Katibu Mkuu NATO, Jens Stoltenberg: Kuchoma Quran sio kosa

Katibu Mkuu NATO, Jens Stoltenberg: Kuchoma Quran sio kosa

Subuana watara wa samia huyu hapa kashikiwa mwamvuli [emoji116]hizi ndiyo akili za waisiharamu zilipo fikia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20230701-221558_Lite.jpg
 
Wa

Pro NATO Wapo? Na huo ndo msimamo wao dini zote zitoweke shetani ashike usukani, utasikia ushoga sio kosa ni uhuru wa mtu.
Ushoga sio kosa katika nchi zote za BRICS,
Africa Kusini na Brazil ndoa za mashoga zinaruhusiwa kwa katiba.
 
Mtego huo,au alikua mamruki,vipi kuhusu mamilion ya waislamu wanao uacha uislamu na kuwa wakristo hao unawaongeleaje,religion fanatic.

Sasa mtu kanunua kitabu kwa pesa yake, kwa hiyari yake mwenyewe kaamua kuchoma moto, kosa lipo wap?
Hebu jaribu ununue mbuzi au kuku!Nenda hadharani kamchome moto,yes si wako?Au jaribu kuchoma pesa na uonekane!Ndiyo,si pesa yako!
Mimi ni mkristu na hapa nimetoka kanisani,naijua mipaka yangu!
Uhuru wangu usiwe kikwazo kwa mwingine,amri kuu iliyobeba amri nyingine zote ni upendo!Ukiongozwa na hilo hutapata mikwaruzano kwenye jamii unayoishi!
Aliyetenda kitendo hicho ni mpuuzi,anayereact violently naye pia ni mpuuzi!
Moja ya advantage ya dini ni hofu juu ya maisha baada ya kifo!Hakuna sayansi imeweza kujibu hilo ila dini zimejibu kuwa kuna maisha baada ya kifo!Hilo limesababisha amani mahala pengi sana!Sasa mtu anayejaribu kuharibu kitu pekee kinachofanya mimi na wewe tuishi kwa amani huyo ni wa kudhibitiwa!
Hujiulizi kwa nini mtu mahakamani anaapa kwa kitabu hicho au Biblia?Hiyo inakupa tafsiri gani?
Acheni kushabikia ujinga!
 
Nikuulize wewe umeelewa nilichoandika?

Mtu kachoma kitabu chake mwenyewe unataka serikali ifanyaje? Huwa mnatumia hata akili japo kidogo?
Hiyo pesa aliyonunulia hicho kitabu,angeichoma ingekuwaje?
 
Hiyo pesa aliyonunulia hicho kitabu,angeichoma ingekuwaje?
Mkuu acha kupotosha huo ni upumbavu unafanya. Pesa ipo kwenye katiba tayari imewekwa hicho kitabu chenu hakipo kuna makosa gani kafanya?

Ukiaanza kuweka dhana ange ange haileti maana na sivyo ilivokuwa.
 
Hebu jaribu ununue mbuzi au kuku!Nenda hadharani kamchome moto,yes si wako?Au jaribu kuchoma pesa na uonekane!Ndiyo,si pesa yako!
Mimi ni mkristu na hapa nimetoka kanisani,naijua mipaka yangu!
Uhuru wangu usiwe kikwazo kwa mwingine,amri kuu iliyobeba amri nyingine zote ni upendo!Ukiongozwa na hilo hutapata mikwaruzano kwenye jamii unayoishi!
Aliyetenda kitendo hicho ni mpuuzi,anayereact violently naye pia ni mpuuzi!
Moja ya advantage ya dini ni hofu juu ya maisha baada ya kifo!Hakuna sayansi imeweza kujibu hilo ila dini zimejibu kuwa kuna maisha baada ya kifo!Hilo limesababisha amani mahala pengi sana!Sasa mtu anayejaribu kuharibu kitu pekee kinachofanya mimi na wewe tuishi kwa amani huyo ni wa kudhibitiwa!
Hujiulizi kwa nini mtu mahakamani anaapa kwa kitabu hicho au Biblia?Hiyo inakupa tafsiri gani?
Acheni kushabikia ujinga!
Unajaribu kulinganisha vitu visivyolingana. Kuku, mbuzi au pesa vyote vimetungiwa sheria. Kuna sheria za Wanyama. Niambie kuna sheria za vitabu vya dini?

Yote uliyoongea ni kutengeneza sympath tu lakin haiondoi ukweli kwamba jamaa hana kosa lolote. Huo ndio msingi wa hoja ya mkuu wa NATO.
 
Mkuu acha kupotosha huo ni upumbavu unafanya. Pesa ipo kwenye katiba tayari imewekwa hicho kitabu chenu hakipo kuna makosa gani kafanya?

Ukiaanza kuweka dhana ange ange haileti maana na sivyo ilivokuwa.
Mahakamani unaapishwaje kwa kitabu ambacho hakitambuliki na katiba?Acha upumbavu!
 
Mahakamani unaapishwaje kwa kitabu ambacho hakitambuliki na katiba?Acha upumbavu!
Wewe ndio kichwa ngumu huelewi mantiki inaonekana uliwapa/unawapa shida sana watu wanaokuelekeza jambo.

Akili nzito kama nzi.

Kuna sheria ya kulinda hicho kitabu? I quote hapa kama ipo. Wapumbavu kama nyie ndio aina ya wale wanaoandama huko kuforce mtu achukuliwe hatua kulingana na hisia tu sio sheria.
 
