Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kwenye mambo ya kihalifu nchi nyingi zimelipa Jeshi la polisi wajibu wa kushughulika na uchunguzi pale uhalifu unapotokea. Kwa Tanzania Polisi kupitia kwa DCI ndiyo wamepewa kazi ya kupeleleza uhalifu unapotokea kupitia kitengo cha CID.
Kwenye Jambo la Lissu ama kwa uzembe ama kwa kukusudia au kwa kuamriwa, Jeshi la Polisi kupitia kwa DCI kwa namna yoyote ile halijaonesha kama lina nia ya kupeleleza nani hasa waliotaka kumuua Lissu. Tangu Lissu ashambuliwe mwaka 2017 leo miaka Sita baadae uwezekano wa kupata ushahidi wa moja kwa moja unakuwa mgumu.
Lakini siku ya tukio kulikuwa kuna kila uwezekano wa kupata ushahidi unaotakiwa kuwatia mbaroni wote waliohusika. Kwanza wale watu walitumia usafiri wa Magari hivyo haikuwa ngumu kupata taarifa zao. Kwa mfano aina ya gari zilizotumika ni lazima tu zilijulikana na kuonekana.
Kwa sababu risasi zilipigwa mchana, ni lazima sauti zilikuwa kubwa hivyo bila ya shaka majirani walitoka kuangalia kuna nini. Hao majirani lazima waliziona gari zilizohusika na aina yake. Majirani hao pia waliona baaada ya tukio gari hizo zilielekea wapi.
Tuliambiwa kwamba Medard Kalemani alikuwa anakaa jengo moja na Lissu. Jee kwa Kalemani kulikuwa hakuna mtu, jee ni kweli kwamba kulikuwa na CCTV na ikaodolewa baada ya tukio. Jee Polisi walipofika kwa Kalemani hakuna waliyemhoji?
Bila ya shaka hao waliotaka kumuua Lissu pia walitumia simu za mkononi, Jee Polisi waliangalia simu zilizopigwa toka kwenye minara ya simu iliyo karibu na tukio lilipotokea, walifanya uchambuzi wa mawasiliano yaliyofanyika toka eneo la tukio masaa miwili kabla ya tukio na dakika chache baada ya tukio?
Baada ya uchambuzi wa mawasiliano hayo walilinganisha namba hizo za simu kabla ya kutumika eneo la tukio zilitumika wapi kabla. Jee hizo namba ziliwasiliana na namba gani nyingine, na hizo namba zinamilikiwa na nani? Lissu ni mwanasiasa, jee Polisi waliangalia mawasiliano ya wanasiasa wa CHADEMA na CCM kabla ya tukio na baada ya tukio walikuwa wamewasiliana na nani na waliwasiliana mara ngapi na kuhusu nini?
Polisi waliwahoji majirani wa Lissu kwa umbali gani na kwa muelekeo upi? Mpaka sasa polisi wanayo maelezo ya watu wangapi waliowahoji toka tukio lilipotokea mpaka sasa. Jee Kuna majirani au marafiki wa Lissu ambaye anatiliwa shaka kutokana na mwenendo wake dhidi ya Lissu?
Polisi mpaka sasa wanao washukiwa wangapi au watu wanaowatilia shaka kuhusika na tukio lile? Hadi hapa ni nani wa kulaumiwa kati ya Polisi na Lissu??