Wordsworth
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,191
- 3,360
Hhahaaaa lol umeshindwa kujibu hoja umeni attack na u Lumumba.Kudeal na vijana walioshiba mafunzo ya Lumumba ni kujuimiza kichwa
😂😂 sijui alitaka baba yake ndo awe raisi wa kwanza Tanzania. Yaani watu wanamchukulia Mwalimu poa.Shida ni kuwa huyo Dos.2020 ni descendants of sultan hawezi mpenda Mwalimu.
Mwalimu siyo nguzo kuu ya umaskini Tanzania. Factors zipo nyingi tu, na ukilinganisha na nchi nyingine za Kiafrika tupo well off.
Tena ninachoweza kumpongeza mwalimu ni kuweza ku maintain amani na kuepuka ukabila unayopelekea madhara makubwa zaidi.
😂😂 sijui alitaka baba yake ndo awe raisi wa kwanza Tanzania. Yaani watu wanamchukulia Mwalimu poa.
Tanzania ipo ilipo kwa sababu ya misingi mibovu ya kiuchumi iliyowekwa na mwalimu.
Caring for Africa?? Inatufaidisha nini Leo? Umeskia raia wa south Africa kuzamia bongo kutafuta maisha?? Ni Sisi ndio tunaelekea huko.
Kila unaloshika halishikiki ndani ya Tanzania, na hii ni kukuonyesha kwamba muasisi alikosa maono. Lichama lake alilolianzisha ndio hili mnaliona ilimradi balaa juu ya balaa
offcourse mwalimu ni zaidi ya madiba kwanza mwalimu mwenyewe alim coach madiba ss tamgu lini mwanafunzi ashindane na mwalimu wake ..ukisikia sisimizi kumpanda tembo ndio huko. Tz chini ya mwal. tuliwasaidia sana nchi na wapigania uhuru akiwepo madiba,..yaani mwalimu ali risk na kuifanya tz kama chuo cha kuwanoa wapigania uhuru hili lipo wazi..... historia inajua ilo...kuanzia madiba, thabo mbeki, samora masheli, and mention other in southern africa walipita hapa TANZANIA ikiwa chini ya mwalimu.
Hizo rasilimali za nchi yetu zingetumika katika kutuletea sisi wenyewe maendeleo basi pengine tungekua mbali saivi. Kazi yake ilikua ushambenga wa kujiingiza kwenye mambo ya watu wakati yake mwenyewe yanamshinda.
Hahahaaa kwahiyo ideology ikifeli inamaanisha kuwa mtu hana akili?
Kwa mantiki hii basi hata Karl Marx alikuwa hana akili.
Unaonekana una upeo mdogo sana wa kufikiri na unadaka maneno ya vijiweni.
Hata hivyo ideology yake haikufeli 100% ilikuwa na mafanikio.
Hahahaaa daaa umeniambia kitu. Bora tu niachane naye.Unatumia logic hadi naona kama inakuwa wasted kubishana na huyu jamaa [emoji23][emoji23][emoji23]
Nimekuacha na ujinga wako. Kama hujui kutofautisha kati ya uwizi na vita wewe ni level nyingine ya ujinga.Hizo ndizo fikra zenu zilovyoharibiwa na CCM, kuaminishwa kuwa Amani, Utulivu sijui ukabila, udini halafu mkajiona mupo kwenye maendeleo ya kijamii, Poleni sana.
Amani ipi unayoizungumza nchi imejaa wizi na vibaka hiyo ndio amani?
Nimekuacha na ujinga wako. Kama hujui kutofautisha kati ya uwizi na vita wewe ni level nyingine ya ujinga.
I rest my case.
Mjinga ni wewe ulielewa na Propaganda za CCM
Tanzania hakuna vita kwa sababu wananchi wake ni wajinga na woga. Lakini hizo sababu unazoziona zimeanzisha vita nchi nyengine na hapa kwetu zipo kikamilifu
sababu gani
Uonevu kwa raia
Umaskini
Wizi wa kura
Kunga'ngaia madaraka hali yakua wananchi hawataki.
Kwenye uonevu wa raia alimuonea nani? taja watatu tu
Kwenye umaskini fika pale butiama kwake ndo utaona uzalendo wake, na pia ukumbuke uhuru tuliwahi kuupata wakati nchi zingine zimepata uhuru huku mkoloni ameshafanya mambo mengi
Wizi wa kura mwalimu aliiba kura gani wakati ilikuwa ni ndio na hapana na kulikuwa hakuna vyama vingi
Mwalimu hakuwahi kung'ang'ania madaraka, tena anasifika kati ya watawala wa africa walioachia madaraka willingly bila shinikizo la mtu yeyote ingawa bado watu walitaka aendelee kutawala
Shida yako unachanganya madesa, unaleta siasa kwenye mambo ambayo hayana siasa, unataka kulazimisha link kati ya Mwalimu na chama tawala cha sasa huku mambo mengi yanayofanyika mwalimu aliyapiga vita sana, mfano Rushwa.
Hapa sitafuni maneno. Mwalimu alitoa mchango sana sana. Hata Madiba alipata mchango kutoka kwa Mwalimu. Kuvuma kwa Madiba ni zawadi kutoka kwa mabeberu na vibaraka wake kwa kuwa aliwasitiri wakati utawala wake. Walitegea angelipiza kisasi. Mwalimu havumi kwa sababu wavumishaji ni haohao mabeberu na kila wakati alikuwa akiwararua kwa maneno yenye kina kirefu.Jamani hiki kitu nimekuwa nikikiwaza kwa muda mrefu sana, hivi kati ya Mwalimu na Mandela nani alitoa mchango mkubwa zaidi?
Kwa fikra zangu nijuavyo mimi, Nyerere alitoa mchango mkubwa sana. Lakini sasa mbona hajulikani na havumi huko nje kama namna Madiba anavopewa sifa? Narudia tena hii ni kwa elimu ya historia niliyonayo na fikra zangu hivo sijaongelea mawazo ya mtu.
Naombeni tueleweshane, ni nani alitoa mchango mkubwa Africa?
Nawasilisha.
Black.
Kifo na usingiziAu kati ya Mwalimu na JPM nan zaid? [emoji23]