Kati ya Polisi na Lissu ni nani wa kuwasaka waliotaka kumuua Lissu??

Kati ya Polisi na Lissu ni nani wa kuwasaka waliotaka kumuua Lissu??

Pole ndugu...Kwa kauli hii Utakua unamapepo mazito... tafuta kanisa karibu ukatolewe ni hatari kukaa namapepo mengi hivyo.
Sawa ntaombea ila nimeomba picha nyingine kama hipo,kila siku mapaja mapaja dah!.
 
Wewe si Polisi haya mambo huyajui bora ungekaa kimya. Kwa miiko ya Kipolisi, na ndiyo ukweli, shahidi mzuri ni yule aliyewaona kwa macho wao huita eyewitness. Kuna mtu mmoja aliwaona mchana kweupe kama ulivyosema, mtu huyo anaitwa tundulissu. Kwa nini hajaenda Polisi, badala ya kuwatukana? Kulikuwa na shahidi mwingine, eyewitness, dereva wake tundulissu naye kawaona kwa macho yake, na ni askari. Kafichwa na CHADEMA (nasikia yuko kafungiwa chumbani pale Ufipa). Finally, hakuna hadi leo aliyelalamika, kwani tundulissu hana ndugu? Hana mke? Umetaja CCTV, nani alizing'oa? Saa ngapi? Kumbuka hakuna aliyejua kuwa tundulissu ataenda lunch siku hiyo, aliyezing'oa kwani alijuaje?

Umetaja majirani, sawa kabisa: Watanzania tunashiriki harusi, iddi, kipaimara, Christmas, mazishi, nk. Mbona hawakujitokeza hata mmoja? Jiulize, au labda tundulissu hana ushirikiano? Si unajua alivyo mshari na matusi, labda wamemtenga? Pia unajua alivyo majivuno, labda majirani kawachosha? Au labda yeye huwaga haendagi kwenye misiba ya jirani?

Kwa basic mathematics, 2+2=4. Ni wazi kuwa tundulissu na CHADEMA walijua kila kitu kilichotokea, haja yao ilikuwa kuitia aibu serkali na kuifitinisha na raia. Wewe uliona wapi risasi za SMG ziingie moyoni au tumboni halafu mtu asife? Hii ilipangwa ila hawakutegemea ataumia kiasi hicho, lakini wanaogopa kusema. Ila tukumbuke Dr Mollel aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA jimbo la Sanya Juu, afisa wao mwandamizi, aliyoboa kuwa alishambuliwa na CHADEMA. Hata Dr Slaa unakumbuka alikataa kwenda kumslamu au kumpa pole kwa sababu ana dukuduku lake. Let CHADEMA come clean on this, our Police are very busy please.
Kwa hiyo hao Cdm ndio waliowaondoa walinzi hilo eneo linalolindwa 24 hrs ili hao wahalifu watekeleze ushetani wao bila interfearance?Nyie watu mtaanza lini kumuogopa Mungu?

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Polisi watanzania wapumbavu ndio maana watu wanaosema magufuli alihusika wanaeleweka zaidi kwasababu polisi wangekuwa Wana nia wangeanza na nani alipangua zamu za walinzi? Nani aliiondoa CCTV camera na kwanini? Mchezo ungeishia hapo! Kwasasa mama anachofanya ni kumlindia marehemu heshima na kumfichia aibu ila Kwa 99% magufuli alihusika na alivyomjinga alitoa clue ya mission kwenye kile kikao Cha makinikia!
 
Kwenye mambo ya kihalifu nchi nyingi zimelipa Jeshi la polisi wajibu wa kushughulika na uchunguzi pale uhalifu unapotokea. Kwa Tanzania Polisi kupitia kwa DCI ndiyo wamepewa kazi ya kupeleleza uhalifu unapotokea kupitia kitengo cha CID.

Kwenye Jambo la Lissu ama kwa uzembe ama kwa kukusudia au kwa kuamriwa, Jeshi la Polisi kupitia kwa DCI kwa namna yoyote ile halijaonesha kama lina nia ya kupeleleza nani hasa waliotaka kumuua Lissu. Tangu Lissu ashambuliwe mwaka 2017 leo miaka Sita baadae uwezekano wa kupata ushahidi wa moja kwa moja unakuwa mgumu.