Wewe ndio kichwa ngumu huelewi mantiki inaonekana uliwapa/unawapa shida sana watu wanaokuelekeza jambo.

Akili nzito kama nzi.

Kuna sheria ya kulinda hicho kitabu? I quote hapa kama ipo. Wapumbavu kama nyie ndio aina ya wale wanaoandama huko kuforce mtu achukuliwe hatua kulingana na hisia tu sio sheria.
Kama hutaelewa na hapa basi una tatizo!Usiwe mvivu wa kusoma,jielimishe upate maarifa kijana!
Hotuba ya Rais Benjamin William Mkapa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania - BAKWATA - Dodoma tarehe 29 Julai, 1999 Mheshimiwa Mufti Sheikh Mkuu wa Tanzania, Hemed bin Juma bin Hemed;
Waheshimiwa viongozi wa Bakwata;

Wajumbe wa Mkutano Mkuu;

Wageni waalikwa;

Mabibi na Mabwana


Assalam Alaykum!

NINAYO furaha kubwa kuwa nanyi, na kuzungumza nanyi, siku hii ya leo. Hivyo, napenda nikushukuru sana Mheshimiwa sana Mufti, Sheikh Mkuu wa Tanzania, kwa heshima uliyonipa kwa kunialika nijukumuike na kuzungumza nanyi. Nina uhakika wengi wenu nimewahi kukutana nao niwapo mikoani kwenu kwenye ziara rasmi, lakini hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi nyote hivi kwa pamoja. Ndiyo maana kwangu hii ni fursa nzuri sana na ya kipekee. Nawashukuruni sana.

Nawashukuru pia kwa mapokezi mazuri, na nyuso za bashasha mlizonipokea nazo. Upendo na kuheshimiana ni sifa mojawapo za Ucha-Mungu. Na nyinyi leo mmeudhihirisha kwa wema wenu kwangu na mapokezi haya. Ahsanteni.

Mheshimiwa Mufti,

Baada ya kupata mwaliko wenu nilitafakari kwa kina, na kisha kuamua kuzungumza nanyi juu ya mambo makubwa matano:

Kwanza, nitazungumzia dhana ya uhuru wa imani za dini;

Pili, umuhimu wa kujenga, badala ya kubomoa, madaraja ya kijamii;

Tatu, umuhimu wa kurekebisha kosoro bila kuanzisha mpya;

Nne, umuhimu wa elimu, na

Tano, umuhimu wa umoja ndani ya kila dini.

Dhana ya uhuru wa imani za dini

Ndugu wajumbe,

Tanzania ni nchi inayotawaliwa, na mambo yake kuendeshwa, kwa misingi iliyowekwa na Katiba, sheria na kanuni mbalimbali. Uhuru wa kila mwananchi wa kuamini na kuabudu kupitia dini aipendayo nao unatokana na haki za msingi za raia zilizowekwa na Katiba. Napenda ninukuu sehemu zinazohusika za kifungu cha 19 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

"19(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

(2) Bila ya kuathiri sheri zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli ya Mamlaka ya Nchi".

Ndugu Waislamu,

Katiba yetu, ambayo ndiyo sheria mama ya Taifa letu, imetoa uhuru wa kutosha kabisa wa kila mwananchi mwenye nia njema kuamini na kufuata dini aipendayo, au dhehebu la dini alipendalo, na kuabudu kwa misingi ya dini yake, au dhehebu la dini linalohusika. Isitoshe, Katiba hiyo hiyo imetoa pia uhuru kamili wa kutangaza na kueneza dini.

Lakini, katika duni hii hakuna uhuru wa asilimia 100 - uhuru ambao hauna mipaka yoyote ile. Kwa mfano, pamoja na uhuru wa kuabudu, haiyumkiniki mtu akaingia Msikitini kuswali na viatu, au akiwa hana udhu, kwa sababu tu ya kudai haki ya kuabudu atakavyo!

Mipaka ya uhuru wa kuamini, kuabudu na kutangaza dini ipo ya aina mbili. Mpaka wa kwanza ni sheria, kanuni na taratibu za nchi, na za dini yenyewe. Ndiyo maana katiba ya nchi katika kutoa uhuru inasema wazi kuwa uhuru huo usiathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali nayo itakuwa haijatimiza wajibu wake kwa wananchi isiposimamia vizuri sheria za nchi, lakini kwa usawa, bila chuki, bila upendeleo na bila huba. Hivyo haiwezekani katika nchi yetu turuhusu zijengeke hisia kuwa zinakuwepo serikali za Waislamu au za Wakristo. Rais ana dini yake, kama ilivyo kwa raia yeyote mwingine. Lakini awapo kazini, yeye na serikali yake, na Chama chake cha siasa, wanatakiwa wasihusudu na wasishabikie dini yoyote ile. Sijui kwa vyama vingine, lakini CCM haina dini, na serikali yake haina dini. Lakini tunawahimiza wanachama wetu, na wananchi wote wawe wacha Mungu na hivyo kuwa raia wema, na kuheshimu utu na dini za raia wote, na binadamu wote.

Aidha, kama tunavyosema, sheria ni msumeno. Lazima iwatendee watu wote haki sawa. Hivyo kila dini na kila dhehebu, lina wajibu sawa na lingine la kuzingatia sheria za nchi katika kuabudu na kutangaza dini. Na ni wajibu wa viongozi wa kila dini na kila dhehebu kuhimiza waumini wao kuheshimu sheria za nchi, na kuheshimu imani za watu wengine.

