Kashfa kubwa Wizara ya Ardhi: Bilioni 375 zatumika kugharamia semina na uratibu

Kashfa kubwa Wizara ya Ardhi: Bilioni 375 zatumika kugharamia semina na uratibu

Kika mtu amepewa nafasi ajisevie. Hebu tuone;

1.January alikwapua bilioni 300.. kwa kutengeneza kampuni ya kihindi ambayo hatuijui na kusema kaipa tenda.

2. Nape alipewa billioni kadhaa kwa ajili ya anuani ya makazi ambapo tunaona nguzo za mitipori na vibao vya kuchora kwa wino.

3. Ridhwani nae kapewa billioni hizo..afanyie mambo yake. Kweli kufanya kazi na mwanamke bogus raha sana. Maana aghalabu mwanaume mwenzio akiwa bogus unaweza kumuogopa kwa sababu ya manhood yake.

Kuwa na heshima na mamlaka.
 
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII imebaini matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Bilioni 375 zilizopangwa kutumika kupima ardhi badala yake asilimia kubwa zimetumika kufanyia semina na kulipana posho za uratibu.

(b) Semina kuhusu Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi.

Mheshimiwa Spika,
semina hii ilitolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi kwa lengo la kuwajengea wajumbe uwezo juu ya mradi huu ambapo Kamati ilielezwa kuwa Serikali imepata mkopo kutoka Benki ya Dunia wa Dola za Kimarekani Milioni 150 sawa na Shilingi Bilion 375 utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano (2022/2023 hadi Juni, 2027). Aidha, Kamati ilielezwa kuwa mradi huu unalenga kuimarisha usalama wa taarifa za ardhi, kuimarisha miundombinu ya upimaji na kujenga majengo ya Ofisi

Mheshimiwa Spika,
matarajio ya Wajumbe wa Kamati ni kwamba sehemu kubwa ya fedha ingeelekezwa kwenye mipango ya matumizi ya ardhi ambayo imeonekana kuwa ni suluhisho la migogoro ya matumizi ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali nchini hasa wakulima na wafugaji lakin hali halisi inaonyesha kwamba ni Asilimia 1 tu ya fedha zote ndiyo itaelekezwa kwenye zoezi hilo. Lakini kinyume chake fedha nyingi zimeelekezwa katika kutekeleza mambo mengine kama vile uratibu wa mradi.

Mheshimiwa Spika, Kamati haioni tija katika mradi huu kwa kuwa haugusi kwa kiwango cha kutosha maeneo yanayolenga kutatua migogoro ya ardhi nchini. Aidha, utekelezaji wa mradi huu ungeweza kutekelezwa kwa ufanisi endapo wangeiwezesha Tume ya Mipango ya Ardhi ambayo imekuwa ikitekeleza majukumu yake ya upangaji kwa ufanisi; hata hivyo ufinyu wa bajeti umefanya ishindwe kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Mathalani hadi kufikia Desemba 2022 ni vijiji 2,678 kati ya vijiji 12,319 vilivyopo nchini ndio vimepangiwa matumizi ya ardhi.
Huyo Mabula inasemekana kuwa yeye ndiyo mmiliki wa ghorofa inayojengwa maeneo ya Nyasaka,Maduka Centre jimboni kwake Ilemela.Huo ukwasi anautoa wapi?
 
Mambo kama haya ndio yanatakiwa mh.Rais kuchukua hatua,Kila siku nasema Mabula ni sukuma gang ambae anacchukua chake mapema Kwa sababu huenda asirudi bungeni next time..

Fukuza Waziri na Katibu Mkuu then wakalipe hizi pesa
Na yule Mtoto wa Born town mbona humsemi?kwa vyovyote vile yule Mwana mfalme lazima yeye ndiyo anatucgezea aya Mabreka.
 
Unapompa Ridhwan uongozi usilalamike ukiibiwa.

Kama alishawai muuibia baba yake wakati ule akiw waziri wa mambo ya nchi, unategemea nini kwenye mali ya umma..........atazipiga tu.

"KAZI YA MIKONO YETU"
Wana mkabidhi fisi bucha alafu wanalalamika kwamba nyama imepungua!!
 