Lakini siku ya tukio kulikuwa kuna kila uwezekano wa kupata ushahidi unaotakiwa kuwatia mbaroni wote waliohusika. Kwanza wale watu walitumia usafiri wa Magari hivyo haikuwa ngumu kupata taarifa zao. Kwa mfano aina ya gari zilizotumika ni lazima tu zilijulikana na kuonekana.

Kwa sababu risasi zilipigwa mchana, ni lazima sauti zilikuwa kubwa hivyo bila ya shaka majirani walitoka kuangalia kuna nini. Hao majirani lazima waliziona gari zilizohusika na aina yake. Majirani hao pia waliona baaada ya tukio gari hizo zilielekea wapi.

Tuliambiwa kwamba Medard Kalemani alikuwa anakaa jengo moja na Lissu. Jee kwa Kalemani kulikuwa hakuna mtu, jee ni kweli kwamba kulikuwa na CCTV na ikaodolewa baada ya tukio. Jee Polisi walipofika kwa Kalemani hakuna waliyemhoji?

Bila ya shaka hao waliotaka kumuua Lissu pia walitumia simu za mkononi, Jee Polisi waliangalia simu zilizopigwa toka kwenye minara ya simu iliyo karibu na tukio lilipotokea, walifanya uchambuzi wa mawasiliano yaliyofanyika toka eneo la tukio masaa miwili kabla ya tukio na dakika chache baada ya tukio?

Baada ya uchambuzi wa mawasiliano hayo walilinganisha namba hizo za simu kabla ya kutumika eneo la tukio zilitumika wapi kabla. Jee hizo namba ziliwasiliana na namba gani nyingine, na hizo namba zinamilikiwa na nani? Lissu ni mwanasiasa, jee Polisi waliangalia mawasiliano ya wanasiasa wa CHADEMA na CCM kabla ya tukio na baada ya tukio walikuwa wamewasiliana na nani na waliwasiliana mara ngapi na kuhusu nini?

Polisi waliwahoji majirani wa Lissu kwa umbali gani na kwa muelekeo upi? Mpaka sasa polisi wanayo maelezo ya watu wangapi waliowahoji toka tukio lilipotokea mpaka sasa. Jee Kuna majirani au marafiki wa Lissu ambaye anatiliwa shaka kutokana na mwenendo wake dhidi ya Lissu?

Polisi mpaka sasa wanao washukiwa wangapi au watu wanaowatilia shaka kuhusika na tukio lile? Hadi hapa ni nani wa kulaumiwa kati ya Polisi na Lissu??
Aliyetoa Maagizo Lissu auawe anajulikana , Kwanza yeye Kishakufa, waliompiga Risasi / Waliotekeleza Amri wanajulikana, Wala hakuna Sababu ya Upelelezi, sema tu hawawezi kuwakamata Kwa Sababu hawataki
 
Mjinga tu kwa sababu kama mtaji wakisiasa anavyofikiri yeye wala haijawa mali. Siku za za mwanzo baada ya kupata fahamu kutoka kupigwa risasi alionekana kama kufurahia na akasema itamuingiza ikulu. ila hadi leo kaishia ukimbizi wa kujitakia huku akiwa kiitikadi ni kibaraka wa magharibi hadi kuunga mkono ushoga
 
Labda kuna siku mmojawapo walihousika atajitokeza kutubu.
 
Hoja zinautata wanasema kesi ya jinai ni lazima victim afike kuanzisha kesi lakini upande wa pili unahoji je,angefariki ingekuwaje? Mimi najiuliza ingekuwa kosa ni kubakwa na aliyebakwa hataki kutoa ushirikiano je,hiyo kesi inaweza Kuwa na mafanikio?
Hata ningekuwa Mimi ndiyo Polisi ningeacha maana victim ni mtata mno.
 
Miaka 6 toka ashambuliwe ni muda mrefu sana Nina shaka hata wahusika tukio hili siyo wengine wamekufa na wengine wamefukuzwa kazi, usihofu iko siku tena nihivi karibuni tamati ipo.
 
Back
Top Bottom