Hivyo, mpaka wa pili, unaotokana na pia haja ya kuheshimu usawa, haki, na sheria, ni wajibu wa kila mtu kuheshimu uhuru wa wengine kwenye mambo ya dini. Kwa maneno mengine, uhuru wa mtu mwingine naye kuamini, kuabudu na kutangaza dini yake bila kuzuiwa isivyo halali, na bila kutukanwa, kukebehiwa au kudharauliwa.

Na ninavyoelewa mimi, hakuna dini au dhehebu kubwa la dini duniani linalohalalisha ubaguzi kwa misingi ya dini, au linalowataka viongozi au wafuasi wake wazue zogo na waumini wa dini nyingine. Tuna hiari ya kushawishiana kubadili dini, lakini kazi hiyo, tunayoiona ni kazi ya Mwenyezi Mungu, tuifanye kwa kuzingatia sifa za Mwenyezi Mungu - sifa za ucha-Mungu - ambazo kamwe haziwezi kuwa kebehi, matusi, dharau au fujo.

Kuna hadithi ya Kikristo ambayo inathibitisha umuhimu wa hoja hii. Kulikuwa na Mapadre wawili, mmoja wa Anglikana na wa pili wa Kikatoliki. Walikuwa hawaelewani, na walikuwa wanakaribia kuchukiana. Hatimaye wakakubaliana kuwa huo haukuwa mtazamo wa kiadilifu; wakaamua kusahau yaliyopita na kuanza mahusiano mazuri.

Muanglikana akamwambia Mkatoliki:

"Tuna kila sababu ya kuwa na mahusiano mazuri. Wote tunafanya kazi ya Mwenyezi Mungu".

Mkatoliki akamjibu:

"Ni kweli. Kwa hiyo tufanye kazi yake Mwenyezi Mungu kwa uwezo wetu wote: Wewe kwa njia zako na mimi kwa njia zake Yeye Mwenyezi Mungu".

Ndipo ikabainika hapakuwa na azma yoyote ya kusahau yaliyopita na kujenga mahusiano mazuri. Mtazamo kama huu una athari hizo hizo kati ya watu wa dini mbalimbali kama ulivyo navyo kati ya watu wa dini moja!!

Ndugu zangu,

Mimi sio Muislamu, lakini bado nakumbuka maneno ya busara ya Rais Mstaafu aliyenitangulia, Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, aliyoyasema kwenye Baraza la Idd, mwaka 1995. Naomba mniruhusu nimnukuu. Alisema:

"Kwa vile Qur'an ni mwongozo wa Waislamu hebu tuone inatuelekeza nini kuhusu uhusiano wetu sisi Waislamu na wale ndugu zetu wasiokuwa Waislamu, na hasa ni ipi njia bora ya kutangaza dini ya Kiislamu kwa waumini wa dini nyingine. Qur'an tukufu katika sura ya 16 aya ya 125 inaelekeza hivi:

'Waite (watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu). Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye (pia) anayewajua walioongoka.'"

Mzee Mwinyi aliendelea na kusema:

"Haya ndio maelekezo ya Waislamu katika utangaza dini yao. Kufanya kinyume cha haya, ni uasi".

Vile vile, Qur'an hiyo hiyo katika sura ya 6, aya ya 108, inatukemea na kututahadharisha kwa kusema:

'Wala msiwatukane wale ambao wanaoabudu, kinyume cha Mwenyezi Mungu, (ili) wasije (na wao) wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri zao bila kujua...'

Maneno haya maana yake ni kwamba mkitukana dini za watu wengine watu hao nao watalipiza kisasi kwa kumtukana Mungu wetu. Katika hali hiyo lawama itakuangukieni nyinyi mlioanza sokomoko hilo. Itakuwa nyinyi ndio mliomtukanisha Mwenyezi Mungu wenu".

Ndugu Waislamu,

Huu ni mwongozo ulio wazi kabisa, na uliosheheni busara na hekima. Ni mwongozo wa kuweka mazingira bora ya kila mtu kuabudu na kutangaza dini kwa staha, kwa ustaarabu, kwa upole, kwa heshima, kwa unyenyekevu na kwa upendo, mambo ambayo ni sifa za ucha- Mungu wa kweli. Mwongozo huu katika Qur'an tukufu kweli ningependa usiwe wa Waislamu tu bali uwe ndio mwongozo wa kila mwananchi, wa kila dini na kila dhehebu la dini.

Najua kwenye mambo ya imani za dini kila muumini anaamini yeye ndiye sahihi, ndiye anayeabudu sawa sawa, na anayefuata maagizo ya Mwenyezi Mungu. Hilo ni jambo la kawaida, na ndiyo maana akawa mfuasi wa dini yake, au dhehebu la dini alilonalo. Lakini ukweli ni kuwa sote tumeumbwa na Mwenyezi Mungu, na peke yake ndiye anayetujua sote, aliyeopotea na aliyeongoka. Qur'an tukufu imesema, kama nilivyonukuu hivi punde, "Hakika Mola wako ndiye anayejua aliyepotea katika njia yake na ndiye pia anayewajua walioongoka".

