Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Absolutely! Sikuelewa toka mwanzo kwanini waliamini kuwa Rais ambaye hakuwa na ajenda ya Katiba Mpya muda wote wa kampeni (na miaka ishirini kabla yake) hatimaye ameona mwanga na sasa angeweza kuwa msimamizi mzuri wa mchakato wa kuelekea Katiba mpya.

Chadema pekee ndio wanaweza kuwa wasimamizi wazuri wa machakato wa katiba mpya???

Aisee mna akili sana??? hivi chadema ndio another super party in making
 

Naweka kifungu kizima cha 86 cha Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la 2007



Pasco anaamini kuwa kwa kutumia kifungu cha 86:3b kwamba Lissu alitakiwa kutoa hoja kwa kutumia kanuni hiyo na mara moja mjadala ungesitishwa. Tatizo ni kuwa kifungu cha 4 cha ibara hiyo kinaweka mtego kuwa hata hoja ya kukataliwa kwa mjadala haisababishi kusitishwa kwa jumla kujadili mswada. Kinachotokea ni kuwa mtoa hoja atapewa nafasi ya kuelezea kwanini mswada usitishwe.

Sasa fikiria kuwa Lissu ametumia ibara hiyo na kupewa nafasi ya kuelezea kwanini mkataba ukataliwe na akaeleza kwa kirefu hoja zake zote. Mwisho akimaliza ibara ya 86:4 inatumika: Yaani,

4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii, Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.

Kumbe, Lissu akimaliza kutoa hoja zote za kuzuia Spika ataliuliza Bunge lifanye uamuzi wa kukataa au kukubali mswada ukataliwe au la. Nani anafikiria kuwa CCM wangeweza kushawishika kukubali hoja ya Zitto kukataa mswada? Maana hoja alizozitoa kwenye hotuba zingekuwa ni karibu zile zile (kama siyo zile zile) ambazo angezitoa kutaka mswada ukataliwe.

Kwa maneno mengine Ibara ya 86 isingeweza kufanya hoja ya CDM ifanikiwe kuzuia mjadala wa mswada kuendelea. Ingeweza tu kumpa Lissu nafasi ya kuelezea kwanini mswada ukataliwe lakini ultimately Bunge lingeulizwa na Spika kama waukatae na sote tumeona kuwa mswada usingeweza kukataliwa na Wabunge wa CCM kwani hata bila hoja za Lissu wao CCM wangeweza kuukataa wenyewe na hawakufanya hivyo!
 

Sure, mkuu muswada uliporudi kutoka bungeni kila wakati tulikuwa tunaonyeshwa wabunge wakifanya semina na wataalamu wa sheria, akina Shivji, etc ili kupata maoni na kuboresha muswada kabla ya kwenda wakiwemo wabunge wa chadema ...

Waziri wa sheria (kivuli) ana haki sawa kuuliza mchakato wote anytime prior to bunge (aseme kama kweli alinyimwa hizo fursa??)

otherwise anatafuta media attettion hana la maana la kutuambia..
 
Chadema pekee ndio wanaweza kuwa wasimamizi wazuri wa machakato wa katiba mpya???
Aisee mna akili sana??? hivi chadema ndio another super party in making

CHADEMA hawapingi ili wao waongoze, wanachotaka ni kufuata taratibu, na taratibu zinasema muswada unaanza kwa kuchukuwa maoni ya wananchi. Shida CCM walishaamua siku nyingi kwamba wao ndio wana akili.

Binafsi ningependa kufuata utaratibu unawashirikisha wananchi ili kuhakikisha kumbe mbeleni hatutakaa tuwe na chama chochote (CCM, CHADEMA, CUF, TLP ,DOVUTWA etc etc) kinakuwa na utawala wa kifalme kama wa sasa. Ni vizuri kurudisha mamlaka kwa wananchi ili wawe na nguvu ya kuwajibisha viongozi mara moja wanapokwenda kinyume tofauti na sasa na hii itatuletea neema wote (ccm included).
 

