Magwangala
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 2,836
- 2,138
Bila shaka huyo atakuwa ni Askofu Method KigumuKuna kanisa fulani, msaidizi wa askofu alisikika zaidi kuliko askofu. Hata wageni wakija wanamuulizia naibu askofu. Huyo naibu ilibidi ahamishwe chapchap. Hutakiwi usikike zaidi ya mkuu wako wa kazi.
Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Habari ya uhakika hiyo, nami nimeipata kwa chanzo cha ndani kabisa.Source mfanyakazi wa online media[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli hii nchi mbumbumbu was amejaa
Hebu tuisome kwa makini, tuanzie alipomalizia "D. G. Chongolo"? Huyu D. G. Chongolo ni nani ndani ya CCM? Najua CCM yumo Daniel, je, ni huyu D. G. Chongolo? Mimi ninaona siye yeye na kama angekuwa yeye angeliandika jina lake kamili na si kwa kifupi ukizingatia anamuandikia bosi wake yaani mwenyekiti wa chama.
Taarifa zilizotufikia usiku huu ni kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amejiuzulu nafasi yake hiyo.
Vyanzo vyetu vilivyo karibu na CCM vimethibitisha kuwa tayari Chongolo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama (NEC), ambavyo vinafanya vikao vyake vya kawaida jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023, huenda vikampitisha Katibu Mkuu mpya wa CCM ambaye atachukua nafasi ya Chongolo.
Sababu za kujizulu kwa Chongolo tutawaletea baadae.
Sishangai, chongolo kwa Ukatibu mkuu alikuwa chongo kweli. Alipwaya sana.
akiondolewa kama sii kwa yeye kuamua ccm kwishney.Unajua fika kuwa wakati Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam na Chongolo ni DC wa Kibindoni walikuwa hawapatani kwani kuna Mmoja kati yao ana Akili na Mmoja ni Mpumbavu Kiasili halafu leo tena unaowaleta pamoja ndani ya Chama Tawala ( CCM ) huku kwa Makusudi, Mahaba na kupenda Kudanganya na Wanafiki unampa Jeuri na Upendo wa wazi wazi Mtu ambaye ndani ya Katiba ya Chama ni mdogo kuliko Katibu Mkuu na unataka Katibu Mkuu amnyenyekee yule anayetakiwa Kumyenyekea Yeye.
Kwa hapa / kwa hili kama ni la kweli ninampongeza sana Bwana Chongolo kwani alichofanyiwa ilikuwa ni Dharau isiyovumilika.
Na najua Chongolo ana Watu wake ndani ya System ya Nchi na Chama ( CCM ) ambao wamemdokeza mapema kuwa Kikao cha leo ( cha CCM ) anaenda Kung'olewa hivyo nae kawa very smart kwa kuwawahi kwa kupeleka Barua ya Kujiuzuru hivyo hatongolewa tena hii leo ( Jumanne ) Kikaoni CCM kwa Mipasho ya Paje Kizimkazi Zanzibar.
Chama kinaungua wewe unasema CCM juu. Ni bahati mbaya chama kimejaa makada wanafiki, waongo na wanaopenda kujipendekeza. Kwa sasa CCM inaendeshwa kwa majungu, upendeleo na inatafunwa na udini pamoja na ukanda.Umekuja umesoma na umetia lako.
CCM juu, juu, juu zaidi.
Nimecheka sana hapo mwishoEti barua zote zipelekwe kwa Katibu mkuu😂😂
Pumbavu nyie
Wala sikatai ila source uliyoweka ndio ya kibwegeHabari ya uhakika hiyo, nami nimeipata kwa chanzo cha ndani kabisa.
Kazi ipo...Sishangai, chongolo kwa Ukatibu mkuu alikuwa chongo kweli. Alipwaya sana.
Ccm hawana huo utaratibu atafia hapo kama nzi kwenye kidonda
Taarifa zilizotufikia usiku huu ni kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amejiuzulu nafasi yake hiyo.
Vyanzo vyetu vilivyo karibu na CCM vimethibitisha kuwa tayari Chongolo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama (NEC), ambavyo vinafanya vikao vyake vya kawaida jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2023, huenda vikampitisha Katibu Mkuu mpya wa CCM ambaye atachukua nafasi ya Chongolo.
Sababu za kujizulu kwa Chongolo tutawaletea baadae.
Leo muhusika alikua mwenyekiti wa kikao Cha Sekretariet ya Chama ( kikao Cha maandalizi ya vikao vya Cc na Nec)H
Hebu tuisome kwa makini, tuanzie alipomalizia "D. G. Chongolo"? Huyu D. G. Chongolo ni nani ndani ya CCM? Najua CCM yumo Daniel, je, ni huyu D. G. Chongolo? Mimi ninaona siye yeye na kama angekuwa yeye angeliandika jina lake kamili na si kwa kifupi ukizingatia anamuandikia bosi wake yaani mwenyekiti wa chama.
Ninaamini bado yumo.
Mimi sina cha kujiuzulu maana sina kazi zaidi ya jembe na kilimo ambacho siwezi nikajiuzulu,maana jembe ndio linaloonilisha.Bado ya Lucas mwashambwa naye ajiuzuru tu.
Nadhani members wajifunze kutambua taratibu za uandishi wa barua za kiofisi.Leo muhusika alikua mwenyekiti wa kikao Cha Sekretariet ya Chama ( kikao Cha maandalizi ya vikao vya Cc na Nec)
Kuna barua feki inatembezwa au kusambazwa mitandoni eti chongolo Kajiuzulu.
Chongolo hajajiuzulu yupo ofisini anachapa kazi. Hii barua ni fake..angalia hata paragraph ya Mwisho. Mmegushi hata saini yakeView attachment 2827408