). Nchi imechafuka madalali stendi, madalali masokoni kwenye nyumba na viwanja ndo balaa ni inzi everywhere🥴
Wanakela kinoma, ukiingia sokoni tu hao washakufata. Mimi nikiona wananifata huwa nasimama nawageukia na sura ngumu kama undertaker halafu nawauliza vipi. hao wanakaa pembeni wenyewe.

Macho ya kuona bidhaa ninayo sasa ndio nini kufatwa fatwa
 
Mi niko kkoo huu ni mwaka 25 mkuu na kwasasa soko linaendeshwa na mawinga. Usipokubali mabadiliko ni kwamba umejiandalia kifo. Na kwa taarifa yako kkoo inategemea zaid wateja wa nje ya nchi sio ndani. So wewe endelea kuishi kwa kukariri maisha wakat wenzio wanavuka ukija kustuka uanze kuilaumu serikali. Maisha lazima ule na watu babu kama unataka kwenda mbali. Kama unataka kwenda karibu kula mwenyewe. Mi nawatumia winga tangu naanza biashara kkoo na wao wanakula na mimi natembea. Winga wananipa idea mipango na sote tunapata maisha yanaenda. We jifanye boss ubaki kuitwa mwenye duka milele. Ctaki huo upuuzi
Hao wateja wa nje mtawakimbiza kwa bei kubwa za mawinga.
Wataenda nchi jirani au maeneo mengine Kama huko Mbagala, Tandika na Mikoani.
Dunia utandawazi watapata taarifa za masoko ya bei nafuu. Msije kuwalilia serikali wameharibu soko lenu kumbe tatizo wenyewe.
 
Me nataka winga wako umlipe mshahara atafute wateja walioko majumbani
Yaani mtu kajileta dukani kwako kununua simu ambayo unauza labda laki 4 wewe unamweka mteja wako midomoni mwa winga wanampiga laki 7 Bado unaona ni raha
Wafanyabiashara wakimataifa watawahama wawe wanachukua mizigo miji mingine
Sure mkuu, mawinga watafute wateja uko mtaani na majumbani, sio mtu unaenda mwenyewe sokoni halafu unafatwa fatwa na kundi la watu kama vile hauna macho ya kuona bidhaa zinazouzwa
 
Mi niko kkoo huu ni mwaka 25 mkuu na kwasasa soko linaendeshwa na mawinga. Usipokubali mabadiliko ni kwamba umejiandalia kifo. Na kwa taarifa yako kkoo inategemea zaid wateja wa nje ya nchi sio ndani. So wewe endelea kuishi kwa kukariri maisha wakat wenzio wanavuka ukija kustuka uanze kuilaumu serikali. Maisha lazima ule na watu babu kama unataka kwenda mbali. Kama unataka kwenda karibu kula mwenyewe. Mi nawatumia winga tangu naanza biashara kkoo na wao wanakula na mimi natembea. Winga wananipa idea mipango na sote tunapata maisha yanaenda. We jifanye boss ubaki kuitwa mwenye duka milele. Ctaki huo upuuzi
Muongo!
 
Back
Top Bottom