Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 783
- 2,057
Useme tu ukweli kwamba Ile nguvu aliyokuwa anakupa mwendazake ufanye ulichokuwa unafanya kwa sasa haipo na uwezi kuipata Tena, umeteuliwa kafanye kazi inayokuhusu izo habari za kulipa kisasi ata Kama unataka kulipa itakuwa ngumu kwako kwakuwa huu ni utawala tofauti na ule uliokufanya uwe na kiburi Cha Kila aina, na nafikiri Kama utakuwa na akili sawasawa utakuwa umejifunza jambo wakati wote ambao ulikuwa benchi, sidhani Kama unaweza kurudia ujinga ule na waliokuteua nafikiri watakuwa wamekupa semina elekezi na maonyo ya nini unatakiwa ufanye na miiko ya uongozi wa cheo ulichopewa!Katika mapokezi ya Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Ndugu Makonda amesema;
"Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupita katika mitandao kusoma maoni ya baadhi ya watu, wengi wanahamaki na wengi wanabashasha, na katika wengi wanaohamaki wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi.
"Wanawaza makonda ataenda kufanya nini, nimeona na wengina wengine wanaanza kuwataja watu wengine kwamba utaona sasa usiyemtaka kaja, wengine wanasema tumejifunza nini katika jambo lamakonda.... Naomba niseme mbele ya hadhara hii, mgeni rasmi na mbele ya watanzania wapenzi wa chama cha mapinduzi na wakareketwa na mbele za Mungu, mimi sina kisasi na mtoto yoyote.
"Na asiwepo mtu akafirikiri lengo langu ni kumkandamiza, asiwepo mtu yoyote akafikiri wakati nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikri wamenitenda mabaya, la hasha... naamini Mungu aliwatumia akiniandaa kufanya kazi kubwa zaidi..."
Tunajua lazima Kuna nguvu kubwa imetumika kukupigia debe kurudishwa chamani Sasa kafanye majukumu yako usitoke njia kuu ukawa Kama rafiki yako sabaya!