Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM, Paul Makonda atambulishwa rasmi CCM, atinga kwa bodaboda

Sisi wananchi tumefurahi sana siku ya leo. Karibu sana Mh Makonda kwenye nafasi yako.
 
Mbona bado ana unaa, au anapewa nguvu na waliomuinua na kumpandisha chati kuwa mkuu wa wilaya. Karudi chatini na mkwara mzito kwa wakuu wa mikoa na mawaziri. Je ataweza kuwasagia kunguni kinomanoma kama wakati ule wa mukulu aliyemteua kuwa mkuu wa mkoa wa dar? Au ni mikwara tu ili aonekane bado ana ule ubabe wake wa zama za utawala ule. Eti anasema ukiwa mcha mungu naye atakuwa mcha mungu, ukiwa rafu rafu naye atakuwa rafu rafu, atakuwa muenezi kutokana mtu anamuundaje ! Kwa hiyo akiundwa shetani naye anakuwa shetani, akiundwa dikteta naye anakuwa dikteta. Aangalie asije akawa dikteta uchwarwa na wanachama chake wakamuona imla mkorofi
 
Laiti ungejua adui mkubwa wa Makonda ni wapambe wa mama na wala sio wapinzani usingesema hayo. Kwa kuteuliwa Makonda;
Hivi Kinana ana furaha?
Hivi JK ana furaha?
Hivi Nape ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi January ana furaha?
Hivi Makamba senior ana furaha?
Hivi Philip Mpango ana furaha?
Hivi Majaliwa ana furaha?
Hivi Ridhwani ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi Abdallah Bulembo ana furaha?
Hivi Bashe ana furaha?
Hivi Sofia Mjema ana furaha?
Hivi mzee Warioba amefurahi?
Hivi Askofu Gwajima amefurahi?

Paskali anafuraha.
 
Laiti ungejua adui mkubwa wa Makonda ni wapambe wa mama na wala sio wapinzani usingesema hayo. Kwa kuteuliwa Makonda;
Hivi Kinana ana furaha?
Hivi JK ana furaha?
Hivi Nape ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi January ana furaha?
Hivi Makamba senior ana furaha?
Hivi Philip Mpango ana furaha?
Hivi Majaliwa ana furaha?
Hivi Ridhwani ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi Abdallah Bulembo ana furaha?
Hivi Bashe ana furaha?
Hivi Sofia Mjema ana furaha?
Hivi mzee Warioba amefurahi?
Hivi Askofu Gwajima amefurahi?
Sophia mjema leo body language imeonyesha hajafurahi kabisa
 
Mh. Makonda Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi, kiongozi mwenye nyota ya pekee inayong'ara nchini anatarajiwa kupokelewa Leo kwenye ofisi ya CCM, Lumumba, Dar Es Salaam.

Siku ya Leo tarehe 26 Oktoba 2023

Kila la kheri Mheshimiwa, kutoka kwa mwana JF Mimi. Natumaini siku moja nitakutana nawe uso kwa uso kwa mara ya kwanza.

Makonda Oyeeee

Kazi iendelee...
Unatumai ukutane nae ili umpe kitumbua chako? Aah be ok!
 
sure upinzani umekua ukifanya siasa harakati muda mrefu softly, sasa huyo kijana ana mtindo wa siasa harakati pia intakua ni majotrooo na motrooo sana
Siasa harakati ni zipi?
 
Nachojiuliza je makonda alichaguliwa na Samia peke yake au na kikao cha kamati kuuu nahis kwenye hiko kamati wapo viongoz woteee vigogo wa ccm ila nashangaaa watu wanamsema samia kwa nn kamchagua makondo hapana tuseme ccm kwa n wamemchagua makonda
Kwa upande wangu mie sion ubaya kwa makonda ila nachonba afanye kazi kwa misingi na mipaka ya seheme yake ya kazi atakwenda mbele na atakuwa sawa tu
 
Laiti ungejua adui mkubwa wa Makonda ni wapambe wa mama na wala sio wapinzani usingesema hayo. Kwa kuteuliwa Makonda;
Hivi Kinana ana furaha?
Hivi JK ana furaha?
Hivi Nape ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi January ana furaha?
Hivi Makamba senior ana furaha?
Hivi Philip Mpango ana furaha?
Hivi Majaliwa ana furaha?
Hivi Ridhwani ana furaha?
Hivi Chongole ana furaha?
Hivi Abdallah Bulembo ana furaha?
Hivi Bashe ana furaha?
Hivi Sofia Mjema ana furaha?
Hivi mzee Warioba amefurahi?
Hivi Askofu Gwajima amefurahi?
Mkuuu kwan hao wote hapo si kamati kuuu si ndio walipitisha kuchaguliwa kwake? Nahis wote ni wahusika kma nao walileta unafiki kwenye kuchagua basi imekula kwako wamekwenda na maji ila kasema hana kisasi
Ila mie napenda BASHE NDIO ALIPWE KISASI MAAANA MPUUZ SANA
 
Huyo nyamitako tunamuona boya tu.Nilidhani kipaumbele ni kuondoa kero kwa watanzania kama vile mgao wa umeme nk. lakini kama ni kuonyesha ubabe kwa Chadema basi ajihesabu ameshashindwa kabla ya kuanza. Kama alishindwa Magu aliyekuwa CIC atakuwa huyo MC wa chama chakavu.
TULIA UBWEDE
 
Watu wanakuza sana mambo. Makonda alikuwa mbabe sana kwa sababu ya aina ya uongozi wa juu uliokuwepo kipindi kile. Alipata "back up" isiyo ya kawaida kutoka kwa aliyekuwa anamkingia kifua. Tusitake kujisahaulisha kuwa hata huyo aliyekuwa anampa "back up " alifika mahali akamtosa Makonda akabaki peke yake kwani hata marafiki zake wa karibu wengine walimkana hadharani wengine walimkimbia na kumkashifu.

Kwa sasa huyo Makonda hawezi kurudia tena ule ubabe wake wa hovyo kwani amejifunza mengi sana kupitia yeye mwenyewe na rafiki yake Sabaya. Kwani sasa anajua kuwa atakayekutuma leo ukafanye mambo ya hovyo kesho akiwa hayupo wanachi watakusulubu. Fikiria tu mfanyabiashara kama GSM alianza kudai nyumba yake hadharani vipi wale waliodai mali zao gizani? Kwa hakika hawezi kurudia makosa ya ovyo aliyofanya japo yale aliyotenda nyuma hayafutiki. Na yeye mwenyewe anajua wazi jinai haifutiki

Mimi nafikiri suala kubwa la kujadili kuhusu Makonda sio ubabe wake kwani kwa mfumo na aina ya uongozi ulipo sasa haumpi nafasi ya kufanya aliyoyafanya wakati zile. Kwa sasa suala la kubwa la kujiuliza ni je uteuzi wa Makonda ni asset au liability kwa CCM? Je Makonda kashaondolewa kashfa yake na wamarekani?

Ni mtizamo tu.
Point mkuuu
 
Wapinzani wake ni mawaziri na viongozi wa serikali, huko kwingine ni kukimbizana na upepo tu, na ajikite huko ili wananchi wapate huduma bora.Kuna miradi kibao aiendi na huku pesa imeishatolewa, makonda anatakiwa kusaidia hapo na sio kukimbiza na upepo wa chadema na act
 
Back
Top Bottom