Tukizikisikia tunafaidika na nini? Watanzania tunajifariji sana, sijujua kwanini, yaani kutajwa ufisadi na hamna hatua zozote zitakazochukuliwa kwetu raha,tuna enjoy..Enzi za utawala wa jiwe habari kama hizi zilikua zinaminywa .
Hii itakuwa 6+4=10Hii awamu ya 6=Awamu ya 4.
Wao ni kula, kula, kula mpaka wavimbiwe. Awamu hii Ina failure leaders kuliko awamu zote kuwahi kutokea Tanzania.Ongezeni kusifu na kuabudu.
WAZIRI YUPO NAIBU WAZIRI YUPO KATIBU MKUU YUPO ni mwendo wa KULA kwa UREFU wa KAMBA ZAOKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII imebaini matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Bilioni 375 zilizopangwa kutumika kupima ardhi badala yake asilimia kubwa zimetumika kufanyia semina na kulipana posho za uratibu.
(b) Semina kuhusu Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi.
Mheshimiwa Spika, semina hii ilitolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi kwa lengo la kuwajengea wajumbe uwezo juu ya mradi huu ambapo Kamati ilielezwa kuwa Serikali imepata mkopo kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Kimarekani Milioni 150 sawa na Shilingi Bilion 375 utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano (2022/2023 hadi Juni, 2027). Aidha, Kamati ilielezwa kuwa mradi huu unalenga kuimarisha usalama wa taarifa za ardhi, kuimarisha miundombinu ya upimaji na kujenga majengo ya Ofisi
Mheshimiwa Spika, matarajio ya Wajumbe wa Kamati ni kwamba sehemu kubwa ya fedha ingeelekezwa kwenye mipango ya matumizi ya ardhi ambayo imeonekana kuwa ni suluhisho la migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali nchini hasa wakulima na wafugaji lakin hali halisi inaonyesha kwamba ni Asilimia 1 tu ya fedha zote ndiyo itaelekezwa kwenye zoezi hilo. Lakini kinyume chake fedha nyingi zimeelekezwa katika kutekeleza mambo mengine kama vile uratibu wa mradi.
Mheshimiwa Spika, Kamati haioni tija katika mradi huu kwa kuwa haugusi kwa kiwango cha kutosha maeneo yanayolenga kutatua migogoro ya ardhi nchini. Aidha, utekelezaji wa mradi huu ungeweza kutekelezwa kwa ufanisi endapo wangeiwezesha Tume ya Mipango ya Ardhi ambayo imekuwa ikitekeleza majukumu yake ya upangaji kwa ufanisi; hata hivyo ufinyu wa bajeti umefanya ishindwe kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Mathalani hadi kufikia Desemba 2022 ni vijiji 2,678 kati ya vijiji 12,319 vilivyopo nchini ndio vimepangiwa matumizi ya ardhi.
MATUMIZI YA HOVYO KABISA MH.RAIS FUKUZA WAZIRI NA NAIBU WAKE NA KATIBU MKUUBUNGENI: Mbunge Hawa Mwaifunga amesema Wizara ya Ardhi imekopa Zaidi ya Tsh. Bilioni 345, bila Kamati kuwa na Taarifa ya Mkopo huo na kuhoji Matumizi na vipaumbele vya Wizara.
Mkopo huo umeidhinishwa kwa matumizi ya Upimaji wa Vijiji 250 kwa Miaka 5 kati ya zaidi ya Vijiji 9,000 vinavyopaswa kupimwa, wakati Tume ya Upangaji wa Ardhi waliomba Tsh. Bilioni 10 kupima Vijiji 600 kwa Mwaka.
Miongoni mwa Matumizi ya Mkopo huo, Bilioni 5 zimetengwa kwa ajili ya Semina, Uratibu zaidi ya Bilioni 40, uboreshaji wa Ofisi za Wizara, Ujenzi wa Ofisi ya Kila Mkoa na Matengenezo ya Magari ya Wizara.
Wako bize kupaka masizi makaburi. Wakija kuamka mchwa wameshatengeneza bonge la chuguuKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII imebaini matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Bilioni 375 zilizopangwa kutumika kupima...
Nimeipenda Hiyo Mbuzi wa bwana Kheri shamba la bwana Kheri yote kheri tu !! Nakumbuka Marehemu Kenyatta aliwaambiaga watu wake Nyati nimeishika mapembe kamueni maziwa mkishindwa shauri yenu !Tukizikisikia tunafaidika na nini? Watanzania tunajifariji sana, sijujua kwanini, yaani kutajwa ufisadi na hamna hatua zozote zitakazochukuliwa kwetu raha,tuna enjoy..
Wakati mbuzi wa Bwana Kheri shamba la Bwana Kheri yote Kheri.
Kumbuka Rizmoko, mtoto pendwa wa Msoga yupo ndani ya nyumba..
HahahNimeipenda Hiyo Mbuzi wa bwana Kheri shamba la bwana Kheri yote kheri tu !! Nakumbuka Marehemu Kenyatta aliwaambiaga watu wake Nyati nimeishika mapembe kamueni maziwa mkishindwa shauri yenu !
Huyo ndo alikuwa mwizi. Alimpiga kabari mswahilina flani ofisini mwake baada ya kumkatalia rushwa.Aridhi aliiwezea lukuvi hao waliopo sasa hasa rizi1 ni wezi wa kutupa.
Pale dalali wa ARDHI anapopandishwa hadhi kuwa Waziri aitunze ARDHI 😳😳😳Ridhiwani atabakiza mifupa mitupu hapo wizarani