Kwa Mungu kila kitu kinawezekana acha kujifanya unajua kila kitu.
Hivi Katiba imetoa maelezo gani kama ikitokea Mungu ameamua kuwachukua Rais wa JMT na makamu wake wote kwa pamoja kwa siku moja?
Tukio kama hili likitokea kikatiba hali inakuaje ndani ya nchi yetu?
Kama inawezekana familia moja kufiwa na watu zaidi ya watatu kwa pamoja na kwa saa moja,au kampuni au taasisi kufiwa na wafanyakazi wake zaidi ya watano kwa pamoja kwa siku moja. Sasa itashindikanaje Rais wa nchi na makamu wake kufa siku moja? Kwani Mungu ndiye apangae.
Yapi maelekezo ya Katiba yetu ya 1977 kama endapo hili likitokea?
Au ndio tutajua siku hiyo hiyo likitokea
Mkuu
Mpangilio ni huu hapa endapo rais na makamu wake wote hawapo anayetakiwa na katiba kushika madaraka ya rais ni>
1. Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania au kama naye kwa pamoja walivyo rais na makamu hawapo kutokana na ugonjwa, kujiuzulu au kufariki basi anayechukua nafasi ni
2. Jaji mkuu wa mahakama ya rufani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Angalizo: Msianze kupanga njama OVU
NUKUU katiba 1977 Ibara ya 37
"...(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b) na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kuteleza kazi na shughuli za Rais...."
Katiba ya ajabu sana imetengenzewa matobo mficho mengi ambayo hayakuonekanamiaka hiyo hadi kizazi cha sasa kimeanza 'testing of its effectiveness'