Hivyo katika siku ya leo nawaomba Watanzania wote tudumishe amani, upendo na ushirikiano, na tuheshimiane sote bila kujali tofauti zetu za dini, na bila kuwakebehi au kuwadharau wanaoabudu tofauti nasi. Tusiingilie kazi ya Mwenyezi Mungu kwa sisi nasi kupimana ni nani kati yetu kapotea na ni nani ndiye kaongoka. Kazi hiyo tumwachie mwenyewe Mola wetu. Wajibu wetu sisi ni kupeana nafasi kila mtu aabudu na kuamini aonavyo inafaa. Na tunapokaribishana kwenye dini zetu, tufanye hivyo si kwa kukashifu dini za wengine au kuwakebehi, bali kwa kufundisha kwa upendo, heshima na huruma.

Mambo haya nayasema hapa si kwa sababu yanawahusu Waislamu tu, bali kwa vile nimefurahishwa sana na mwongozo ulio wazi wa Qur'an tukufu juu ya njia bora ya kutangaza dini kama nilivyoinukuu hapa. Wito wangu leo ni kwa Watanzania wote, wa dini zote, kwamba tuzingatie mwongozo huo ambao ndiyo salama yetu katika kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Watanzania wote kama ambavyo siku zote tumezoea.

Tujenge badala ya kubomoa madaraja ya kijamii

Ndugu Waislamu,

Katika jamii yoyote yapo mambo ambayo yakiendelezwa yanasaidia kuimarisha umoja, mshikamano, ushirikiano na amani. Hayo ni sawa na madaraja yanayounganisha watu wa aina mbalimbali, dini mbalimbali, rangi mbalimbali, na kabila mbalimbali. Lakini yapo pia mambo ambayo yakiendekezwa yatavunja madaraja hayo, na kila kikundi katika jamii kikajali maslahi yake peke yake na kujitenga na jamii kubwa zaidi wakiwemo wengine wenye dini, kabila, jinsia au rangi tofauti.

Siri mojawapo ya amani na mshikamano katika Taifa letu la Tanzania ni madaraja yaliyojengwa tangu wakati wa kupigania uhuru - madaraja yaliyounganisha watu wa dini zote, kabila zote, rangi zote na jinsia zote katika kupigania uhuru na kujenga Taifa jipya la Tanzania. Leo tunafika mahali ambapo Watanzania wanajitambulisha kwanza kama Watanzania, kabla ya kujitambulisha kama watu wa kabila fulani, au dini fulani. Tumeunganishwa na uzalendo wetu, na mapenzi yetu kwa nchi hii.

Juzi nilikuwa mkoani Kagera kuadhimisha Siku ya Mashujaa ambayo mwaka huu iliungana na kumbukumbu ya miaka 20 tangu vita dhidi ya Nduli Iddi Amin kwisha. Baadhi ya shughuli nilizofanya ilikuwa kutembelea mnara wa kumbukumbu pale Kaboya, na kutembelea shamba walikozikwa mashujaa wa vita hivyo pale Kaboya. Niliyasoma kwa makini sana majina ya vijana wale waliofia nchi yao ya Tanzania, vijana walioonyesha uhodari, ujasiri na uzalendo wa upeo wa juu kabisa. Walikuwepo vijana wa kabila mbalimbali, dini mbalimbali - Waislamu kwa Wakristo - na wengine wenye imani zao za asili, wanaotoka pembe mbalimbali za nchi yetu. Wote hawa walikwenda mstari wa mbele kama watu wamoja, wakapigana na kufa kiume bega kwa bega kama Wanzania wanaolinda nchi yao na heshima yake. Mimi nina uhakika hawakuulizana dini au kabila zao.

Hayo ndiyo madaraja yanayosaidia kudumisha umoja wetu. Tuyaenzi. Maana siku hizi zipo dalili za wazi za baadhi ya wenzetu kuanza kuvunja madaraja hayo kwa kupuuza yale yanayotuunganisha, na kutukuza yale yanayotutofautisha - udini, ukabila, ubaguzi wa rangi au jinsia, na eneo analotoka mtu. Tusiwakalie kimya watu hao. Kidogo kidogo wanavunja madaraja yetu ya kijamii na hatuwakemei na kuwatenga vya kutosha. Leo, wapo wanasiasa au viongozi wengine wa jamii, wanaozungumzia wazi wazi lugha ya udini, ukabila na majimbo. Tusiwapuuze na wala tusiwaonee haya.

Tufungue macho yetu tuone yanayotokea nchi jirani na nyingine. Mbegu inayopandwa leo ya udini, au ukabila au umajimbo itachipua na kuzaa matunda yake, kama si wakati wa uhai wetu basi wakati wa uhai wa watoto wetu au wajukuu zetu. Sasa mimi sijui ni nani angependa kizazi chake kijacho kiishi katika nchi kama vile Somalia, Yugoslavia au Burundi. Kama hatutaki, basi sisi wenyewe tusishabikie wapandaji wa mbegu hizo, na wala sisi wenyewe tusikubali kulaghaiwa tukajikuta tumeshiriki kupanda mbegu hizo. Tuwatenge na kuwazomea wapandaji wa mbegu hizo!

Turekebishe kasoro, tusianzishe mpya

Ndugu Waislamu,

Mojawapo ya visingizio vinavyotumiwa na wanaotoka kuvunja madaraja ya umoja wa utaifa wetu ni kwamba watu wa eneo fulani wameachwa nyuma, au watu wa dini fulani hawapewi nafasi fulani katika uongozi wa nchi na jamii. Siwezi kukataa kuwa inaweza kukawepo na kasoro katika mambo hayo. Lakini kila kasoro ya namna hiyo ina historia yake na maelezo yake. Tusipoangalia tutahangaika kutibu dalili za ugonjwa, badala ya kutibu ugonjwa wenyewe.

