Pre GE2025 Katibu Mkuu wa CHADEMA kutangazwa mchana huu. Nani kumrithi John Mnyika?

Pre GE2025 Katibu Mkuu wa CHADEMA kutangazwa mchana huu. Nani kumrithi John Mnyika?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba, Katibu Mkuu mpya wa Chadema atatangazwa mchana huu

Bado haijajulikana ni nani hasa, japo kuna Majina kadhaa yanatajwa.

Juhudi zangu za kulazimisha kuvujishiwa jina kwa manufaa ya JF zinaendelea, Nzi wangu akiweza tu kunusa basi haraka sana kwa chap nalileta jina hapa

Usiondoke JF
Yule wa kulala makanisani kipindi cha maandamano hatakiwi tena!
 
Yule wa kulala makanisani kipindi cha maandamano hatakiwi tena!
Maombi ni muhimu ili maridhiano yatekelezeke. CHADEMA huwa tunasema tunaanza na Mungu na kumaliza na Mungu.

Pale makao Makuu Mnyika aliweka chumba cha ibada. Na kukawa na Biblia na Quran Kwa ajili ya kusoma kama mtu akitaka kutabaruku!!

Kwa masuala ya Imani na Ibada Mnyika ni kilongola. Rafiki yake kwenye mambo hayo ya Ibada alikuwa Mzee Ali Kibao(mwenyezimungu amrehemu).
 
Bado sijapewa jina, ila ningependa awe mtu mnoko hivi, Ili tuheshimiane, kuna haja ya kukomesha utekaji kwa vitendo
kama ndiyo hivi basi ateuliwe godbless Lema kuwa katibu mkuu wa chadema, ikiwezekana tundu lisu amuombe john mnyika akubali kuwa naibu katibu mkuu wa chadema kwa upande wa Tanganyika. tafadhali penyeza haya maoni yetu ili yamfikie tundu lisu huko ndani wakati wanapoendelea na mchakato wa uteuzi wa viongozi wengine wa chama hicho
 
Screenshot_20250122-143622.png
 
Godbless Lema ambaye ni Mbunge mustaafu wa Jimbo la Arusha (CHADEMA) na Mwenyekiti mustaafu pia wa Kanda ya Kaskazini, anatarajiwa kupendekezwa awe SG mpya wa Chadema.

Wakati huo huo, aliyekuwa Mkuu wa shughuli za Uchaguzi zilizo muhusu Mwenyekiti wa sasa wa Chadema Taifa bwana Lissu afahamikaye kwa jina la Lyenda, anatarajiwa kupendekezwa awe Naibu SG wa Chadema Bara.

Majina ya wawili hao yanatarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema linalotarajiwa kuanza hivi punde.
 
Katibu Mkuu anaweza kuwa Amani Golugwa,kwa sasa ni Katibu wa Kanda ya Kaskazini na Meneja Kampeni wa TAL kwenye uchaguzi mkuu 2020,ni mtu makini sana na mtulivu pia
 
Back
Top Bottom