Kati ya Subaru Forester and Toyota GX100 ipi ni mnyama barabarani?

Nakusoma kaka mkubwa ila tusonge nao mdomdo si unajua hata mbuyu ulianza kama mchicha. Kama ombi la kuanzishiwa jukwaa maalim litapitishwa the kila mmoja wetu atachangia kidogo mwisho wa siku tutakuwa happy and knowledgeble on roads
 

Ha ha haaaaaaaaa on same page babu Wazungu hao ni habari nyingine ndo maana wala sijawagusa kabisa katika hii mada as wao wanafanya kujiridhisha (quality) while wengine wanafanya kwa kujaza soko (quantity)

No wonder Rover wanashinda tu mashindano ya off-road...hii tells a lot on technology. Racing imetawaliwa na magari yao pia harnesses on the same
 
Inategemea ni ya mwaka gani, lakin around 23.5M unaiendesha barabarani!

23.5M = Altezza mbili na chenji
Du! Hapa umenivunja moyo kabisa, nimegundua kwa nn magar ya japan yamejazana hapa bongo...BEI ndo tatizo kumbe?

Kwa kuwa nina nia nitazichanga tu niipate iyo Subaru.

Hivi hapa bongo kuna mafunzo ya mashindano ya magari? Nafikiri ningezaliwa ughaibuni ningetimiza ndoto yangu kuliko kuwapigia kelele watu mtaani na mikokoten yetu.
 

Hhahaa, nunua ya nyuma kidogo, around 15, mambo mengine utaupgrade mwenyewe taratibu kadri unavyopata pesa, au chukua kutoka japani hata auto ya kuuzia sura mkuu! Shule kubwa ya mambo haya ni kuwa karibu na wakongwe, Jiune na Subaru Fans of Tanzania kule FB utajifunza mengi tu!
 

kitu tunachomiss hapa bongo ni RACE TRACKS,ndio maana vijana wa kihindi na waarabu usiku wanageuza barabara zetu race tracks,subaru hizo zinawachinja kinoma.....kwenye race tracks unakuja na mashine yako unalipia then u just burn rubber.....au ukiona vipi unalipia zaidi unapata ferrari/lambo/porsche unakula ride.....
 

Haina noma mkuu, ile pg ya fb nimeipitia ni nzur.

Kuna muvi moja ya wa_Hong Kong inaitwa MOTORWAY ni hatari sana kuna huyo Dereva machachari anaendesha gari utadhani alizaliwa nayo, ananikosha sana we itafute uichek...
 

Dah! Hii kitu nitaifanya nikirudi kijijin kwe2 kwenye barabara za ng'ombe
 

Mfano mdogo tuu kulingana na maelezo yako

Subaru impreza sports wagon 1490 cc and Carina TI, PREMIOS, GX ENGINE TOYOTA SERIES.based 1500 CC to 3400CC, Impreza inabeat all of those. ebu nambie kwann?
 
Mfano mdogo tuu kulingana na maelezo yako

Subaru impreza sports wagon 1490 cc and Carina TI, PREMIOS, GX ENGINE TOYOTA SERIES.based 1500 CC to 3400CC, Impreza inabeat all of those. ebu nambie kwann?

rudi juu kasome maelezo yangu....narudia tena.....nilisema kuna gari zina engine ndogo[mfano subaru impreza cc2000] zinakimbia kuliko gari zenye engine kubwa......nilisema tena subaru forester yenye TURBO[hii ndio inacompansate udogo wa engine yake] inakimbia kuliko gx100 lakini ISIYO NA TURBO[FORESTER] iko sawa na gx100.....kuna njia nyingi za kupata powerful engine.....moja ni kuweka cc kubwa mfano bmw m3 ina cc karibu 3000 kuliko bmw 3 series ya kawaida i.e 316i,318i,320i etc.....njia ya pili ni kuwa na same small engine size lakini una weka TURBO CHARGER AU SUPERCHARGER[ukitaka somo la turbo na supercharger nitakupa]
sasa basi SUBARU badala ya kuweka big engine kama bmw na most european models,wao wameamua kuweka TURBO CHARGER hence small engine more power more speed.......lakini uchukue subaru ya cc1400[sijui ya mwaka gani hii] ISIYO NA TURBO haiwezi kusumbua gx100.......naomba usome kwa makini.
 

Hukunielewa!!!!!! anyway let me do my home work as you advised.
 

Somo tam sana hili mkuu shusha madesa ya TURBO CHARGER AU SUPERCHARGER
 
Hata kama Subaru haina turbo haiwezi kwenda sawa na GX 100 ndugu yangu. Hiyo ni H engine na si inline engine. Hakuna usawa hapo hata kidogo.Jamaa hakutaka ligi au ni mwoga. Katika gari zote zenye engine yenye ukubwa sawa na yenyewe si rahisi kukaa nayo pamoja barabarani. Ogopa H engine kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…