Zipo nchi katika dunia yetu ambapo watu wa dini fulani, au watokao katika eneo fulani, kwa makusudi wanabaguliwa au hawapewi nafasi sawa za elimu au madaraka. Bado sijapewa ushahidi kwamba CCM na serikali yake inayo, au imewahi kuwa na, sera ya aina hiyo. Kama yuko mwenye ushahidi huo ninaomba niletewe na hatua zitachukuliwa mara moja kurekebisha hali hiyo. Kwangu mimi kasoro ya namna hiyo ni rahisi kuirekebisha.

Narudia. Hakuna sera ya CCM na serikali yake ya kumbagua mwananchi yeyote, kwa jamb lolote, kwa misingi ya dini, kabila, rangi, eneo atokalo au jinsia yake. Pale zinapoonekana kasoro, chimbuko lake si sera - ni historia, ni hulka za watu, ni maandalizi ya watu, na ni vitendo vya mtu mmoja mmoja. Kasoro za namna hii ni ngumu zaidi kuzirekebisha na zinachukua muda mrefu zaidi kuzimaliza.

Tushirikiane kurekebisha kasoro hizo, lakini tuwe waangalifu kuhakikisha kuwa kwa kufanya hivyo hatuanzishi kasoro nyingine mpya. Kigezo kimojawapo cha kuonyesha kama kweli nia yetu ni kurekebisha kasoro bila kuanzisha nyingine ni kuyachukulia matatizo haya kama matatizo ya kitaifa na wala sio matatizo ya kabila fulani au dini fulani.

Mimi naamini kuwa, kwa maana ya mapungufu ya huduma na haki, hakuna matatizo ya Waislamu, yapo matatizo ya kitaifa yanayohusu Waislamu. Na ipo tofauti kubwa kati ya mitazamo hii miwili. Unaposema haya ni matatizo ya Waislamu, tayari umetugawa, na wala si sahihi maana Waislamu hao tunaishi nao katika jamii moja na taifa moja. Familia nyingine zimechanganyika Waislamu na Wakristo. Siamini kuwa yupo Mtanzania wa dini moja ambaye hana rafiki wa dini nyingine. Furaha yao ni yetu sote, na huzuni yao ni yetu sote.

Vibaya zaidi ni kuanza kuona matatizo haya kama vile ni ya dini moja dhidi ya nyingine, kabila moja dhidi ya kabila jingine. Kwa mtazamo huo ufumbuzi wa tatizo moja lazima utazua tatizo jingine. Mtazamo sahihi ni kuwa tatizo ni la kitaifa, la kijamii, na ufumbuzi wake ni wa kitaifa na kijamii. Na ufumbuzi huo usiwe wa kumfanya mmoja ajione ameshinda na mwingine ajihisi ameshindwa, bali wote - wa kabila zote, dini zote na rangi zote, na jinsia zote - waone wameshinda.

Tukubali pia kuwa matatizo yenye chimbuko lake katika historia hayawezi kumalizwa siku moja. Yatachukua muda. La muhimu ni kuanza kuyashughulikia. Na hapa napenda niwahakikishieni kuwa niko tayari, na kwa kweli nimeshaanza kuyashughulikia matatizo ya kitaifa yanayohusu Waislamu. Katika uteuzi ninaoufanya mimi ninajitahidi sana kila inapowezekana kuzingatia uwiano mzuri baina ya dini, kabila, jinsia na kadhalika. Lakini hatuwezi pia kuweka kanuni ya kudumu ya kugawa vyeo kwa misingi ya dini, kabila, jinsia na kadhalika. Kwa faida ya taifa, ni vizuri zaidi tugawe vyeo kwa vigezo vya ujuzi, uwezo na upimaji makini wa matokeo ya kazi. Kuna maeneo mtu unaweza kufumba macho kwa muda, lakini zipo taaluma ambazo haiwezekani kufumba macho.

Mimi siamini yuko mtu yeyote ambaye akienda hospitali anatafuta daktari wa dini yake au kabila lake; la muhimu zaidi ni umahiri wa daktari. Nani atataka kupasuliwa na daktari aliyekuwa wa mwisho darasani kwake kwa vile ni wa dini yake, na amwache yule aliyekuwa wa kwanza na bingwa wa upasuaji lakin ni wa dini tofauti? Kama vile mtu binafsi anavyotaka kutibiwa na daktari aliyehitimu vizuri, bila kujali dini yake au kabila lake, vivyo hivyo taifa linahitaji kuongozwa na watu waliohitimu vizuri na wenye sifa na uwezo bila kujali eneo watokalo, jinsia zao, au dini zao. Tukijiachia tutafika mahali ambapo kila uteuzi ninaofanya, au unaofanywa kwingineko serikalini, unapimwa kwanza si kwa uwezo wa walioteuliwa bali kwa kuangalia dini au kabila zao tutakuwa tumelifikisha taifa letu mahali pabaya sana, na pa hatari kubwa, ambapo haitakuwa rahisi kujitoa.

Nasema, panapowezekana ninaweza kufumba macho lakini huo si ufumbuzi wa kudumu, na ukiendelezwa unaweza kuanzisha matatizo mengine na kuzidi kujenga chuki na uhasama. Ufumbuzi wa kweli, na wa kudumu, ni kusaidia kumpa kila mwananchi, wa kila dini, jinsia, kabila na kadhalika ajiendeleze kielimu kwa kadri ya uwezo wake bila kubaguliwa kwa sababu ya dini, jinsia, kabila au eneo analotoka.

