Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
- Thread starter
- #161
Dondoo/point imekuja kwenye msimu wa Disemba, tuchukuliane mizigo Bwashee...Wewe nae huna hekima ume anza mambo ya ukabila humu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dondoo/point imekuja kwenye msimu wa Disemba, tuchukuliane mizigo Bwashee...Wewe nae huna hekima ume anza mambo ya ukabila humu
Kweli kabisa mkuu, bila hekima hasingeamua mambo kwenye lile Bunge la wakeze ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kuliko Bunge la Ndugai.Maamuzi ya individual ni tofauti na maamuzi ya kiutawala hasa kwa ngazi kubwa kama maRais na Wafalme,ndo maaana hata Sulemani alipoomba Hekima watu wakadai kuwa kwa kuwa tayari ana mali kitu ambacho ni kweli kwa ngazi ya individual lakini alichoomba kilikuwa ni cha kitaifa na ndo maana akaomba Hekima kuwaamua watu wake.
Watu wa mwisho darasani hawakosekani kwasababu ya upumbavu wao na wewe ni mtu wa mwisho kwenye darasa hili. Ni toto tu kikuwa taacha!Hapo ni pesa tu baba, kichwa cha habari tu kimenifanya nitoe jibu maneno mengine zaidi ya hilo jibu ni upumbavu
Mwl Mwakasege aliwahi kusema akifundisha kwenye moja ya semina zake Dar kwamba "Hana uhakika kama Suleiman ameingia Mbinguni"Nadhani tunashindwa kumuelewa Suleiman na mawasiliano yake na Mungu, na tunashindwa kutofautisha mtu mwema na mtu Mwovu, Suleiman alifanikiwa kuwasiliana na Mungu kwa utu wema wake tena akiwa mfalme akaulizwa apewe nini yeye akiwa mfalme tayari anakazi ya kumuingizia kipato na mtu mwema pia kwenye kazi yake na maisha yake ndipo alipoomba hekima Ili aitumie kwenye maamuzi atakayokuwa anafanya yawe ya hekima na kuacha kuomba mabaya kama kuua maadui zake au mambo mabaya ila aliridhika na kazi aliyokuwa nayo na kuomba aongezewe hekima ndipo Mungu akambariki kwa kuwa mtu mwenye Mali nyingi kwa kuchagua kuwa mwema badala ya kuomba mambo mabaya, Sasa mtu huna kazi alafu uulizwe upewe nini alafu ujibu hekima Sasa hizo hekima ukipewa uzunguke nazo kutoa hekima bila kazi siutazeeka ukiwa masikini? Hao wakina Trump ni kweli wanamali lakini tunawapima kwa wema au ubaya wao maana sasa tunamfumo wa sheria ndiyo zinazotumika kurekebisha watu wabaya na pia tunakuwa na watu wema na watu wabaya katika maamuzi yoyote yanayofanyika katika ngazi zote hivyo watu wanatakiwa kuangalia maana yoyote yanayofanyika je yatakuwa yenye haki au wema au yatakuwa yenye chuki au mabaya tofauti ni kipindi cha Mfalme Suleiman yalitoka kwa Mfalme pekee mpaka kwa mambo ya kifamilia kitu kutenda katika wema bila kuongozwa na nguvu ya ziada kutoka ndani ilikuwa ngumu kutoa majibu ya haki ndipo Suleiman akaomba Hekima yaani kutendea watu wake Wema na siyo ubaya kwa mambo yatayokuja mezani kwake kutolea maanamuzi.
Marko.10:25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.Hiyo ni tofauti ya wema na ubaya, au watu wema na watu wabaya wakikaa pamoja nini watafanya na siyo Hekima aliyoomba Mfalme Suleiman, watu wawe na hela ila wawe wema na Hekima aliyoomba Suleiman ilikuwa ni kutenda wema au kutoa maamuzi yenye haki Sasa Kuna watu wameshindwa kutofautisha hekima ambayo ni haki ya kumtendea mtu anayestahili na maarifa au elimu ya kujielewa aliyonayo mtu.
