Kati ya Polisi na Lissu ni nani wa kuwasaka waliotaka kumuua Lissu??

Wewe si Polisi haya mambo huyajui bora ungekaa kimya. Kwa miiko ya Kipolisi, na ndiyo ukweli, shahidi mzuri ni yule aliyewaona kwa macho wao huita eyewitness. Kuna mtu mmoja aliwaona mchana kweupe kama ulivyosema, mtu huyo anaitwa tundulissu. Kwa nini hajaenda Polisi, badala ya kuwatukana? Kulikuwa na shahidi mwingine, eyewitness, dereva wake tundulissu naye kawaona kwa macho yake, na ni askari. Kafichwa na CHADEMA (nasikia yuko kafungiwa chumbani pale Ufipa). Finally, hakuna hadi leo aliyelalamika, kwani tundulissu hana ndugu? Hana mke? Umetaja CCTV, nani alizing'oa? Saa ngapi? Kumbuka hakuna aliyejua kuwa tundulissu ataenda lunch siku hiyo, aliyezing'oa kwani alijuaje?

Umetaja majirani, sawa kabisa: Watanzania tunashiriki harusi, iddi, kipaimara, Christmas, mazishi, nk. Mbona hawakujitokeza hata mmoja? Jiulize, au labda tundulissu hana ushirikiano? Si unajua alivyo mshari na matusi, labda wamemtenga? Pia unajua alivyo majivuno, labda majirani kawachosha? Au labda yeye huwaga haendagi kwenye misiba ya jirani?

Kwa basic mathematics, 2+2=4. Ni wazi kuwa tundulissu na CHADEMA walijua kila kitu kilichotokea, haja yao ilikuwa kuitia aibu serkali na kuifitinisha na raia. Wewe uliona wapi risasi za SMG ziingie moyoni au tumboni halafu mtu asife? Hii ilipangwa ila hawakutegemea ataumia kiasi hicho, lakini wanaogopa kusema. Ila tukumbuke Dr Mollel aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA jimbo la Sanya Juu, afisa wao mwandamizi, aliyoboa kuwa alishambuliwa na CHADEMA. Hata Dr Slaa unakumbuka alikataa kwenda kumslamu au kumpa pole kwa sababu ana dukuduku lake. Let CHADEMA come clean on this, our Police are very busy please.
 
Wewe si Polisi haya mambo huyajui bora ungekaa kimya. Kwa miiko ya Kipolisi, na ndiyo ukweli, shahidi mzuri ni yule aliyewaona kwa macho wao huita eyewitness.
Kwanza umeandika mambo meengi yasiyohusiana na hii mada kasoro hili moja. Kuwa eneo la tukio siyo sifa ya kuwa "Eyewiteness" kwa kuwa ili uweze kuona ni lazima ubongo wako utoke kwenye kuangalia kwenda kwenye kuona. Ndiyo maana unaweza kumuangalia mtu lakini usimuone.

Yaani kwenye Mazingira yale ulitaka Dereva wa Lissu awe na uwezo wa kuona waliomshambulia Lissu kuliko CCTV? Yaani CHADEMA wasio chombo cha kufanya upelelezi unataka kuwatwisha jambo lisilowahusu? Hivi kama Lissu alikuwa hana mahusiano na majirani zake inazuia vipi polisi kuwahoji hao majirani?


Unamuona huyu dada, anaitwa Gabby Gilford, alikuwa ni Mbunge kwenye Bunge la Marekani na alipigwa Risasi iliyopenya toka upande mmoja wa sikio kwenda sikio jingine. Leo Gabby yupo hai akiwa na akili timamu.

Unashangaa vipi Lissu kuwa hai!!??
 
Utopolo mtupu, yaani inaonekana ww ni mmoja wa wale waliomshambulia mhe Lissu

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 

Ndugu policeman:

1. Hukuwaongelea polisi waliopaswa kuwa getini kuwakagua wote wenye kuingia kwenye Ile compound ya viongozi area D.

2. Hukuwaongelea polisi Dodoma, ambao taarifa yao ya awali ilisema walizipata CCTV recordings husika za tukio.

3. Umejisahaulisha kuwa CCTV ziling'olewa baada ya tukio.

4. Umejisahaulisha pia kuwa upelelezi ulipaswa kufanyika na kuwapata wahalifu hata kama Lissu na Dereva wote wangalikuwa marehemu.

5. Umejisahaulisha pia kuwa hata kama Chadema, Lissu au driver walihusika upelelezi ulipaswa kuonyesha hayo na kuwakamata wahusika wote.

Kwani mna kipi cha kuficha kwenye hili sekeseke ndugu?

Au ni Ile habari kubwa kuwa mwenye lake jambo alikuwa ni yule mwenye ule mhimili uliokuwa umejichimbia zaidi?
 
Lisu anaogopa nini kumleta dereva wake?
Nini dereva, kwa nini yeye mwenyewe Lissu hawamuhoji? Ushahidi wa dereva na ushahidi wa CCTV cameras footages upi ni wa uhakika zaidi? Polisi waliopaswa kuwa zamu na mabosi wao wanaopanga zamu za lindo kwa nini hawakuhojiwa? Kwa nini hata Jiwe mpenda sifa hakuwahi hata 'kuwapiga' chini mabosi wa polisi Dodoma au hata IGP manake alikuwa maridadi kwa misifa.
Vipi wazo la Mbowe la kushirikisha FBI au MI6 ya Scotland Yard mbona polisi walilikataa wakidai kila kitu kipo ndani ya uwezo wao, kumbe ilikuwa ni danganya toto hawakuwa wakitaka upelelezi ufanyike.
Mambo ya ajabu baada ya shambulio:
-Kuzuia watu wasimuombee Lissu.
-Kuzuia T-shirts zenye maandishi ya 'Get well soon Lissu'
-Kufura kwa subwoofer Ndugai kwamba imekuwa Lissu kapelekwa kutiwa Nairobi(obviously angebaki wangemmalizia hospitali) na wakadai ni mtoro asilipwe chochote wala asigharamiwe matibabu.

La muhimu kuliko yote - Footages za CCTV cameras ziibuliwe kokote zilikofichwa tujionee shambulio lilivyofanyika na si kupewa story za watu za kuungaunga au kuwatia watu kwenye pressure(brutal interrogations) mpaka wakiri hata mambo ya uongo, a picture speaks thousand words.
 
We jamaa mbona una maswali magumu kiasi hicho?
 
Hitller hakuna nayejua kwamba aliuwawa au alijiua mwenyewe kwenye Tindikali.....mfano wa hovyoo huu.Lissu dereva wake yupo na yeye yupo watajwe tu.
Yule Muhutu mwenzako Jiwe ndiye alikuwa muhusika namba moja(hii ni kwa mujibu wa Lissu mwenyewe na ameongea live kwenye vyombo vya habari) na mpaka leo si polisi wala uongozi wa serikali waliokanusha, wanatamani lile tukio lisahaulike lakini halitosahaulika na litakuwa likiibuliwa mara kwa mara mpaka majibu yapatikane.
 
Lissu angekufa kwenye lile shambulio moja kwa moja kesi angepachikwa Mbowe, sasa ilikuja kuwawia vigumu kufanya hivyo kwa kuwa Lissu yuko hai na ujinga huo angeupigia kelele sana hasa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa.
 
Achana nae huyu ni mmoja wa wahusika!!
 
Wewe utakuwa unakipele kinakuwasha huko matakoni,unawezaje kunishadadia hivyo kama nilishakununua wala sikukulipa?,husiniharibie mfungo plz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…