Hivi ndivyo tunavyofanya, na hakuna mchujo wowote katika kuandikisha watoto shule, kwenda sekondari, au vyuo vikuu, au katika ajira, unaofanywa kwa msingi wa kuwabagua watu wa dini fulani. Hiyo nawahakikishieni kabisa, na kama yupo mwenye ushahidi kwamba mwanafunzi fulani amezuiliwa kuendelea na masomo kwa sababu tu ya dini yake, jinsia yake au kabila lake, basi wanaohuska wajulishwe na ikishindikana hata mimi mwenyewe nijulishwe na tutarekebisha mara moja na kuwachukulia hatua kali wafanyao hayo, kama watakuwepo.

Kwa tahadhari tu, pengine nitumie nafasi hii kurudia onyo langu kali kwa yeyote ambaye atambagua mtu yeyote kwenye elimu, kwenye ajira na kupandisha cheo, kwenye kutoa leseni au haki mbalimbali, kwa msingi wa dini, jinsia, kabila, rangi au eneo analotoka mtu huyo. Siwezi kuruhusu mizizi ya ubaguzi ianze kuota, nitachukua hatua kali pale ushahidi wa ubaguzi utakapoonekana. Lakini pamoja na kutovumilia ubaguzi tuepuke pia kugeuza hisia kuwa kweli na kukuza tatizo kuliko hali halisi ilivyo.

Umuhimu wa Elimu

Ndugu Waislamu,

Elimu ndiyo maandalizi muhimu kuliko yote ya sifa na uwezo wa kazi kwa ujumla, na uongozi katika taifa. Na kadri dunia inavyobadilika tuingiapo karne mpya, ndivyo umuhimu wa elimu utakavyozidi. Kwa jambo hili hatuna hiari ni lazima tusomeshe vijana wetu, wa kike na wa kiume. Elimu ya dini ni muhimu sana kutuandaa kwenda peponi, lakini elimu ya watu binafsi, na taasisi za dini, kujenga na kuendesha shule tangu za chekechea hadi vyuo vikuu, lakini bila ubaguzi wala ya dunia ni muhimu sana kwa maisha na utendaji wetu katika dunia. Elimu zote tuzipe uzito unaostahili.

Serikali inajitahidi sana kupanua nafasi za elimu. Ndio maana tukafungua milango ka watu binafsi na taasisi za dini kujenga na kuendesha shule tangu za chekechea hadi vyuo vikuu, lakini bila ubaguzi wala kujenga chuki, na kuzigatia maadili ya taifa, uzalendo, usawa na heshima kwa wote. Kila ninapokutana na viongozi wa dini zote na madhehebu zote, ninawahimiza sana wawekeze katika kuelimisha vijana wetu. Kasi za kuitikia wito huo zinapishana, lakini si kwa sera ya serikali, bali kwa jinsi wahusika wenyewe na wahisani wao wanavyoitikia.

Kwa vile taasisi zetu, ikiwemo za dini, hazina uwezo peke yao kujenga na kuendeha shule nyingi ingekuwa vizuri wakiendelea kujenga mahusiano mazuri na wahisani wao kutoka nchi za nje wasaidie ujenzi wa shule sambamba na misaada ya kidini. Napenda niwahakikishie kuwa serikali itazidi kuunga mkono jitihada za jumuiya yoyote ya dini inayotaka kujenga na kuendesha shule na vyuo, ili mradi ziwe shule za kuandaa vijana kwa utumishi mzuri wa taifa na kwa kuzingatia maadili ya uzalendo, utaifa, haki, usawa na heshima.

Mojawapo ya misaada serikali inayotoa kwa taasisi za dini zinapoamua kujenga na kuendesha huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji ni msamaha wa ushuru wa forodha.

Tunatambua kuwa mara nyingi taasisi zetu za dini zinapata uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uhisani wa taasisi nyingine za dini nchi za nje, na ndio maana serikali ikaamua kusamehe ushuru wa vifaa vinavyohusika viingiapo nchini. Misamaha hiyo si kidogo; kwa mwaka ni fedha nyingi sana ambazo serikali ingeweza kuzitumia kwa mambo mengine. Kwa mfano katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi uliopita wa Juni, 1999 misamaha ya ushuru wa forodha kwa taasisi za dini ilifikia sh. 9.8 bilioni, sawa na bajeti za miaka 3 za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Ni matumaini yangu kuwa taasisi za Kiislamu nazo zimetumia kwa kikamilifu misamaha hiyo kujenga na kuendesha huduma za jamii. Tumieni zaidi msaada huo wa serikali ambao tutaendelea kuutoa licha ya malalamiko ya wengine kuwa misamaha hiyo ni mikubwa mno na inaipunguzia serikali mapato yake. Iwapo mnapata matatizo katika kupata misamaha hiyo tujulisheni tuone namna ya kuikwamua. Lakini wito wetu kwa taasisi zote za dini ni kuwa wasimamie vizuri vifaa vinavyosamehewa ushuru ili kweli vitumike kwa lengo lililokusudiwa katika kutoa msamaha na kwa manufaa ya wananchi wote. Nasema hivyo kwa sababu mojawapo ya malalamiko juu ya misamaha hiyo ni kwamba wapo watu wachache wasio waadilifu katika baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya serikali wanaotumia vibaya misamaha hiyo. Lakini mimi ninaamini kuwa ninyi viongozi wa dini mnao uadilifu wa kutosha na uwezo wa kuwadhibiti watendaji wenye tabia hiyo ndani ya taasisi za dini. Tusaidieni kufanya kazi hiyo ili kupunguza malalamiko yanayoweza kuchafua jina zuri la taasisi zetu za dini.

