Ndugu zangu Watanzania,
Baada ya hapo jana katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi pamoja na secretarieti Kupokelewa Kifalme na kwa kishindo kikuu Mkoani Singida. Hii leo tena Amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapo kwa kishindo kikubwa sana kilichotikisa Mikoa ya kanda ya kati nzima.
Ambapo ametoa hotuba nzito sana katika siku zake hizo mbili za ziara. Ambapo katika kuonekana kujibu mapigo ya Lissu . Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi amewataka wana Singida na watanzania wote kwa ujumla kukataa katakata kuvuruga umoja wetu ,kupandikizwa mbegu ya ubaguzi kwa misingi ya Udini ,ukabila ,ukanda na aina yoyote ile ya ubaguzi.
Amesisitiza na kuwaasa watanzania kuhakikisha tunadumisha umoja wetu na Amani yetu , ambayo ndio imekuwa nguzo kuu ya maendeleo yetu kama Taifa. Amesema tukatae kabisa kubaguana sisi kwa sisi.
Hotuba hii imeonekana kugusa mioyo ya watu wengi sana, ambao wameonyesha masikitiko yao na kuendelea kulaani kauli za kibaguzi na chuki zilizotolewa na Lissu wiki chache zilizopita,kauli ambazo zimeendelea kulaaniwa na kupigwa vita kila kona ya Nchi yetu na hata kupelekea CHADEMA kwa sasa kuchukiwa na watu wengi sana kwa kuonekana kuwa ni chama kinacho chochea ubaguzi na chuki kwa wananchi baada ya kuwa kimeishiwa hoja za kuwashawishi watanzania kukiunga mkono.
Kwa sasa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi anakwenda kuitikisa kanda ya kaskazini kwa kupiga mikutano mizito kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na kumalizia kwa kishindo Mkoa wa Tanga.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.