TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

Dereva wa Vieti akaona isiwe kesi kasukumizia kwa katibu

Alale panapostahili.
 
Alikua na v8 akitokea Arusha kuelekea Dodoma.Walipofika mdori mkoa wa Manyara wakagongana na Bus.Ndani walikuwemo na wanawake 3 ambao ni majeruhi pamoja na dereva.Pole zao wafiwa.
 
Maisha hayana maana kabisa na tunahangaika bure tu kutafuta hela na maisha mazuri.
Maisha yana maana sana. Muhimu ni kutambua kwamba duniani tupo kwa muda mfupi, baada ya muda tutaondoka kwenda kwenye makazi ya milele.

Utaondoka kwa ajali, ukimwi au hata korona haijalishi.
 
Alikua na v8 akitokea Arusha kuelekea Dodoma.Walipofika mdori mkoa wa Manyara wakagongana na Bus.Ndani walikuwemo na wanawake 3 ambao ni majeruhi pamoja na dereva.Pole zao wafiwa.
Karatu hoyeee
 
Akili matope hizi! Kwahiyo hapo Lisu atarudi kuwa rais?

Nchi hii ina miaka 60 na wananchi wanaokaribia 60m, katika idadi hiyo na miaka hiyo, ni watu watano tu wamefanikiwa kuwa marais wa nchi hii. Hivyo hata Tundu Lisu asipokuwa rais sio tatizo kwani nafasi hiyo ni kama bahati nasibu. Hata hivyo sijajua hoja yako ilikuwa ni nini kwenye post hii.
 
Viongozi na watumishi wa serikali ni wahanga wakubwa wa vifo/ulemavu uletwao na ajali...

Sijui chanzo ni nini? Mwendokasi au juju
Mwendokasi Mkuu.
Wanajiamini sana Barabarani nadhani ni Kwa vile Askari Wa Usalama Barabarani hawana sauti kwao..

Anyway, R.I.P Katibu Tawala.
 
Anaweza sifiwa na wengi ila binafsi nilimfahamu kama mtu wa manyanyaso, kukosa utu, majungu (na hivi alikuwa ofisi moja na mkewe), roho mbaya, kukandamiza surbodinates asio wapenda n.k
Mhanga pia.
hili umemsingizia
 
Oooh my God, vile nimemfaham huyu mtu hakika duniani tupo njiani, sina zaidi ila Mungu awape faraja ndugu, jamaa na wanaArusha wote kwa kumpoteza mtendaji huyu ofisi ya RC.
 
Apumzike kwa Amani. Ila madereva wa serikali na hizo overtake zenu hapana. Sasa ukichanganya na overtake za mabasi inakuwa si hali. Hata kama mnaendesha magari ya serikali (au hata mabasi) jueni ajali haichagui uimara wa gari au status ya gari-nashangaa hata hamuofii maisha yenu wenyewe mnovyo overtake! Chonde chonde fuateni sheria kama sisi raia na muache mchezo wa kuwasha mataa yenu na kupita kwenye 50 kph na hizo 120+kph. Ajali inaweza kumpata mtu yeyote ila kuna anayejiweka katika nafasi hatarishi zaidi kupata ajali kwa kuvunja sheria za barabarani kwa ubabe tu. Sasa baba wa watu kapoteza maisha hivi hivi, inauma. Poleni familia ndugu jamaa na marafiki.

Wamekusikia mkuu ila msafara wa slow ni wa harusi na msiba tu hii ya jamhuri ni kuwahi kazi. Mengineyo ni matokeo tu
 
Salaam Wakuu,

Habari Mbaya ni kwamba Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Richard Kwitega amefariki Dunia kutokana na ajali.
View attachment 1693548

Richard Kwitega kafariki alasiri ya leo kwa ajali ya gari katika kituo cha afya cha Magugu. Alikuwa anaenda Dodoma Kikazi, alipofika maeneo ya Mdori Manyara gari lake iligongana na Basi la Makala uso kwa uso, basi lilikuwa linalotoka Babati.

Baada ya ajali akakimbizwa kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi.

Ilipofika saa tisa na dakika 50 akafariki Dunia. Mipango inafanyika ya kuurudisha mwili Arusha.

Apumzike kwa amani

View attachment 1693569
View attachment 1693583View attachment 1693584View attachment 1693585
Mbona sielewi hapo gari zote zimeumia upande wa kushoto, hapo walikuwa wanapishana wrong side au?
Basi limeimia kushoto mbele, na cruiser nayo ni kushoto mbele, je hapo ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom