Sasa wewe Afrika upewe msaada sawa na Marekani kama anavyopewa Israel, unawapa nini Wamarekani?
Wayahudi waliopo USA ni 7.4m, wakati population ya pale Israel ni 9.4m, na hao 9.4m wapo pia waarabu na makabila mengine madogo madogo. Lakini wayahudi hapo Israel ni 7.2m. Kwa hiyo kuna wayahudi wengi Marekani kuliko waliopo Israel.
Na ufahamu kuwa hao 7.4m jews huko USA siyo hohe hahe, wapo wawekezaji wakubwa, wapo wataalam wa viwango vya juu kwenye tekinolojia mbalimbali, wapo wanasayansi na wagunduzi.
Leo hii wayahudi waliopo USA wakiamua kuhamishia utajiri wao wote Taifa jingine, pengo la uchumi Marekani litaonekana, na huko watakakohamishia, nchi kama ilikuwa maskini itahama na kuwa miongoni mwa nchi tajiri.
Utajiri wa mabilionea 267 wayahudi unafikia kiasi cha dollar 1.7 trillion, yaani zaidi ya mara 4 ya GDP ya Iran, zaidi ya mara 4 ya GDP ya Israel, zaidi ya mara 4 ya GDP ya South Africa, zaidi ya mara 3 ya GDP ya UAE.
Kwa hiyo, msaada wa Marekani kwa Israel, kiuhalisia siyo msaada, bali Marekani huwa inalipa fadhila ya Wayahudi waliopo USA wanaotoa mchango muhimu kwa maendeleo ya Marekani na Dunia.