Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Kwahiyo kinachomuongoza mtu kufikia toba ni HEKIMA siyo pesa. Pesa haina uwezo huo, kwahiyo kumbe bora HEKIMA kuliko pesa siyo?

Mada tamu hii... kutokana na michango mizuri inayojenga sana. Hapa nilipo tu nimeishapata digrii ya kujuwa kipi ni kipi kati ya Hekima na Pesa.
 
Mtumishi,

Leo ukiita wenye mali waliozipata kwa Mungu (kwa haki) na wenye mali waliozipata kwa shetani (kwa njia haramu) wepi watakuwa wengi zaidi?
 
Hivi hekima ndio busara au kuna utofauti..
maana tafsiri yake ni wisdom ileile.

Tunakosea kuchanganya maneno: Hekima/Busara, Werevu, Akili, Elimu.

Hekima/busara ni maarifa ambayo msingi wake ni uzoefu..na haihusiani na elimu-shule....na ndio maana busara/hekima huhusishwa na umri mkubwa..

Topik hii ilipaswa kulinganisha elimu (zote rasmi na elimu mtaani) vs fedha..

Elimu na hekima kwa mbali vinataka kuingiliana lakn ni tofaut..

Kwny ulimwengu huu wa ubepari hekima ni msamiati..
 
Umechanganua vizuri sana. But what about Philosophy?


My take:
Hekima ni jinsi unavyojipresent (mode of self-presentation) kwa wanaokuzunguka unapo-interact nao.

Busara ni kauli au maandishi yanayobaki kama legacy. Hekima siyo lazima iwe kwenye form ya kauli au maandishi, ila inawezakuwa hata kwenye tabia mfano uvaazi wako. Ilhali Busara haiwezi kuwa kwenye tabia e.g. mavazi nk.
 

lugha ya kiingereza, mostly hutumia neno moja tu WISDOM kumaanisha hekima au busara

Waswahili ndio tunachanganya haya maneno kwa kudhani kwamba yanatofautiana wakt sivyo....

Ni sawa na kuyalazimisha maneno Fununu, Tetesi au Uvumi
yatofautiane.

Mimi nafikiri hekima & busara hujidhihirisha kwny decisiona making na kauli..siyo haiba ya nje kama uvaaji, kupendeza nk
 
Mtu anayevaa nusu uchi hawezichukuliwa kama ana hekima. Waadventista Wasabato 100% wana hekima katika uvaaji wao. Hekima huzaa heshima, hakuna mwenye heshima ambaye hana hekima, respect is the result of wisdom. Kwa ufafanuzi mwingine kuna uvaaji wa heshima (dress code) ambayo hiyo ndiyo hekima. Baadhi ya taasisi zinahitaji watu wenye heshima ili watunze na kuhifadhi hekima ya taasisi ambayo ndiyo identity yake, mfano pale IFM Dar na Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea kuna dress code (heshima ya uvaaji) ili kutunza, kuhifadhi na kuendeleza wakfu wa kitaasisi. Ukiitwa Ikulu leo lazima upewe sharti la uvaaji hata kama wewe ni Mmaasai. Kumbe basi hekima ambayo huzaa heshima; inahusiana na nidhamu/tabia pia.


Taswira kwa hisani ya google.
 
Kati ya hawa, nani yuko upande wa pesa na nani yuko upande wa hekima?

Taswira kwa hisani ya JF Photo Forum.
 

Mkuu unatumia nguvu mno,generation hii hutaeleweka,binafsi na familia yangu tunakushukuru Sana,UMENENA HEKIMA TUPU!!vijana Wahuniwahuni hawatakuelewa🤣🤣
 
Mkuu unatumia nguvu mno,generation hii hutaeleweka,binafsi na familia yangu tunakushukuru Sana,UMENENA HEKIMA TUPU!!vijana Wahuniwahuni hawatakuelewa🤣🤣
Ndiyo maana vijana wa leo life expectancy yao ni fupi mno kuliko wazee.

Yawezekana pia pesa zinafupisha maisha na hekima inarefusha maisha. Pesa zinaleta magonjwa sugu (Ukimwi, Pressure, Diabetes, Insomnia nk) na hekima haihusishwi na kuleta magonjwa. Pesa zimefunga wengi jela... pesa zimetenganisha udugu lakini hekima zimeunganisha na kuimarisha udugu.

Fikra ngumu hii.
 
Mkuu unatumia nguvu mno,generation hii hutaeleweka,binafsi na familia yangu tunakushukuru Sana,UMENENA HEKIMA TUPU!!vijana Wahuniwahuni hawatakuelewa🤣🤣
Mkuu,

Vijana wasiponielewa basi wakajifunze kwa Sabaya na yule wa Koromije pesa zilipowafikisha na kwamba sasa wanatamani wangelikuwa na hekima hata bila pesa.
 
Suleiman hakuwa majalala! Hilo la kwanza kabisa😅...

Sikuhizi bila hela utaishia kukoka kuni jikoni na hekima zako!
Mkuu,

Mbona Sabaya na ela zake leo anakoka kuni kwenye mafiga ya Magereza? Ela zimeshindwa kumuokoa. Mbowe naye hatujui kama ataungana naye kukoka kuni Jela Ukonga (Mungu aepushie mbali) kama ela zitashindwa kumuokoa, ni vivyo hivyo kwa mzee wa Koromije.
 
Hahahahahah
 
Aya ya mwisho rudia tena sijakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…