Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Dkt. Bashiru Ally unasumbuka sana. Rais Samia tarehe 30, Aprili atashinda kwa asilimia 100%

Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Dkt. Bashiru Ally unasumbuka sana. Rais Samia tarehe 30, Aprili atashinda kwa asilimia 100%

Si sawa kubisha tu bila kuwa na hoja au kufikiri vizuri kidogo.
Serikali inatekeleza ilani ya chama na chama ndio kinatengeneza serikali kwa mfumo wetu....Hili hujui pia?
Kwa hivyo maendeleo ya nchi yanapangwa na chama.
Nadhani tumeelewana.
Hapo chama na nchi vinakutania wapi?
 
Hii ni mbinu mojawapo itumiwayo na watawala kubaki madarakani(waliosoma siasa wanajua hii).
Issue hapa nini tufanye kuzuia hii ni kujenga taasisi imara na huru km katiba nzuri mahakama na bunge huru.
Nani anafanya hili ni mtu mwenye mapenzi mema na nchi.
Shida tunampata wapi huyu mtu kwa kua viongozi wetu wanatokana na vyama vya siasa na km mfumo uliopo unabenefit chama kilichomadarakani nani ataunda taasisi imara.
Hapa ni mambo kadhaa tu yatokee apatikane rais asiye na kiu ya madaraka au ifanyike ile wanaita uprising km zile zilitokea nchi nyingine.
Chama cha siasa kumaintain status quo tulivofundishwa kinaruhusiwa kutumia dola lkn hii inaweza kupunguzwa pale tu tutakapokua na taasisi imara huru na zisizoingiliwa.

Ccm itatumia dola kubaki madarakani
 
Unamuitaje "mstaafu" labda mimi sijui kiswahili vizuri (maana ya kustaafu). Anafanya rough gani tena huko? Kwa sababu nafasi zote mbili (Katibu mkuu wa chama na Katibu mkuu Kiongozi) zote hakustahili. Ameleta mikakati michafu sana ndani ya CCM, mikakati ya manunuzi ya "wanachama" na amechangia uchafuzi mkuu wa October 2020. Angetulia tu na hiyo heshima aliyoheshimishwa ya ubunge wa kuteuliwa wakati akijipanga kwa siasa za majukwaani kama ana uwezo nazo, maana huyu amekuwa ni wa kuteuliwa mwanzo mwisho.
 
Uongo uongo tu. Amewanyang'anya mali za chama nyie ndio mnaoteseka. Bashiru kuzuia mama asipate asilimia 100 inasaidia nini? Wajinga tu ndio watafuatilia post yako na kuona umeandika topic ya maana.
Na wewe no mjinga mbona umefuatilia post?
 
So far, muacheni Bashiru pia aweze ku-heal, maana kimtazamo amekutana na changamoto ya quick shift in position toka SG kwenda CS na ndani ya siku 33 anakuwa mbunge wa kawaida. Bashiru apewe muda wa kupumzika kiakili ili atimize majukumu yake mapya ndani ya Bunge la JMT.
We will not give him that luxury... Hukuwepo kwenye mchakato wa kugombea ubunge wewe ndio maaana unaongea hivi. There was no mercy there. Ilikuwa ni mwendo wa kuliwa vichwa. Tuliwaambia kina Bashiru kuwa mmnajaza watu wasioweza kuwasaidia mbele ya safari. Sasa boti imetoboka, kila mtu aogelee kivyake kuokoa nafsi yake!
 
We will not give him that luxury... Hukuwepo kwenye mchakato wa kugombea ubunge wewe ndio maaana unaongea hivi. There was no mercy there. Ilikuwa ni mwendo wa kuliwa vichwa. Tuliwaambia kina Bashiru kuwa mmnajaza watu wasioweza kuwasaidia mbele ya safari. Sasa boti imetoboka, kila mtu aogelee kivyake kuokoa nafsi yake!
Poleni sana mkuu; siasa zina mambo yake. Hata akina mzee Makamba nao walilaumiwa baada ya uchaguzi wa 2010, ndio maana akaondolewa na kuingia Mukama
 
Na wasipoangalia li CCM litarudi kwenye zama zile za kukataliwa na wananchi, vyama vya upinzani wajipange sasa waweke safu mpya za uongozi zenye kueleweka hawa akina mnyika, mbowe lipumba mbatia uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo hawana jipya tena.
 
Mbona mnashusha hadhi ya neno "mstaafu"?? Hilo neno lina heshima yake mkuu. Hapo labda ungesema tu Mtumbuliwa at least, ndiyo haki yake.
 
Msilitumie vibaya neno mstaafu huyo mtu hajastaafu bali kafurushwa na rais wetu mpendwa mh.Samia,alipewa hiyo nafasi kimagumashi.
Bashiru alipaswa awe balozi nje ya nchi kwa kazi nzuri aliyoifanya.
 
Hayo ni mambo ya chama chenu wala sio ya nchi kwa ujumla.
Kwenye siasa kufuata makundi na falsafa fulani inaruhusiwa. Lakini hili jambo la kumchukia Bashiru kwa kua alitimiza majukumu yake vizuri na wewe ukaathirika si vema.

Kumgombanisha na Rais si sawa na ninaamini Rais ana vyombo ambavyo vinamsaidia na vitasema km Bashiru ni threat au la.

Ifike mahala tuwe tunareason kidogo tuache majungu na fitina ambazo hazitasaidia kujenga nchi hii.

Mimi na wewe tunaowajibu wa kujenga nchi hii kwa kutoa mawazo ya kujenga sio kufitinisha.

Rais pia anapaswa kutulia naona kuna miruzi mingi mno kipindi hichi.
 
Back
Top Bottom