Pre GE2025 Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi amehitimisha ziara ya siku mbili mkoani Singida kwa kusambaratisha hoja zote za Lissu za kibaguzi

Pre GE2025 Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Emmanueli Nchimbi amehitimisha ziara ya siku mbili mkoani Singida kwa kusambaratisha hoja zote za Lissu za kibaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya hapo jana katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi pamoja na secretarieti Kupokelewa Kifalme na kwa kishindo kikuu Mkoani Singida. Hii leo tena Amehitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani hapo kwa kishindo kikubwa sana kilichotikisa Mikoa ya kanda ya kati nzima.

Ambapo ametoa hotuba nzito sana katika siku zake hizo mbili za ziara. Ambapo katika kuonekana kujibu mapigo ya Lissu . Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi amewataka wana Singida na watanzania wote kwa ujumla kukataa katakata kuvuruga umoja wetu ,kupandikizwa mbegu ya ubaguzi kwa misingi ya Udini ,ukabila ,ukanda na aina yoyote ile ya ubaguzi.

Amesisitiza na kuwaasa watanzania kuhakikisha tunadumisha umoja wetu na Amani yetu , ambayo ndio imekuwa nguzo kuu ya maendeleo yetu kama Taifa. Amesema tukatae kabisa kubaguana sisi kwa sisi.

Hotuba hii imeonekana kugusa mioyo ya watu wengi sana, ambao wameonyesha masikitiko yao na kuendelea kulaani kauli za kibaguzi na chuki zilizotolewa na Lissu wiki chache zilizopita,kauli ambazo zimeendelea kulaaniwa na kupigwa vita kila kona ya Nchi yetu na hata kupelekea CHADEMA kwa sasa kuchukiwa na watu wengi sana kwa kuonekana kuwa ni chama kinacho chochea ubaguzi na chuki kwa wananchi baada ya kuwa kimeishiwa hoja za kuwashawishi watanzania kukiunga mkono.

Kwa sasa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi anakwenda kuitikisa kanda ya kaskazini kwa kupiga mikutano mizito kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na kumalizia kwa kishindo Mkoa wa Tanga.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Amesambaratisha nini? Kwamba lisu ni muongo kumbe mtu wa Bara anaweza kununua ardhi zenji na wazenji hawaruhusiwi huku Bara? Eeh?
Lissu hana hoja zenye mashiko zaidi ya kujaa ubaguzi na chuki Binafsi kwa Mheshimiwa Rais wetu. Hata hivyo watanzania wameamua kumpuuza kabisa Lissu . Ndio maana unaona hata michango yake yakutaka gari jipya la kifahari inasua dua sana .hata wanachadema wenyewe wamegoma kuchangia.
 
Hoja hazisambaratishwi kama kupuliza majivu ya mabua halafu yachafue mashati na blauzi za watu.Siyo hivyo!😂😂😂
Lissu baada ya kuona hotuba ya Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi zimezima na kusambaratisha hoja zake ,ameamua sasa arejee tena Singida June 1 kujaribu kujisafisha.baada ya kugundua kuwa wananchi wana hasira kali zidi yake na wala hawataki hata kumuona.
 
Lissu hana hoja zenye mashiko zaidi ya kujaa ubaguzi na chuki Binafsi kwa Mheshimiwa Rais wetu. Hata hivyo watanzania wameamua kumpuuza kabisa Lissu . Ndio maana unaona hata michango yake yakutaka gari jipya la kifahari inasua dua sana .hata wanachadema wenyewe wamegoma kuchangia.
Rais ni Mzanzibar au Mmatumbi?

Katiba ya Zanzibar haioingani na Katiba yaMuungani ktk masuala kadhaa?

Mzanzibari anaweza kutamba na kufanya lolote Tanganyika,lakini Mtanganyika haruhusiwi!

Wanzibar ni Wabaguzi na wadini
 
Huyu atakuwa na fungus kwenye ubongo wake,sijui hana ndugu wa kumstua kuwa anajidhalilisha kwa hizi mada zake za kiduwanzi
Wewe ni wakusamehewa bure tu maana matatizo iliyonayo kichwani mwako yanahitaji msaada wa haraka na dharura.
 
Lissu baada ya kuona hotuba ya Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi zimezima na kusambaratisha hoja zake ,ameamua sasa arejee tena Singida June 1 kujaribu kujisafisha.baada ya kugundua kuwa wananchi wana hasira kali zidi yake na wala hawataki hata kumuona.
Baadaye uje utueleze ni kwa namna ipi Nchimbi alivyopangua hoja za TAML kama shaolin monk.Tunasubiri.
 
Rais ni Mzanzibar au Mmatumbi?!
Katiba ya Zanzibar haioingani na Katiba yaMuungani ktk masuala kadhaa?
Mzanzibari anaweza kutamba na kufanya lolote Tanganyika,lakini Mtanganyika haruhusiwi!
Wanzibar ni Wabaguzi na wadini
Kaa chini utulie ndio uandike vizuri ,kuliko hivi ulivyoandika utafikiri unakimbizwa nyuma.
 
Rais ni Mzanzibar au Mmatumbi?!
Katiba ya Zanzibar haioingani na Katiba yaMuungani ktk masuala kadhaa?
Mzanzibari anaweza kutamba na kufanya lolote Tanganyika,lakini Mtanganyika haruhusiwi!
Wanzibar ni Wabaguzi na wadini
Naenda kunywa komoni.Nikirudi naamini atakuwa amejikusanyakusanya na kujibu.
 
Ziara ya huyo jamaa, hata haileweki... Haina mvuto.. Ipo ipo tu kama pombe za kienyeji
Haina mvuto kwako wewe na upeo wako.lakini wananchi wameona namna ilivyo na tija ,kwa kuwa wamepata nafasi ya kusikilizwa kero zao mbalimbali na kupatiwa majibu.
 
Back
Top Bottom