Katiba Mpya: Kakobe aungana na Wapinzani Jangwani

Katiba Mpya: Kakobe aungana na Wapinzani Jangwani

Kakobe alionekana mkutano wa jangwani ulioitishwa na vyama vya siasa akihutubia.Swali alienda na gari ya kanisa au binafsi? Maana ana kesi aliyoshitakiwa ya kutumia mali za kanisa kisiasa kuzunguka nazo wakati wa kumpigia kampeni za uraisi Augustino Lyatonga Mrema miaka ile.

Ni muhimu kujua jibu la swali hili kujua kama mali za kanisa hazijatumika ndivyo sivyo.
Alitumia V8 nyeupe haikuwa na nembo yoyote hivyo ni vigumu kuitambua ni binafsi au ya kanisa
 
labda mngeanza kujisafisha ndani ya chama chenu kwanza ndipo muwe na uhalali wa kuhoji ya wenzenu...kunatuhuma nyingi tu za chama kutumia mali za serikali ktk shughuli zake zikiwemo magari..helcopta za polisi..ila ya juzi kuwa2mia hadi mabalozi hapo mlionesha jinsi mlivyo juu ya sheria...
 
kakobe hata mungu anayemwabudu sijui ni yupi mtumishi wa mungu anakuwa wa ajabu kiasi hicho.

Ukiwashwa mkono utapata hela,je wewe unayewashwa nanihii unataka kufanywa nini? Mwenye jibu amsaidie yeye na wenzake wa lumumba
 
Kakobe alionekana mkutano wa jangwani ulioitishwa na vyama vya siasa akihutubia.Swali alienda na gari ya kanisa au binafsi? Maana ana kesi aliyoshitakiwa ya kutumia mali za kanisa kisiasa kuzunguka nazo wakati wa kumpigia kampeni za uraisi Augustino Lyatonga Mrema miaka ile.

Ni muhimu kujua jibu la swali hili kujua kama mali za kanisa hazijatumika ndivyo sivyo.

Hizi ndio thread watu wanazoanzisha wakiwa baa au vilabuni, au wakiwa wamepiga viloba.
 
Kama wewe ni mzalendo mbona huhoji kutumika STJ,SU kwenye shughuri za chama
 
Kwani wewe ni muumini wa full gosple fellowship? kama siyo unataka nini kama siyo umbeya. ulitakiwa kwenda ili ujue kila mtu kaenda na usafiri gani.
 
Kakobe alionekana mkutano wa jangwani ulioitishwa na vyama vya siasa akihutubia.Swali alienda na gari ya kanisa au binafsi? Maana ana kesi aliyoshitakiwa ya kutumia mali za kanisa kisiasa kuzunguka nazo wakati wa kumpigia kampeni za uraisi Augustino Lyatonga Mrema miaka ile.

Ni muhimu kujua jibu la swali hili kujua kama mali za kanisa hazijatumika ndivyo sivyo.

Acha ukuda wewe utapata faida gani ukisha jua? angekua ustadh ponda ungehoji?
 
Kwanza hao waliomfungulia kesi kakobe hawana akili, tena majinga sana, wanamshtaki kakobe kwa kifungu kipi kutoka wapi??

Sadaka sio michango, ukishatoa hupaswi kuuliza utendaji kazi wake, sadaka inatolewa kiimani na ili ubarikiwe na Mungu,

na kama huna imani hutajua kama umebarikiwa, na sadaka haina risiti sasa unashtaki kwa reference ipi?

Kakobe anaongozwa na roho, aongozwi na watoa sadaka, kakobe anafungwa na mamlaka ya Mungu sio ya ki binadamu,

Kakobe anamtumikia Mungu hamtumikii Mwanadamu, poleni sana mnaomuonea wivu Kakobe

Ahahahaha, hii balaa
 
Tangu nianze kujua harakati za Kakobe kwenye maenea mbalimbali sijawahi kumuona au kushuhudia Zakaria Kakobe amefanikiwa kwenye mipango yake yoyote.

Hata huku kwenye siasa alikoamua kuingia tena kwa mara ya pili atafeli tena, alifanya hivyo mwaka 95 akimsapoti Mrema wakafeli wote sasa ameingia tena hatujui ataondoka na nani.
 
haijalishi kafika hapo kivipi, mhimu ni kuwa kama mtanzania ana haki ya kukusanyika na pia kununua gari lake, achilia mbali kutoa maoni yake kama wewe tu unavyoandika hapa.
 
Kakobe sasa kafilisika ile mbaya. hata huko kwenye siasa alifeli muda mrefu. Nakumbuka mwaka 1995 alizunguka maeneo mengi ya nchi kuwashawishi wananchi wamchague AUGUSTINO LYATONGA MREMA ambaye hata hivyo hakuchaguliwa. huko ni kufeli. hata hawa anaowaunga mkono bila shaka amefeli
 
jambo lingine la kujiuliza kwa nini kakobe anatapatapa kiasi kwa nini asifanye kazi ya mungu mambo ya siasa awachie wanasiasa kwani mshika mawili moja humponyoka.
 
Kwani kakosa nini kumshauri rais juu ya katiba? sini raia wa Tanzania kama wengine? je nyinyi hamjawahi ku fail mipango fulani mliyopanga maishani mwenu?

yeye kama mwanaharakati wa dini kwa nini asitumie forum yake ya dini kumshauri rais anakwenda majukwaani kujumuika na wanasiasa.
 
hii hoja kwangu naona kama haina mashiko kwa jamii.sijui kwa wenzangu
 
yeye kama mwanaharakati wa dini kwa nini asitumie forum yake ya dini kumshauri rais anakwenda majukwaani kujumuika na wanasiasa.

kwa hiyo tatizo lako ni kwa nini alijumuika na wanasiasa au kwa nini alitoa maoni yake akiwa jukwaa moja na wanasiasa? mbona watumishi wa Mungu kama D.Tutu Afrika kusini ametoa mchango mkubwa katika ukombozi wa taifa hilo?,vipi Martin luther si alikuwa mtumishi wa Mungu na mwanaharakati?
 
Back
Top Bottom