Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Sasa unakuta m Swahili, kipato chair, hakifiki hata 2000 kwa siku, na yeye anaandsmana kumshangilia bashite!
Unaruhusu utumiwe na majizi, Yao yananeemeka, wewe unakufa njaa!
 
Sasa unakuta m Swahili, kipato chair, hakifiki hata 2000 kwa siku, na yeye anaandsmana kumshangilia bashite!
Unaruhusu utumiwe na majizi, Yao yananeemeka, wewe unakufa njaa!
Vipi na wake wanaotumika na vyama vya upinzani kuandamana kuna faida yoyote wanapata
 
ELIMU ni nyenzo muhimu sanaa Tanzania tumebarikiwa rasilimali watu ma million Kwa mamilion kulikua Kuna haja Gani ya kumrudisha Paul makonda (Daud Bashite) kwenye chama kama spoke man wa chama Cha mapinduzi....

Wapo wanao sema kua Paul makonda ni mshirikina wa kiwango Cha juu sanaa kiasi kwamba Huwa anatumiwa na viongozi wake kuwasaidia mambo mengi yaende inavyo takikana Mimi nilisikia yakisemwa ivyo......

Ni lini kama taifa tutaacha siasa za kujimwambafy na kujipa mabavu nimemsikia Paul akijigamba kua Tanzania hakuna vyama vya upinzani bali ni vikundi vya watu wenye maslah binafsi.....

Kama taifa tunaenda mbele au tunarudi nyuma 🤨🤨🤨🤨
 
Umesahau kuweka namba ya simu ili muonane uso kwa uso.
 
Wanalialia tu
Watanzania wengi tuna changamoto kubwa ya kufikiri sana.
Makonda hana tofauti na Musiba au Sabaya. Nguvu ulizoziona kwao nyakati zile Hazina tofauti na kifaa cha umeme kinachoitwa MOTA, hata iwe kubwa kiasi gani utendaji wake unategemea na umeme kutoka kwenye chanzo/ transformer. Ambayo nayo hupokea nguvu kutoka chanzo kingine I.e.generator. Makonda alipata umaarufu tena wa aibu siku alipomshambulia Mzee Warioba kwenye kongamano la katiba Ubungo, na viongozi wasio na haya walikiona kitendo hicho ni cha kishujaa wakamzawadia ukuu wa Wilaya.
Huko kwenye ukuu wa Wilaya hakuwa na jipya zaidi ya kelele za hovyo hovyo tu, kwa sababu anajua kucheza na akili za viongozi wasiojiamini akalamba ukuu wa mkoa awamu ya Tano.
Ni mkuu wa mkoa pekee aliyepewa ulinzi kuliko wote, na huyo huyo aliyempa ulinzi, baadaye akamuacha kwenye mataa alipojitosa kwenye uchaguzi wa ubunge akiamini yeye ni maarufu sana. Wakristo wanaosoma biblia,Iko hadithi ya punda aliyembeba Yesu.Yerusalemu kuelekea hekaluni, na Yesu alishangiliwa sana na bahati mbaya inawezekana punda alidhani anashangiliwa yeye na bahati mbaya wako watanzania akili zao ni kama za huyo punda, kwamba Makonda alifokea marpc.. kwenye mikutano walifikiri ana nguvu hizo, anasema siye wabara tusije Dar bila kuoga wanajua mwamba amesema, ukweli mchungu sana ni huzuni sana kuamini hao watu wapo mpaka awamu hii na wengine wamo humu. Kweli ndio maana ni afadhali ya mjinga akielimika hataitwa mjinga tena,lakini tunao wapumbavu ambao hata ufanye nini hawatabadilika labda aliyewaketa duniani aingilie kati.
Kwamba tunasahau huyo huyo aliyempandisha mabega ndiye aliyemshusha mpaka anaondoka duniani, Makonda alikuwa mtaani.
Awamu ya tano wengi walikuwa kama MOTA kubwa, Ally Hapi, huyu Rc wa dar, hata yule mbunge wa Arusha sasa hivi. Nguvu yao ilitokea ikulu na ndio sababu Chalamila wa Mbeya siyo Chalamila wa Mwanza au Kagera. Ni Makonda huyu huyu aliyesavabisha Nape apoteze uwaziri, ni Makonda huyu huyu aliyemwita Ridhiwani Kikwete ajieleze kuhusu biashara ya dawa za kulevya.
Sasa mnaosema huyu ni kiboko cha Chadema, hampaswi kulaumiwa, maana unafiki ni moja ya sifa kubwa ya ccm.
Hivi huyu ataondoa shida ya umeme! Ajira!kuungua kwa masoko!! Haswa Kariakoo!!
Makonda wa sasa hana tofauti na MOTA ya 1.5Kw. labda mama huyu amrudishie like genge lake la gizani.
 
