Kati ya Polisi na Lissu ni nani wa kuwasaka waliotaka kumuua Lissu??

Hakuondoshwa aliondoka. Hivi Dereva umuhimu wake kwenye hili jambo uko kwenye nini ama unazuia nini Polisi kufanya uchunguzi wao? Hivi kati ya Dereva na CCTV iliyong'olewa kwa Kalemani kipi cha muhimu??
Yeye ndio ana taarifa muhimu kwa sababu alijua kuwa kuna gari inawafuatilia
 
Hata ukiibiwa fedha chumbani kwako polisi wanaanza kumuhoji mkeo ndio wanaendelea na wengine!

Very simple
Polisi kuanza kuhoji mkeo na kufanya utafiti wa kuwahoji majirani lilipotokea tukio la kutaka kuua havihusiani. Wao mpaka sasa wameshafanya nini iwe imebakia tu kumhoji Dereva wa Lissu??
 
Polisi kuanza kuhoji mkeo na kufanya utafiti wa kuwahoji majirani lilipotokea tukio la kutaka kuua havihusiani. Wao mpaka sasa wameshafanya nini iwe imebakia tu kumhoji Dereva wa Lissu??
Wewe hujiulizi Kwanini Wote wamerudi isipokuwa dereva wa Lisu tu?
 
Beki 3 wa Lisu na yule wa Tulia ambao kimsingi ndio waliokoa Maisha ya Tundu Lisu wameshatoa Maelezo yao!

Au unataka majirani gani?
Usiwadhalilishe Polisi wetu. Kutokuwepo kwa Dereva wa Lissu hakuwezi kuzuia Polisi werevu kufanya uchunguzi wao. Labda utuambie kuwa Polisi wetu viwango vyao vya kufanya uchunguzi ni vya chini sana.
 
Polisi hawajawahi kujiangaisha na inshu ya Lissu kupigwa risasi, ndo maana chadema ilipoomba wachunguzi kutoka nje ya nchi waje wafanye uchunguzi serikali ilikataa kbs, ilikataa kwa sababu ilihusika kwa 100% ... Order ilitoka kwa raia namba moja,ikatekelezwa na mwanaye mpendwa lkn mwenyezi mungu akasema hafi mtu hapa .. kwahiyo hata hao pimbi wanaomtaka dreva wa Lissu aje kutoa maelezo ni makanjanja tu, walitaka dreva wa Lissu aje ili wamhonge aseme ni chadema ndo walihusika na lile tukio...uzuri kila kilichokuwa kinapangwa na yule raia namba moja wa kipindi kile kulikuwa kinavuja moja kwa moja... hvyo ni tukio la hovyo kuwahi kutokea ambalo kila mwenye akili timamu anajua kbs serikali ilihusika na lile jaribio

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Very simple!
Wakati mwingine najiuliza ni kwa nini kwenye chama chenu mmejaza "Manipulators" na "Spinning Doctors", Yaani mnataka kila Mtanzania awe "Zombie" kwa faida zenu za kisiasa.

Hivi hao polisi wanaongojea Dereva wa Lissu arudi wangepewa kazi ya kupeleleza lile tukio la Bomu la Oklahoma wangefanyaje? Zama hizi za teknolojia bado kuna mtu mwenye akili timamu anakaa na kuwaambia watu kwamba ameshindwa kupeleleza tukio la Lissu kupigwa Risasi eti kwa kuwa Dereva wa Lissu hayupo!!

Ujinga kabisa huu!!
 

Zama hizo palikuwa na genge la wasiojulikana. Majina haya yalikuja kutajwa kuwa kwenye genge hilo:

Goodluck, Mahita, Jumanne, na yule Mwingine akiwamo.

Sasa kama hiyo ofisi kubwa ndiyo yenye kulisaka kundi hili hili mbona hapo mtihani mkuu?

Kwamba wanajitafutaje wenyewe sasa?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…