Baada ya kusema hayo lazima nishukuru sana taasisi za dini kwa mchango wao mkubwa sana katika ujenzi na uendeshaji wa huduma za jamii nchini. Kwa hakika, bila mchango wa taasisi za dini hasa za Kikristo, Kiislamu na Kihindu hali yetu ingekuwa mbaya zaidi. Kwa mfano, kati ya hospitali 224 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 1997, ni asilimia 36.2 tu ndizo zilikuwa zinamilikiwa na serikali. Idadi ya vituo vya afya ilikuwa 344, na serikali ilimiliki asilimia 82.6. Idadi ya zahanati ilikuwa 4,276 na serikali ilimiliki asilimia 58.7 tu ya zahanati hizo. Nyingi ya huduma zilizobaki zilikuwa za taasisi za dini, na chache za mashirika ya umma na watu binafsi.

Kwenye elimu hali kadhalika. Mwaka 1997 shule za sekondari zilizosajiliwa zilikuwa 709 na kati ya hizo serikali ilimiliki asilimia 49 tu, yaani chini kidogo ya nusu. Nyingi ya zilizobakia ni za taasisi za dini, na chache za watu binafsi na mashirika mengine yasiyokuwa ya serikali. Aidha, vipo vyuo vingi vya ufundi vya taasisi za dini zote; na vyuo vikuu vipya vinavyosajiliwa sasa vingi ni vya taasisi za dini zikiwemo za Wakatoliki, Waprotestanti na Waislamu. Napenda nitumie nafasi hii kurudia tena shukrani zangu za dhati kwenu, na kwa taasisi zote za dini, kwa mchango wao na wenu huu mkubwa. Nadhani tunaweza kufanya mengi zaidi tukiendelea kushirikiana. Serikali mlango wake uko wazi na tupo tayari kusaidia na kupokea ushauri wenu juu ya namna ya kuzidi kuongeza mchango wenu katika mambo haya.

Umoja ndani ya dini

Ndugu Wajumbe,

Jambo jingine linalonisikitisha sana ni kuona mifarakano na utengano miongoni mwa waumini wa dini moja au madhehebu ya dini. Tatizo lipo miongoni mwa Wakristo kama lilivyo kwa Waislamu. Tofauti inakuwa tu kwenye viwango vya mifarakano yenyewe na athari zake.

Hali hiyo inahatarisha ucha Mungu wetu, na inahatarisha pia amani na usalama katika nchi yetu. Hivyo tatizo hili haliishii kwenye dini inayohusika, ni tatizo la jamii nzima. Ni tatizo pia la serikali yenye jukumu la kulinda usalama wa raia wake wote na mali zao. Serikali haiwezi kuacha kutekeleza jukumu hilo pale mifarakano hiyo inapohatarisha usalama wa raia na mali zao. Ndiyo maana napendakutoa wito kwa waumini na viongozi wa dini zote kuhubiri amani, upendo na umoja, badala ya magomvi, chuki na mifarakano.

Lakini kwa kujua mafundisho ya dini zote kubwa ni pamoja na upendo, umoja, kuvumiliana na kusaidiana napata taabu kidogo kuelewa kwa nini tunaachia magomvi yaanze na kukua, ndani ya dini moja au kati ya dini au dhehebu moja na dini au dhehebu la dini jingine, mpaka kufikia kuhatarisha amani na usalama. Ninavyoelewa pia kuwa kila dini inayo katika misahafu yake utaratibu wa kupatanisha waumini na kusuluhisha migogoro inapotokea. Kila waumini wangetumia utaratibu huo, magomvi yasingefika mahali pa kuhatarisha amani na usalama wa wananchi na mali zao, hivyo kulazimisha serikali kuingilia kati kwa maslahi ya wananchi walio wengi, wasio na hatia.

Aidha, usimamizi wa utaratibu wa usuluhishi ndani ya kila dini ni wajibu wa viongozi wa dini inayohusika. Ingawa nimewahi kuombwa kusaidia kutatua migogoro ya kidini, napata taabu sana kukubali ombi hilo maana siamini ninao ujuzi wa dini, hata ule wa dini yangu mwenyewe, wa kutosha kukubali jukumu la usuluhishi katika mambo ya dini. Na kwa vyovyote vile, serikali si taasisi ya kidini, na suluhu juu ya imani na elimu ya dini si jukumu la Rais! Hivyo narudia. Viongozi wa dini nawaomba wasaidie sana kuwahi kumaliza migogoro itokeapo na kujenga umoja miongoni mwa waumini wa kila dini, na kila dhehebu la dini.

Nadhani pia wakati umefika wa dini zote kukubali kuwa na mfumo wa mazungumzo na mawasiliano baina yao, si kwa lengo la kupimana bali kwa lengo la kuelewana vizuri zaidi kama watu wa jamii moja na nchi moja. Mara nyingi kutoelewana chanzo chake ni kutoelewa. Mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii na kitaifa yatasaidia sana kuelewana na hivyo kuheshimiana.

