Naombeni mniambie mimi sijawahi kukutana na mamba wala chatu ila nahitaji kujua je ukikutana na Hao Wanyama.
Assume una upanga mkali yupi ukipambana naye Shambani huko ng'anya yake sio ndogo.
Yaani yupi ukijiingiza kwenye mfumo wake wa mtego pambano lake atakuzidi kirahisi na yupi mwepesi kumshinda.
bora simba kuliko chatu na mamba. chatu ni hatari kupita watu mnavyodhani, akifanikiwa kukukamata tu hata uwe na nguvu gani hutoki, anakubana mbavu muda si mrefu umeshanyooka. mamba ana nguvu kwenye maji za ajabu, na ule mdomo akiufumba baada ya kukung'ata, hata jeki inahangaika kuufunua. ndizo nguvu Mungu aliwaumba nazo. simba ni hatari ila ana akili, huwa anajihami pia, unaweza walau kusavaivu.
lakini hatari kuliko vyote tunavyojadili ni dhambi, Mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu. mauti inayoongelewa hapa ni hii ya mwili kufa, na baada ya hapo, mauti ya kutengwa na Mungu na kuunguzwa moto milele na milele. bora uuliwe na hawa wanyama ukaenda uzimani, kuliko kuuliwa na hawa na zaidi ya hapo ukaenda motoni. Neema ya Mungu imefunuliwa kwetu nayo yatufundisha kukataa mabaya, ukiona unapumua, unaongea, una afya, jua ni Neema ya Mungu, anakuvuta pengine utabadilika, Mungu anakupenda mno kuliko unavyoelewa, ameshaona hatari iliyoko mbele yako, hatari ya moto wa milele, hatari ya kifo cha kidunia pia, na anakupa nafasi pengine uokoke ili ukifa ufe katika Bwana na ukiishi uishi katika Bwana. Mpe Yesu maisha yako leo, uone kama hautabadilika, Okoka leo, kwasababu hujui lini utakata pumzi.