DOKEZO Kashfa kubwa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kanisa latumika kuwauzia mashamba hewa waumini wake. Ekari feki 15,000 ziliuzwa

DOKEZO Kashfa kubwa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kanisa latumika kuwauzia mashamba hewa waumini wake. Ekari feki 15,000 ziliuzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Idara ya usalama wa kazi zake ni zipi? Tz ni taasisi gani unahusika na uchunguzi wa wizi mkubwa na kutakatisha fedha?
 
9e99fabbb328336ce3be874d3c30ac2d.jpg
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani limeingia kwenye kashfa kubwa ya utapeli baada ya makanisa yake ya Kijitonyama, Salasala, Mwenge, Ubungo na Mbezi Beach kuwauzià waumini wake mashamba feki yaliyopo Bagamoyo.

Mashamba hayo yenye zaidi ya heka 15,000 yalikuwa yakiuzwa kwa shilingi laki tano na sitini elfu kwa heka ambapo heka zote zilizopangwa kuuzwa ziliuzwa na baadhi ya waumini wengine hadi leo hawajawahi kupewa wala kuonyeshwa mashamba yao.

Malipo ya mauzo ya mashamba hayo yalifanyika kupitia account za kanisa hilo, kumbe ardhi inayouzwa ni mali ya Ranch za Taifa huku kanisa hilo likijua fika uhuni huo.

Katika kijiji cha Fukayose, Ranch imesema itaachia heka mia tu kwa kijiji. Kwenye kijiji cha Fukayose Ranch ina heka 3000.

Heka nyingine zimesambaa kwenye vijiji mbalimbali wilayani Bagamoyo.


View attachment 2639510
Hataree
 
Unaongea hisia zako na mahaba kwq kanisa la wapigaji
Wewe unaonekana una CHUKI KUBWA na KKKT

KKKT kwa ninavyowajua hawawezi kufanya uzembe kama huo, labda waliouziwa kuna terms hawakuzifuata vizuri
 
Duuh yalikuwa fake yale mashamba na watu wameyanunua bwana

Washarika wa Ubungo tujuane kwa Mch Oscar Mlyuka
Mpendwaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mambo ya Fukayose nawe yalikupata?
 
Kwa sasa madhehebu/makanisa yasiyofanya biashara ni machache sana sema hii ya viwanja bado haijawa maarufu.

BTW:Labda nia ilikuwa nzuri ila wao wenyewe wakaingizwa mjini na akina Juma Kasangu.

 
Mpendwaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mambo ya Fukayose nawe yalikupata?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hayajanipata auntie sasa sijui ki kweli au vipi woiii roho ilikuwa inasita sanaaa kila nikitaka kuingia inakubali na inakataa
 
Apo inaonekana ata kanisa walikua hawajui,huo ukanda eneo la ranch ya taifa ni kubwa,wangemleta surveyor wa serikali kwanza ,kuwajulisha Kama eneo lote ni salama ,au ranch imepitia
 
Back
Top Bottom