Utaratibu uliopitishwa sasa unakunyima vipi kutokufikia hicho unachotaka?? yaani katiba nzuri uipendayo??

Usije na speculations? kwamba ccm vile na vile??
 
Aksante sana Mkuu
hivi hili National gazeete linapatikan wapi? . nadhai ni kila muswada kabla ya kuwa sheria lazima utangazwe kwenye national gazeete lakini huwa hasa sijui ni lipi hasa na linaptaikanaje kwa wananchi. hii katiba ya mkoloni naona kuna vitu tumerithi wengi hatuvielewi. Kama hii natonal gazzeti huwa nasikia sana lakini sijui sura yake. Au ndio Daily News????11111

Duh hii basi kali wanafanya Pilot testing hata kwenye katiba. Hapa sasa ndio naanza kukusoama na kuona Tatizo


Hata hivyo hatua hii ilikuwa pre-mature kwa sababu bado muswada ulikuwa kwa lugha ya kiingereza hivyo wananchi wengi wasingejua nini kimeandikwa. Wajumbe wa kamati walipoomba kwenda mikoa mingine walau 10 Spika akazuia.
hili nalo ni Tatizo lingine sababu hata bunge letu ni la vyama vya siasa. watu hawaruhusiwi kugombea bila vyama . Sina tatizo kubwa na hili lo lakini nataka kuonyesha kuwa na bunge letu lisisijahau likadhani lenyewe ndio driving seat kwenye katiba mpya. Na bunge letu linahitaji kuwa reformed wenye katiba mpya......

mkuu hapa sasa ndio nilitaka kujua right sequce ya event ilitaiwa kuwaje. Nani anataiwa kuusanya maoni. nani anataiwa kumteau nani . Yaani Nani anatakiw kuform structure na muundo na wajumbe wa katiba mpya. Wajumbe wapatikane vipi?

Yaani kuna maswali najiuliza sipati majibu sabbau kama ni bunge linangozwa CCM ukitumia demokrasia ya bunge Cm watakuwa washini wa kile wanachota ndio kiitakuwa .

Je hili suala si sahihi lisimmiwe na Sheria na majaji na Mahakama . Wanasisa na vyama vya siasa kiwemo rais Vikae pembeni. Badala ya bunge la katiba basi iwe ni Mahakama ya Katiba. Inawezekana ni carzy idea lakini naon bunge lenyewe kama alivyo rais JK wawezeshe tu kuunda muswada wa kuunda mahaaKama ya katiba ambayo May be Jaji mkuu ndiyo atajua How, Who,when etc nyingine
 


Kuoneshwa wabunge wakikutana na some interesting professor hakukufanyi wewe mwananchi uwe umeshiriki! Taratibu zinasema wananchi washirikiwe, na sio wananchi-maprofessor tu! Ni vizuri viongozi wakajenga utamaduni wa kuheshimu wananchi hasa pale wanapoanza kulalamika. Topical Tanzania ina mikoa 27, hawa wakubwa wamefanya kikao Dodoma, Dar na Unguja. basi. Tena wakati huo wanatembeza muswa ulikuwa umeendikwa kwa lugha ya kiingereza! Kwa kitu nyeti kama katiba kwa nini ulipue namna hii, tena huku watu wakikuambia unalipuwa? Kisiwa chote cha Pemba hawajaulizwa na kama mtu hana TV basi atakuwa hajaona hata hayo mahojiano ya kamati na ma-professor!

Hapa ndio naona CCM wamewaongezea CHADEMA mtaji. Tabia zao za kufanya mambo kwa ujanjaujanja sasa zimeanikwa.
 

Mimi nafikiri hatua inayofuata ndio hasa sisi wananchi tutashirikishwa kutoa maoni kwenye tume itakayoundwa...

Na logic ni kwamba bunge linawakilisha wananchi katika muswada yote..hata hii ya katiba.
 
Narudia tena:

Nadhani kupiga kura inayohalalaisha upuuzi ni kubaya zaidi kuliku kutohusika kupiga kura hiyo; hata kama kura yako itakuwa inalipinga jambo hilo, bado rekodi zitaonyesha kuwa na wewe ulikuwa ni sehemu ya wale waliohalalisha upuuzi huo.
 

