Karibu asilimia 70% ya maswali ya baadhi ya waandishi wa habari Bongo ni ya ovyo; nina wasiwasi na ubora wa vyuo vya habari

Karibu asilimia 70% ya maswali ya baadhi ya waandishi wa habari Bongo ni ya ovyo; nina wasiwasi na ubora wa vyuo vya habari

Bongo hakuna waandishi wa habari kuna wavamia fani.
 
Hakuna namna ndio upande tuliochagua ndio maana hata ukiangalia kwenye Baraza unakuta watu wa hivyo hivyo, maendeleo ni process ndefu yenye hatua nyingi ngumu..
Yaan watu wa hovyo ndiyo tunaowategemea kutuvusha
 
Niliachana na media za Tanzania yapata mwaka wa Saba Sasa nilihamia bbc, CNN, Aljazeera, CBS, fox news , NHK Japan ,nk
Tbc,itv,chanel 10, zilishanishinda kitambo sana
 
Nimefuatilia mahojiano (interview) nyingi za waandishi wa habari Tanzania!

Wengi wao wanamaswali ya hovyo na kipuuzi kuliko mahitaji ya jamii inachohitaji kujulishwa!

Maswali yao mengi yapo kwenye mlengo wa taharuki kwamba Flani kasema vile na vile almradi tu jambo lionekane la kuishangaza jamii.

Mfano: Kesi ya Feisali na TFF wanahabari wanaonekana kuuliza upuuzi upuuzi mwingi mara ooh tumesikia mama akilalama kuwa mwanae alilishwa ugali na sukari. Je, Feitoo alipokuwa yanga alikula ugali na sukari ya mtibwa? au alilambishwa mayonaiza?

Hivi kwrli Maswali ya sampuli kama hiyo yanamsaada gani katika jamii kama siyo ubovu wa wanahabari wetu?

Huenda wanaohojiwa wanakerwa lakini wanayavumilia tu! Hayana tija kabisa!

Natamani kuona wanahabari wenye uwezo wa kuhoji kila swali lenye tija angalau 80% ya ujumbe
Waandishi wengi wa Sasa hawana taaluma ya uandishi kabisaa ukiingia kwenye hivi vionline tv ndiyo bure kabisaaaa

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom