Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Makonda amesema Watesi wake wamejenga na Kumfanya awe karibu na Mungu wa mbinguni zaidi, na hatimaye yuko Jirani na Patakatifu pa Patakatifu

Source: Channel ten
Kwahiyo ni same code na Kawe
 
Sijafanikiwa kufika Lumumba kutokana na kukwama kwenye foleni ya kwenda huko Hapa Magomeni

Kwahiyo nipo Hapa Sea Boys ghorofani nashiriki mapokezi kupitia Channel ten tv

Cha ajabu nasikia shangwe za Magufuli, Magufuli Ndio najiuliza anayepokelewa ni Makonda sasa Magufuli inakuwaje tena?

Dogo ametisha sana, akabidhiwe tu Chama hakuna namna [emoji23][emoji23][emoji23][emoji91]
Kama usemayo ni kweli utakataa kuwa Makonda ameigawa CCM?
 
Tukio hili la kusikitisha limetokea mbele ya hadhara , ambako Majeruhi huyo amekimbizwa MOI

Screenshot_2023-10-26-12-52-04-1.png
 
Mimi kwangu Makonda ni mwanasiasa bora sana angalau ameacha legacy ya kupunguza kama sio kukomesha biashara ya unga enzi zake akiwa mkuu wa mkoa wa Dar. Kuhusu uzalendo wake hapo sina uwakika siwezi lisemea.
 
Mtu apate ajari wewe ulete habari kishabiki na uitafsiri kuwa ni laana kwasababu tu jambo lililokuwa linafanyika ni mlengo tofauti nawewe kisiasa!.
Ifike hatua tuwe na utu ndani yetu sio mpaka tufundishane,akili tumepewa ya utafakari na sio kutumia kama makapi ya kudharirisha wengine.
 
Katika mapokezi yake Makonda ametuma salamu kwa mawaziri, wakuu wa miko na watendaji wote watakaokuwa hawafanyi kazi zao kikamilifu chama hakitasita kuchukua hatua.

Akisema hayupo tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi na wanaomsaidia Mwenyekiti kiwe na viongozi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, na kwamba kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe.

Akaongeza kuwa hajahifadhiwa miaka 3 na miezi 3 kusema uongo.
 
Back
Top Bottom