Pale dalali wa ARDHI anapopandishwa hadhi kuwa Waziri aitunze ARDHI [emoji15][emoji15][emoji15]

Tusubiri
Baba yake naye analazimisha wakuu wa mikoa wampe ardhi kuanzia hekari 500 eti za kujenga matawi ya UDSM,hekari zote hizo za nini?kama siyo kutengeneza mazingira ya kutupiga kwenye upimaji!
 
Kika mtu amepewa nafasi ajisevie. Hebu tuone;

1.January alikwapua bilioni 300.. kwa kutengeneza kampuni ya kihindi ambayo hatuijui na kusema kaipa tenda.

2. Nape alipewa billioni kadhaa kwa ajili ya anuani ya makazi ambapo tunaona nguzo za mitipori na vibao vya kuchora kwa wino.

3. Ridhwani nae kapewa billioni hizo..afanyie mambo yake. Kweli kufanya kazi na mwanamke bogus raha sana. Maana aghalabu mwanaume mwenzio akiwa bogus unaweza kumuogopa kwa sababu ya manhood yake.
Si CCM wenzio, unalia Lia Nini Sasa?

Alafu miaka 60 ya uhuru Marais wanaume wangapi? Miaka yote hiyo ufisadi wa kutosha kwani walikuwepo wanawake??

CCM ni mafisadi awe mwanaume au mwanamke so msiweke lawama kwenye gender as if tukiwapa Urais hao wanaume Kuna kitu kitabadilika.
 
Ni kama Serikali na CCM wamejaa majizi watupu, wanatofautiana kwenye viwango. Maana si mawaziri, si wakuu wa mikoa, si wakuu wa wilaya, si polisi, si majaji, kila mmoja ni mwizi.
 
Tunatarajia Ofisi za mikoa za wizara ziwe na ubora kama zilivyo mahakama kuu vituo jumuishi, hata kama jengo si kubwa, lakini ubora wa vituo jumuishi vya mahakama ni kiboko.

Naunga mkono, wizara hii ikifanyiwa uwekezaji, Kodi ya ardhi ni matrilioni kwa mwaka.
Wizi mtupu, kiwanja/nyumba moja kodi kibao, TRA, HALMASHAURI, MKOANI kote huko unalipa kodi kwa kitu kilekile.
 
BUNGENI: Mbunge Hawa Mwaifunga amesema Wizara ya Ardhi imekopa Zaidi ya Tsh. Bilioni 345, bila Kamati kuwa na Taarifa ya Mkopo huo na kuhoji Matumizi na vipaumbele vya Wizara.

Mkopo huo umeidhinishwa kwa matumizi ya Upimaji wa Vijiji 250 kwa Miaka 5 kati ya zaidi ya Vijiji 9,000 vinavyopaswa kupimwa, wakati Tume ya Upangaji wa Ardhi waliomba Tsh. Bilioni 10 kupima Vijiji 600 kwa Mwaka.

Miongoni mwa Matumizi ya Mkopo huo, Bilioni 5 zimetengwa kwa ajili ya Semina, Uratibu zaidi ya Bilioni 40, uboreshaji wa Ofisi za Wizara, Ujenzi wa Ofisi ya Kila Mkoa na Matengenezo ya Magari ya Wizara.

Heri wanaokula kuliko wanaotupa
 
Nchi inahitaji KATIBA MPYA ili iweze kutoka kwenye mkwamo huu, shughuli za maendeleo zinachukua miaka mingi kukamilika kwasababu ya BAJETI ZA HOVYO zinazolenga kunufaisha viongozi na familia zao

Bajeti.PNG

Uongozi.jpg
 
Kika mtu amepewa nafasi ajisevie. Hebu tuone;

1.January alikwapua bilioni 300.. kwa kutengeneza kampuni ya kihindi ambayo hatuijui na kusema kaipa tenda.

2. Nape alipewa billioni kadhaa kwa ajili ya anuani ya makazi ambapo tunaona nguzo za mitipori na vibao vya kuchora kwa wino.

3. Ridhwani nae kapewa billioni hizo..afanyie mambo yake. Kweli kufanya kazi na mwanamke bogus raha sana. Maana aghalabu mwanaume mwenzio akiwa bogus unaweza kumuogopa kwa sababu ya manhood yake.
Inasikitisha sana, hakuna Rais pale
 
Oh rizone ,ongea na mshua ohooo rizone!!

Unategemea nini sasa wakati makontawa ndiyo wapo kwenye hiyo wizara ohoo rizone ongea na mshua.
 
Back
Top Bottom