Itakapotakiwa school fees ya watoto wako wewe ndenda kawalipie hekima zako.PUMBAFUKweli kabisa mkuu, bila hekima hasingeamua mambo kwenye lile Bunge la wakeze ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kuliko Bunge la Ndugai.
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daahh!mmecheka saanaSuleiman hakuwa majalala! Hilo la kwanza kabisa[emoji28]...
Sikuhizi bila hela utaishia kukoka kuni jikoni na hekima zako!
Ndio ukweli[emoji3][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daahh!mmecheka saana
Hivyo vinaendaga pamoja flani hiv.Ndiyo maana Mungu alimuongezea fedhaIngekuwa Mungu anawauliza vijana wa leo wachague kati ya Hekima na Fedha unadhani wangechagua kipi?
View attachment 2057925
Mfalme Sulemani akiongoza kikao cha Baraza la Wakeze. Taswira kwa hisani ya google.
Mbona una majibu kama uko kwenye hedhi? Hizo pedi ulizovaa zimetengenezwa na wenye hekima baada ya kuona madaso yanakuadhiri na visenti vyako vya kudanga.Itakapotakiwa school fees ya watoto wako wewe ndenda kawalipie hekima zako.PUMBAFU
Maxence Melo Human Rights Icon of his days alitumia hekima kuanzisha jukwaa la JF, Ruge Mutahaba alikuwa na hekima kwanza alipobuni wazo la kuwa Media Mogul, Erick Shigongo alitoka Buchosa bila nauli akijificha chini ya viti vya treni Ma-TT wasimkamate na alipofika Dar alitumia hekima kuwashawishi Wahindi kumkopesha mtaji.Sawa mkuu
Hakuambiwa achague kati ya hekima na hela apewe nini Bali aliambiwa aombe chochote kwa Mungu apewe akiwa na level ya ufalme kama ajira yake ndo Suleiman akaomba kupewa Hekima Ili aitumie kufungua mafumbo wakati wa kutoa maamuzi kama Mfalme au kutoa mashauri mema akiwa kama Mfalme kipindi hicho walikuwa ndiyo wanaoongoza kutoa dira ya Nchi iendeje na kutoa maamuzi ya kesi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia mpaka jamii yote hivyo yeye aliona akipata Hekima ataweza kufungua mafumbo ya mashauri yatakayoletwa kwake na pia kutoa ushauri yenye haki baada ya kuchambua mafumbo yanayokuja kwake kama kesi na dira ya watu wake kwa mtu mmoja mmoja, hivyo hatuwezi kufananisha hekima na hela kwasababu hakuambiwa afanye uchaguzi wa hela na Hekima ila baada ya kuomba kwa Mungu kitu chema na kilichompendeza Mungu ndo Mungu alipombariki wa utajiri mkubwa wa Kila kitu yaani watoto, wake, Mali za kuhudumia hao wake na watoto, Taifa lake kubarikiwa na Hekima yenyewe aliyotumia kwenye kazi yake au maamuzi yake.kwahiyo, hapo napata ufahamu kwamba hekima aliyoiomba Sulemani, ilikuwa ni kitendea kazi ktk ofisi yake ya Kifalme. ASANTE kwa ufahamu huo.
Lakini Mkuu, unadhani HEKIMA ni nini na ina THAMANI gani hata kuthubutu kuilinganisha na FEDHA?
Hawakuwa na hekima hao wengine ni Akili tu ila hekima hapanaKarl Marx? Plato? Socrates? Aristotle? Pythagoras? Newton?
Walikuwa makapuku wa pesa lakini walikuwa na hekima.
Sidhani Kuna watu wanahekima na pesa hawana na pia Kuna watu hawana hekima na pesa wanazo maana wamejua kuwa na nidhamu ya pesa tu wakaweza kuwa pesa, ila kwa Suleiman yeye alimpendeza Mungu na Mungu akambariki kwa Mali na asipungukiwe na Mali ikiwemo pesa.Hakuna mwenye hekima asiye na Pesa.