Mwisho

Ndugu Wajumbe,

Nimejulishwa kuwa Mkutano Mkuu huu wa Taifa unayo kazi pia ya kuchagua viongozi wa Kitaifa wa Bakwata, na kuzingatia upya Katiba ya Bakwata. Nawatakieni mafanikio makubwa katika shughuli zote hizo. Napenda niwahakikishieni kuwa serikali yangu itafanya kila iwezalo kuweka mazingira mazuri, ya amani, usalama, haki na heshima ili kila raia aabudu, kuamini, kubadili na kutangaza dini yake kwa kuheshimu sheria za nchi na haki za raia wengine.

Tutazidi pia, kwa kushirikiana nanyi, kuchunguza kasoro zote zinazoleta hisia za ubaguzi au upendeleo kwa misingi ya dini ili kweli kila mtoto anayezaliwa katika nchi hii akue, asome na apate nafasi ya kutumikia taifa lake, na kupata riziki bila ubaguzi au upendeleo kwa misingi ya dini, kabila, eneo, rangi au jinsia.

Ndugu Wajumbe,

Kanuni moja ya hotuba nzuri ni kwa mzungumzaji kuhakikisha kwamba wasikilizaji wake hawaanzi kutazama saa zao za mkononi, au kuzitikisha masikioni ili kujiridhisha kwamba hazikusimama! Mmekuwa waungwana sana, lakini nisiwe mchoyo wa shukrani!! Namalizia basi kwa kuwaomba Watanzania wenzangu wote tuimarishe yale yanayotuunganisha kama taifa, na tuimarishe umoja, uzalendo na utaifa wetu, na kuyapuuza yale yanayotugawa na kudhoofisha taifa letu. Zaidi sana tujitahidi kuongeza nafasi za elimu kwa watoto wetu ili tuwaandae vizuri kwa uongozi wa taifa lao.

Nawashukuruni kwa kunisikiliza.
 
Sasa kuabudu kunahusiana vipi na kuchoma kitabu? Aliwazuia wengine kuabudu? Si chake kaamua kuchoma pengine atanunua kingine au kahama dini hataki kumbukumbu yoyote mlitaka afanye nini?

Vijana kama wewe ni hasara kwa Nchi.
Uko timamu kweli?Si hayo angefanya chumbani kwake?
Haya,nakupa mtumishi aliyelewa na kuchana Koran!Alifutwa kazi,nenda ukawe wakili wake mahakamani ili arejeshwe kazini!
 
Hapo balaa lingekua mzungu kachoma kuru1 lakini kwakua ni mvaa kobasi mwenzao hawalii sana
 
Uko timamu kweli?Si hayo angefanya chumbani kwake?
Haya,nakupa mtumishi aliyelewa na kuchana Koran!Alifutwa kazi,nenda ukawe wakili wake mahakamani ili arejeshwe kazini!

Post yako ya juu sijasoma huo upuuzi nipoteze muda wangu bure.

Kazini kuna miiko na miongozo kama kaivunja kwanin asichukuliwe hatua?

Huoni tofauti na mtu kuvunja sheria za nchi? Si wangemshtaki?

We jamaa kweli hamnazo hapa nimeconclude hakuna kitu kabisa.
 
Katoka iraq halafu achome hicho kitabu? Mbona iraq ni nchi ya waamini hicho kitabu?
Kwa taarifa yako tu ni kuwa Iraq, Syria, Lebanon wakristo wapo pia. Unamkumbuka the late Tariq Aziz aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq? Alikuwa mkristo.

Ila siyo lazima kwamba yule aliyechoma awe mkristo, hata muislamu anaweza kuchoma kama ameamua kuingia dini nyingine.
 
Post yako ya juu sijasoma huo upuuzi nipoteze muda wangu bure.

Kazini kuna miiko na miongozo kama kaivunja kwanin asichukuliwe hatua?

Huoni tofauti na mtu kuvunja sheria za nchi? Si wangemshtaki?

We jamaa kweli hamnazo hapa nimeconclude hakuna kitu kabisa.
Wewe ndio hamnazo kabisa!Unajua sheria za utumishi wa umma?Huyo alikuwa mwajiriwq wa serikali!
Unajua katiba ndio sheria mama?Yaani kwamba hakuna sheria yoyote inayoweza kutungwa kukiuka Katiba!
So hata sheria/kanuni zinazowekwa lazima zisikiuke katiba!Hata sheria na kanuni za utumishi wa umma hazipaswi kukiuka katiba!Huyo alitimuliwa kwa kukiuka sheria/kanuna za utumishi wa umma!
Wewe unakaza fuvu
Haya nakupa clip ya Magufuli akimfuta kazi huyo mtumishi kwa barua!!!!
Wewe ndio unajiona una akili!
 
Wewe ndio hamnazo kabisa!Unajua sheria za utumishi wa umma?Huyo alikuwa mwajiriwq wa serikali!
Unajua katiba ndio sheria mama?Yaani kwamba hakuna sheria yoyote inayoweza kutungwa kukiuka Katiba!
So hata sheria/kanuni zinazowekwa lazima zisikiuke katiba!Hata sheria na kanuni za utumishi wa umma hazipaswi kukiuka katiba!Huyo alitimuliwa kwa kukiuka sheria/kanuna za utumishi wa umma!
Wewe unakaza fuvu
Haya nakupa clip ya Magufuli akimfuta kazi huyo mtumishi kwa barua!!!!
Wewe ndio unajiona una akili!

Bro naona unabwabwaja sana. Lets make long story short. Kosa la kuchoma kitabu cha dini lipo? Na hukumu yake ni nini? Naomba jibu.
 
Back
Top Bottom