Katika mapokezi ya Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Ndugu Makonda amesema;
"Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupita katika mitandao kusoma maoni ya baadhi ya watu, wengi wanahamaki na wengi wanabashasha, na katika wengi wanaohamaki wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi.
"Wanawaza makonda ataenda kufanya nini, nimeona na wengina wengine wanaanza kuwataja watu wengine kwamba utaona sasa usiyemtaka kaja, wengine wanasema tumejifunza nini katika jambo lamakonda.... Naomba niseme mbele ya hadhara hii, mgeni rasmi na mbele ya watanzania wapenzi wa chama cha mapinduzi na wakareketwa na mbele za Mungu, mimi sina kisasi na mtoto yoyote.
"Na asiwepo mtu akafirikiri lengo langu ni kumkandamiza, asiwepo mtu yoyote akafikiri wakati nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikri wamenitenda mabaya, la hasha... naamini Mungu aliwatumia akiniandaa kufanya kazi kubwa zaidi..."