Hivyo vyote ni utu mbaya au mtu mbaya uliosema yaani roho ya ubaguzi na jeuri na pengine Hekima anayo ila wakati wa kufanya maamuzi akiwa na Hekima zake kabisa anajitoa fahamu kupindisha maamuzi mazuri anachagua maamuzi mabaya makusudi tu Ili roho yake mbaya ifurahi au ajinufaishe na hayo maamuzi mabaya maana Hekima ni kufungua mafumbo magumu na ukajua ukweli utatoa maamuzi gani? Yenye haki au yasiyohaki.Hekima haikai kwenye roho ya ubaguzi, udukuzi na jeuri.
Pesa haikumuharibu ila ubaya wake ndo ulimuharibi hivi kama Mungu anambariki mtu hela iweje tena hela nyingi ziwe ni tatizo? Tatizo hapo ni mtu kama mtu akiwa ni mtu mbaya na matendo yake yakiwa mabaya au mtu Mwovu tu hata akipata bahati ya kupata Mali anatumia hizo Mali kuumiza watu na kufanya roho mbaya yake kama yeye mwenyewe alivyo Mwovu, hivyo tusikatae kubarikiwa Mali nyingi kama sisi ni watu wema na Mali hizo tukazifanyia wema kama kutoa kwa wahitaji.Hekima yake ndiyo ilimfanya Mike Tyson akamuajiri, baada ya yeye Trump kupata pesa nyingi pesa hizo zikabomoa hekima yake. Kumbe pesa zinaharibu hekima lakini hekima haziharibu pesa, bora basi hekima kuliko pesa kama ni hivyo.
Kuna watu wananeema ya Mungu maana amesema anawajua waliowake tayari na hao kwa wema wao wanaoutenda hata pale wanapokosea huwa wanapewa nafasi au njia ya kutubu mpaka wanatubu na hao huwezi kujilinganisha nao maana wakikosewa Mungu huwa anawalipizia kisasi yeye Mwenyewe anaweza kuwa hata mtoto wako amechaguliwa na Mungu utaona anapenda kufanya haki, na wale wengine wengi wasiochaguliwa ila wataokolewa kwa Neema tu kulingana na matendo yao duniani kama yakiwa mema na Mungu haangaiki nao zaidi ya kuwanyuka tu pale anaona wanazidi kuumiza wake.Mwl Mwakasege aliwahi kusema akifundisha kwenye moja ya semina zake Dar kwamba "Hana uhakika kama Suleiman ameingia Mbinguni"
Tajiri maana yake ni mtu mwenye kiburi cha kujiona anaweza Kila kitu bila msaada wa Mungu yaani yeye kama yeye anajiona kama mwenye uwezo wa jambo lolote na anapofanikisha jambo Hana shukurani yoyote kwa Mungu huyo ndo tajiri na ndo ni ngumu kwake kuingia Mbinguni ila watu waliobarikiwa Mali kwa uweza wa Mungu kuwa kwao na Mali siyo kikwazo kwao kuingia Mbinguni kama wanatenda mema, Mbingu ipo kwa watenda mema wote kasoro watenda mabaya na hao matajiri yaani wenye viburi hata kama ni masikini hawana kitu kama wanatabia za utajiri au kiburi cha kujiona wao ndo Kila kitu na walijiumba wao hawana wa kumshukuru kwa wao kuubwa basi hawataingia Mbinguni.Marko.10:25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.
Hilo andiko linateta wenye pesa au? Mbona halijatoa angalizo kwa Mamajusi (wenye hekima) pia?
Askofu Desmond Tutu (just deceased)? Martin Luther King Jr? Che Guevara?Hawakuwa na hekima hao wengine ni Akili tu ila hekima hapana
Vipi Anania na Safira?Pesa haikumuharibu ila ubaya wake ndo ulimuharibi hivi kama Mungu anambariki mtu hela iweje tena hela nyingi ziwe ni tatizo? Tatizo hapo ni mtu kama mtu akiwa ni mtu mbaya na matendo yake yakiwa mabaya au mtu Mwovu tu hata akipata bahati ya kupata Mali anatumia hizo Mali kuumiza watu na kufanya roho mbaya yake kama yeye mwenyewe alivyo Mwovu, hivyo tusikatae kubarikiwa Mali nyingi kama sisi ni watu wema na Mali hizo tukazifanyia wema kama kutoa kwa wahitaji.