Mwanakijiji nimekupata, kuwa mwamuzi wa miwsho hapo ni spika aliyeteuliwa na JK, Ila nadhani wangekataa tu ili wananchi wajuwe moja kuwa ilkataliwa.

Unajuwa sometimes the message you send to the people matters big times...It signals what direction they should take.
 
Pasco, kama Lissu angeweka pingamizi kwanza na baadaye akapewa fursa ya kusoma hotuba ya wapinzani ni kitu gani kingefuata? Nadhani hapo ndipo panapotatiza. Ukishasema tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema Lissu alikuwa sahihi au alikosea

Pili, katiba ni yetu na katika mazingira ya kawaida haikutakiwa tusikie CCM au Chadema. Kilichotokea ni kuwa CDM wameona uporaji wa haki kama walivyoporwa hoja na JK, wanatueleza sisi wenye katiba. Sisi wote tunapaswa tu-bank katika peoples power kwasababu ndiyo silaha yetu kwa sasa. Kwa mantiki hiyo tujadili namna ya kuikoa katiba yetu na si katiba ya CDM.
 
Utaratibu uliopitishwa sasa unakunyima vipi kutokufikia hicho unachotaka?? yaani katiba nzuri uipendayo??
Usije na speculations? kwamba ccm vile na vile??


Unampa rais mamlaka ya kunichagulia nani akusanye maoni yangu. Hiyo huyu alipewa kazi na rais atareport kwa boss wake = rais na sio mimi =mwananchi. Mimi (wananchi wa Tanzania) simwamini rais kusimamia hela zangu (bank kuu - EPA) au kumamia mali zangu nyingeni (wanyama hai - Qarta, Kagoda,etc) itakuwaje nimwamini asimamie ujenzi wa nyumba yangu? Cement itabaki kweli?
 
Ameshasema watanzania ni makondoo,hilo la people's power liondoe kwenye msamiati wake....
 

Mkubwa, hebu tuanikie hapa kanuni ya Bunge inayosema Mbunge mmoja anaweza kuzuia muswada usisomwe mara ya pili.

Usitaje namba ya kifungu tena, umeshakitaja, itandike hapa hiyo kanuni neno kwa neno tuione.
 

Wananchi wote kwa pamoja wanawezaje kukusanya maoni yao??

Nani anaweza kuchagua watakaokusanya maoni kutoka kwa wananchi?? kwa niaba yao???
 

Mkuu soma thread yako, wewe mleta mada amesema mwenyewe yeye ndio uliuliza hayo maswali na umedai lissu amepiga chenga kukujibu wakati ulijibiwa vizuri tu.
Ila nakataa wanaokuita mnafiki, snitch nk mana kupishana mtazamo ni jambo la kawaida ndio ukubwa huo. Umetoa mtazamo wako na umetumia haki yako.
Tukuelimishe tu kuwa Chadema hawajakosea.
 
Mimi nafikiri hatua inayofuata ndio hasa sisi wananchi tutashirikishwa kutoa maoni kwenye tume itakayoundwa...
Na logic ni kwamba bunge linawakilisha wananchi katika muswada yote..hata hii ya katiba.

Kwa taratibu zilivyo (miswada) wabunge wanatakiwa wajadili muswada baada ya kupata maoni ya wananchi. Ni sawa na kwenda hotelini mhudumi anakuletea ugali bila kujua unakata chakula gani. Kumbe akitakiwa alete menu, wewe mteja unachagua anachotaka ndio ampe taarifa mpishi mengine yanafuata. Wabunge wa ccm wanajua tuna nini sisi wananchi?
 
Wananchi wote kwa pamoja wanawezaje kukusanya maoni yao??

Nani anaweza kuchagua watakaokusanya maoni kutoka kwa wananchi?? kwa niaba yao???

Kumbe walifanyaje walikwenda kwenye hiyo mikoa 3? Walipiga mbiu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…