Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Makonda amesema wakati wote alipokuwa kwenye Likizo ya miaka 3 na miezi 3 Viongozi wa Dini, Wajane na Wanyonge walikuwa Wakiomba na Kufunga kwa ajili yake, anawashukuru sana

Makonda ameahidi Kutolipa Kisasi kwa mtu yoyote mbele ya Mungu wa mbinguni

Makonda amesema Watesi wake wamemjenga na Kumfanya awe karibu na Mungu wa mbinguni zaidi, na hatimaye yuko Jirani na Patakatifu pa Patakatifu

Source: Channel ten
Sijawahi kuona mtu anaemtaja mungu mara nyingi kama shetani.
 
Mtu apate ajari wewe ulete habari kishabiki na uitafsiri kuwa ni laana kwasababu tu jambo lililokuwa linafanyika ni mlengo tofauti nawewe kisiasa!.
Ifike hatua tuwe na utu ndani yetu sio mpaka tufundishane,akili tumepewa ya utafakari na sio kutumia kama makapi ya kudharirisha wengine.
Laana
 
Katika mapokezi ya Katibu Mwenezi, Makonda amesema Tanzania haina chama cha upinzani bali ina watoa taarifa waliojikusanya katika jina la vyama.

Akisema ukimwomna Lissu anaongea si chama kinaongea ni mtu tu anatoa taarifa na wakati mwingine inawezekana taarifa anayoitoa inaweza kuwa imetoka kwenye chanzo ambacho si cha kweli au cha uhakika, lakini kwakuwa ni mtoa taarifa kazi ya chama cha mapinduzi ni kusikiliza taarifa zao, badala ya kushughulika na mtoa taarifa tunashughulika na aliyesababisha hizo taarifa kutoka.

Mfano akisimama kiongozi yoyote wa chama cha kutoa taarifa akatoa taarifa ya kwamba umeme umekatika, jukumu letu kama chama ni kushughulika na anayekata umeme kwa wananchi.
 
Hivi Makonda ana utimamu gani wa akili au kwa usmart upi mpaka ionekane anafaa sana?

Kweli CCM imechoka.
Tatizo nyota yako kaka, watanzania hawataki utimamu hawataki ujuaji wanataka vitu vya ujinga ujinga badili mtazamo wako
 
Team!
Hii iko very serious na to be frank ni kwamba ili twende vizuri kisiasa lzm tuwe kundi la watu wanaojiheshimu na kuheshimu wengine.

Nasema hivi kwa kuwa wafuasi kibao wa CDM, CUF, NCCR, NLD, Umoja, ACT nk wana kautamaduni walikojenga vichwani ka kutukana, kumkashifu na kudhihaki viongozi wa CCM. Siku zote hudhani kwamba bila kutukana basi chakula hakitapita kooni.

SASA:
Atakayemtukana CDE Paul Makonda kwa namna yoyote ile atakuwa ameitukana CCM na kwa hali hiyo tutamuwajibisha nje na ndani. CDE Paul Makonda sawa na wewe anastahili kushika nafasi yoyote na sifa anazo za kutosha. CCM tumefurahi kwa kuwa ujio wake utainyima CDM usingizi.

Tusilaumiane kwa atayeshupaza shingo.

Ngaika Ndenda
Kakonko.

Punguza bangi za uzeeni.
 
Back
Top Bottom