Makonda Mungu akupe hekima usijaribu kulipa kisasi!! Mazingira ya kazi yako yatakuwa magumu sana!! Huku Gwajima, huku Nape, huku Kinana!! Umewekwa hapo kuimarisha timu mama kuelekea 2025!! Hilo usilisahau!! Vinginevyo mtumbuo utakuhusu!!
 
"Niseme tu kuanzia leo Oktoba 26, 2023, Taifa hili halina chama cha upinzani bali lina vyama vya watoa taarifa, na sisi kama chama tawala tutafanyia kazi taarifa zao kwa sababu ni chachu ya ujenzi si tu wa demokrasia bali wa maendeleo katika Taifa letu."

 
🔴#Live: MAPOKEZI-MAKONDA AANDIKA HISTORIA DAR ATUPA KOMBORA ZITO KWA FREEMAN MBOWE

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda a.k. a “BABA KEAGAN” amesema tangu ateuliwe kuna Watu wamehamaki wengi wao wakiwaza kuwa Makonda ataenda kulipa kisasi huku wengine wakiwataja baadhi ya Watu na kuwaambia ‘Utaona sasa usiyemtaka kaja’, ambapo Makonda amesema hajaja kulipa kisasi kwa yeyote.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam baada ya kupokelewa na Viongozi na Wanachama wa CCM, Makonda amesema “Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupitapita kwenye mitandao, nimesoma maoni ya baadhi ya Watu, wengi wanahamaki na wengi wana bashasha lakini wanaohamaki wengi wao wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi, nimeona na wengine wanaanza kuwataja Watu wengine kwamba ‘Utaona sasa usiyemtaka kaja’, naomba niseme Mimi sina kisasi kwa Mtu yoyote, na asiwepo Mtu yoyote yule akafikiri lengo langu ni kumkandamiza, au nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikiri wamenitenda mabaya”

“Mnaohisi kuna jambo halikuwa sawa Mimi naelewa Mungu aliwatumia kunisaidia kumjua Mungu zaidi, naamini Mungu aliwatumia ili kuniandaa kwa kazi kubwa zaidi msiwe na hofu, naomba ushirikiano na umoja wenu na wala Dkt. Samia hajaniteua kuja kuhangaika na mambo ya Makonda bali uenezi wa CCM na wala Dkt. Samia na Kamati Kuu haikukaa kwenye kikao kumtafuta Mtu wa kwenda kulipa kisasi, walimtafuta Mtu atakayeongeza nguvu katika kujenga imani ya Watanzania kwenye CCM”

Katika moja kati ya mazungumzo yake Bwana Makonda amesema ameongea na Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA apewe kibali cha kuruka angani na Helkopter kuendelea na mikutano ya hadhara na kama ameishiwa mafuta amepewa kibali rasmi cha kujaza mafuta kwa ajili ya helkopter anayotumia.

“Naomba kuchukua nafasi hii kuiagiza Serikali inayohusikamna Mamlaka ya Vibali, kama ni watu wa Anga nawaelekeza mpeni Mbowe kibali aruke na Helkopter na kama hana mafuta nimeongea na Dkt.Samia, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amesema atamchangia, Akiruka angani tutamfata, akienda nchi kavu tutamfata, akiingia kwenye boat tutamfata atapigwa kila kona”

Mbali na hayo Mnec huyo ameingia katika ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam (Lumumba)na Pikipiki za kubeba abiria maarufu kama “Bodaboda”.

Mamia ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wamejitokeza kwa wingikumlaki Makonda licha ya eneo la Ofisi za Ccm kuwa dogo kutokana na watu kufurika.

Mwisho Paul Makonda amesema ameongea na Rais Samia kumtembelea Rais wa Zanzibar Dkt.Hissein Ali Mwinyi pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wakamwambie wanahitaji Mwenezi wa aina gani kwa sababu hajawahi kuwa Mwenezi mahali popote.
Credit by Mimi Mwenyewe.
 
Failing State! Badala ya kupambana na Ripoti ya CAG na mchwa walioiba trilions mnapambana na Mbowe aliyekulia ushuani wakai mimi na wewe tukiwa tunalala nyumba moja na mifugo huko kolomije?
 
Umesahau kuweka namba ya simu ili muonane uso kwa uso.

Eeeeh
Siku moja yaja.. kuna siku nilikuwa nimekuja Dar kutoka huku mkoani.. nikaenda kukutana na friends restaurant moja Oysterbay.. nafika tu wananiambia nimepishana nae.. wakanionyesha alipokuwa amekaa anaongea na watu fulani nao walikuwa wanaondoka.

Ningemfata kwa kweli.. kumsalimia..

Labda atanitumia inbox humu niende ofisini kumsalimia 😅😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…