Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Kati ya uMagufuli na Samia ni upi umejaa wahuni zaidi? Tuorodheshe matukio ya kihuni

Kwamba hajasema wajipimie? Kipi ambacho nimeandika sicho alichosema?
Samia alikuwa akiwaambia Mawaziri waache rushwa na ndio maana ya kula kwa urefu wa kamba, hiyo tafsiri nyingine za kulazimisha ni kutafuta agenda tu
 
Samia alikuwa akiwaambia
Mawaziri waache rushwa na ndio maana ya kula kwa urefu
wa kamba, hiyo tafsiri nyingine
za kulazimisha ni kutafuta
agenda tu
Kujipimia ndio kuacha rushwa? Au hajasema wajipimie?

Hebu kamsikilize tena vizuri.
 
Mkuu ulikuwa ukifuatilia ile kesi? Kama hukuwa unafuatilia ni kuwa watuhumiwa wote na mashahidi wote walikuwa wameshaandaliwa mwaka 2020 na ushahidi wao ukimu implicate Mbowe kama mtuhumiwa mkuu

Samia ana Makosa ila Magufuli anayo pia
Mnadanganywa sana nyie watu. Mnatumia nguvu kubwa kumchafua jpm. Tuseme ushahidi ulishaandaliwa kumshitaki Mbowe, tena mbona awamu hii ikaamua kuendelea nayo hiyo kesi? Si wangeacha tu. Hampendi sana kuambiwa kwamba Mbowe alishitakiwa na Serikali hii iliyopo. Mnaona kama ni doa siyo?

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
Ila ile awamu ya 5, awamu ya Jiwe, ilikuwa awamu ya uongozi wa kibaradhuli.

Uongozi unaoua wanaokosoa, ni uongozi wa kishetani, ambao hauwezi kupata nafasi ya kuoshwa kwa namna yoyote ile.

Marehemu Magufuli ataendelea kukumbukwa kwa vizazi vingi kama mtawala baradhuli, muuaji, mtesaji na ambaye hakukubali kukosolewa kutokana na uuaji, utekaji na utesaji watu. Makosa mengine yote, kama uwongo na kuharibu uchumi, kuvunja haki za uhuru wa watu, udikteta, kutapanya pesa ya umma, uporaji wa pesa za watu na kuwabambikia watu kesi, ataweza kusamehewa lakini ushetani ule wa kuua na kuteka watu, kamwe hautasahaulika. Alijipa mamlaka ya kuondoa uhai wa watu, kama vile yeye ndiye anayeugawa, hakujua kabisa, shetani alimpumbaza, hata asijue kuwa hata yeye hawezi kukikwepa kifo.

Watawala na sisi sote tulio hai leo, tuogope kutenda maovu, tuogope na tusisogelee wala kuwaza kuwaua wanadamu wenzetu. Uhai wa mtu ni mali ya Mungu, ndiye aliyetupatia, na ndiye mwenye uwezo wa kuundoa.
Mkuu umeandika vizuri ,binafsi sijawai kumtukuza mwenda zake hata siku MOJA na ukipitia maandiko yangu nilionya Sana, ila Sasa hata aliemshikia haendi sawa hata kidogo ,viatu vimekua vikubwa mno KWa taifa thanks
 
Wote ni wahuni kwani Samia alikuwa makamu wa rais, baada ya kushika madaraka kawarudisha mafisadi wote na sasa wanaitafuna nchi kwa raha zao huku wananchi tukipandishiwa bei ya kila kitu. CCM wote majizi
Fisadi gani karudishwa?
 
Ubaya ni ubaya tu, na wote hautakiwi kufanyiwa mwanadamu, haijalishi uwe wa large scale au small scale.

Hii tabia yenu ya kuendelea kulinganisha ubaya wa serikali iliyopita na hii ya sasa unawadumaza wengi kiakili, hamuoni ubaya wa serikali iliyopo madarakani, na ndio maana mnajikuta mnageuka kuwa chawa bila kujitambua.

Lakini pia mnaidumaza serikali iliyopo madarakani, iendelee kujiona ni ya malaika wakati nayo imejaa mabaya yake, uvunjifu wa sheria wa wazi inayoukumbatia kwenu mnaona ni jambo la kawaida, na kwa ujinga wenu mnachangia kuiendeleza tabia hiyo.
Mleta mada katoa facts na wewe toa za serikali ya ssh acha blaa blaa
 
Mnadhani 'kufa' ni adhabu wakati hata nyie mtakipata kwa wakati wenu.
Hata wewe utakufa usitishie watu, swali ni hili: kwa nini mkiambiwa huyo bwana yenu alishakufa mnang'aka? Au hamkushuhudia mazishi baada ya maonyesho ya mzoga wiki nzima
 
Hii tabia ya kuendelea kulinganisha mabaya wa serikali iliyopita unawadumaza wengi akili zenu na inapelekea hamuwezi kuona ubaya wa serikali iliyopo sasa, ndio maana mnajikuta mnageuka kunguni bila kujitambua.
Hata nyie mlikua kunguni wa hayati na mlikua hamuambiliki, zamu yenu imepita acha machawa nao watambe mjini si ndio zenu huko chama twawala
 
Samia kumuweka ndani mwanasiasa mkubwa wa upinzani kwa tuhuma za ugaidi.
Samia alirithi ile kesi kama ulikua unaifatilia kesi ilifunguliwa mwezi wa 8 2020 ndipo ikaanza kutafutiwa watuhumiwa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Samia alirithi ile kesi kama
ulikua unaifatilia kesi ilifunguliwa mwezi wa 8 2020
ndipo ikaanza kutafutiwa
watuhumiwa[emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwahiyo kama karithi kesi ndio unataka kusema nini? Mbowe kakamatwa na kuwekwa ndani katika utawala wa Samia na yeye mwenyewe Samia alipoulizwa kuhusu hiyo kesi hakusema kwamba ameikuta tu bali alionesha kuwa Mbowe ana kesi ya kujibu.
 
Historia ya nchi haiwezi kuachwa ikawa bygones, sio mambo ya kifamilia haya
Umeandika facts..ukweli ni kwamba hawawezi kukujibu zaidi ya kutukana tu.
Mambo mabaya yaliyofanywa na magufuli nchi hii itachukua miaka 10 kuyarekebisha ni mambo ya hovyo kwelikweli
 
Juzi kuna mzee aliniambia nioe, niache uhuni.
 
Hivi unaifahamu maana ya "collective responsibility" hasa pale ilipotumika ili kulinda maslahi ya CCM?
Wewe ni mpumbavu usiyejielewa, sikuisifia CCM wala Samia hapa
Ninachokisema ni wanaodai utawala huu una wahuni kuliko wa Magufuli waweke fact mezani

Kama wewe unaona zote ni za wahuni basi sawa mada haikuhusu
 
Kipindi cha Magufuli ndio mtu kama Sabaya alitamba sana, na kuna matukio kibao kama ya ubakaji, uporaji, kubambikizia kesi n.k
umemsahau na yule mwana habari huru na kile kipeperushi chake kwamba " Shoga awagombanisha viongozi waandamizi.
 
Back
Top Bottom