Karibu nyumbani Rais Samia, siku 10 nje ya nchi zimelijaza Taifa mapene ya maendeleo

Karibu nyumbani Rais Samia, siku 10 nje ya nchi zimelijaza Taifa mapene ya maendeleo

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
652
Reaction score
443
Karibu nyumbani Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Siku 10 ulizofanya ziara Ufaransa na Ubelgiji, tayali tumepata Fedha nyingi sana kwenda kuongeza nguvu kwenye sekta mbalimbali za maendeleo kama reli na usafiri wa mwendokasi, kilimo, Uchumi wa Buluu, masuala ya Bahari na maendeleo endelevu.

Tayali siku 10 hizi pale Ufaransa na Ubelgiji tumepata Fedha Trilioni 1.15 za Kamisheni ya Ulaya kwenda kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo, EURO Milioni 178 za Ufaransa (zaidi ya Bilioni 464) kwa ajili ya kugharamia awamu ya 5 ya mradi wa mwendokasi Dar es Salaam kuelekea Gongolamboto, EURO Milioni 80 (Bilioni 208.6 kwa ajili ya kuboresha kilimo na EURO Milioni 1 za Shirika la Maendeleo-Ufaransa kwa ajili ya shughuli zingine nyingi za maendeleo. Yote haya yanakwenda kwenye maendeleo.

Tayali siku 10 hizi umekutana na Viongozi wakubwa wa Mataifa makubwa kama Rais wa Ufaransa Bwana Emmanuel Macron, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bwana Charles Michel, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Bwana Alexander De Croo pamoja na Viongozi wengine wengi wa Taasisi kubwa za Kimataifa, Wafanyabiashara wakubwa wa Ufaransa na kadhalika na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji na kufanya biashara na Taifa letu. Hii ziara imelipa sana sana sana kwa Taifa. Sasa, ni muda wa maendeleo.

Bwanku M Bwanku
[email protected]

IMG-20220220-WA0020.jpg
 
Tuambiwe tu tunazilipaje hizo maana ni mkopo.
 
Yani tumekuwa Kama tumeolewa na mabeberu kila siku wanatupa hela za matumizi kwa njia ya msaada au mkopo, muda c mrefu tutaanza kuliwa na sie
 
Tuache kuwa wapuuzi kwamba huko alikokwenda alikuwa na shamba amevuna??, Mkiwa mnamsifu muulizeni namna ya ULIPAJI wa hizo pesa.
Nakazia
Dawa Ya Deni Ni Kulipa
 
  • Thanks
Reactions: Exy
Yule mzee alikuwa mshamba sana! Alikuwa akiwatukana mataifa wahisani kwa kuwaita mabeberu wakati huohuo anawakopa kimyakimya, matokeo yake wakawa wanampa masharti magumu ikiwa ni pamoja na riba kubwa. Wakati huo huo anadanganya Taifa kuwa anatekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani! He deserved to pass away!

YESU NI BWANA
 
Yule mzee alikuwa mshamba sana! Alikuwa akiwatukana mataifa wahisani kwa kuwaita mabeberu wakati huohuo anawakopa kimyakimya, matokeo yake wakawa wanampa masharti magumu ikiwa ni pamoja na riba kubwa. Wakati huo huo anadanganya Taifa kuwa anatekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani! He deserved to pass away!!!!!


YESU NI BWANA
Tanzania Ni Tajiri
Tunajenga Miradi Mikubwa Kwa Pesa Zetu
Tuchape Kazi Pesa Zipo Ndugu Zangu
Jiwe, Chuma, Mzilankende Mnyago, Ngosha
Haa Huyu Baba Jamani Tulipatikana Mchana
 
Mama kwa kweli anajitahidi. Hizo hela zisimamiwe vizuri tu kama zile za madarasa. Kwenye kilimo ingetakiwa iwe hata zaidi ya euros 200.
 
Magufuli, kwa miaka yake 5 ya utawala, aliwezaje kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati na kuboresha huduma za jamii bila kwenda kwa wenye mapesa kuomba?
 
Tuache kuwa wapuuzi kwamba huko alikokwenda alikuwa na shamba amevuna??, Mkiwa mnamsifu muulizeni namna ya ULIPAJI wa hizo pesa.
Hawa washezi wanakere sana, utadhani sio matanzania..yamejaa unafiki tu..eti kufurahia mikopo wakati nchi inaendelea kujiingiza kwenye mtego wa mabeberu kila uchwao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwamba wewe wahukumu kuwa alistahili kufa? Wewe ni Mungu?

Ilikupasa kusema Mungu atende kulingana na mapenzi yake
 
Wakati kiongozi anakopa au anachukua misaada wakati wa utawala wake hakiongelewi kitu ila anapotoka madarakani

Ni sawa kupokea ila kuna maswali yakujiuliza katika ufahamu wa kawaida tu, kwamba mtu anakupa trillion 1.15 ukaendeleze miradi ya maendeleo nchini kwako ikiwa yeye hana matumizi na fedha hizo?

Haya tunajiuliza tena mtu akupe billion 464 bila manufaa yeyote kwake ispokuwa ni kukuletea maendeleo nchini kwako?

Haya unapokea billion 208.6 kutoka kwenye taifa la ulaya bila kujiuliza wao wanamipango gani na fedha hizo kwako?

Ni muda wa kuamka kifikra na kujua tunachokifanya tunapokwenda na kutanguliza uzalendo kwaajil ya Tanzania ya leo na kesho, hata kama tunafahamu hatutoishi milele.

Mtu hutoa kitu akitegemea kupokea kitu hakuna cha bure katika uchumi wa dunia ya sasa.
 
Yule mzee alikuwa mshamba sana! Alikuwa akiwatukana mataifa wahisani kwa kuwaita mabeberu wakati huohuo anawakopa kimyakimya, matokeo yake wakawa wanampa masharti magumu ikiwa ni pamoja na riba kubwa. Wakati huo huo anadanganya Taifa kuwa anatekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani! He deserved to pass away!!!!!


YESU NI BWANA
Wenzio waliombwa waweke mikopo bungeni wakashindwa,huo wa kukopa mikopo ya biashara ni uhuni wenu tu hakuna kitu Kama hicho, magu alikuwa akili kubwa nchi hii hajawahi tokea, na hii Vita mnayopigana na marehemu hamtashinda endeleeni kuteseka hakuna namna.lbd hiyo ya kula urefu wa kamba.
 
Nakazia
Dawa Ya Deni Ni Kulipa

Sawa kuwa dawa ya deni la MPEMBA ni kumlipa ; sasa siku Mpemba akikuchukulia mkeo kwa kushindwa/kusuasua kulipa utamlaumu?
Samia anahangaika kukopa huku wakina January wanaingia mikataba ya mabilioni ya $$$$ bila kupepesa macho!!! Tatizo mama liko kwenye matumizi mabaya ; huwezi kujaza maji kwenye ndoo yenye TOBOOO!! Utawaua wadanganyika na hizo TOZO ili kulipia hiyo madeni yako.
 
Magufuli, kwa miaka yake 5 ya utawala, aliwezaje kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati na kuboresha huduma za jamii bila kwenda kwa wenye mapesa kuomba?
Alikuwa anawatuma Mahiga na Kabudi
 
Back
Top Bottom