Katibu UDASA: Dkt. Kaijage aliniambia Mkipata nafasi msaidieni mke wangu

Katibu UDASA: Dkt. Kaijage aliniambia Mkipata nafasi msaidieni mke wangu

Na iwe fundisho kwa Wahadhiri uchwara
Hapana haijawahi kufika hivi toka tumepewa uhuru na wakoloni Mwalimu na harakati zake hakuwahi kuingilia mijadala ya elimu za juu hasa ( chuo kikuu enzi hizo maana kilikuwa kimoja) kina Sitta (RiP) spika, wamebishana sana na mwalimu mpka wanaitwa ikulu kuelezea shida zao wakadai hawapati tena mkate wenye siagi kama zamani waliishia kutandikwa viboko licha ya kuwa na hoja, mijadala ndio chanzo cha fikra hatuwezi wote kuwaza mawazo sawa hilo haliwezekani mkubali mkatae. Kwanini zama hizi ndio zimekuwa za kukandamiza uhuru wa kujieleza mwalimu alinusurika mapinduzu mara 4 zama hizi maelfu wameuwawa kisa maandamano na bdo wanapea watu kila uchao kesi za ugaidi hili ajabu jingine
 
Watanganyika imefika mahali kama tunangoja Malaika ashuke na Panga atupiganie!
Kama mhadhiri anaweza kukamatwa harafu Wahadhiri wengine wakaendelea kufundisha bila kuweka Chaki chini basi.
Sina hakika kama Wahadhiri wa Kenya wangekubali!
Tuna hali mbaya kuliko tunavyofikiri tusione wanasheria wanapambana kote nchini kuwanasua wenye mashtaka hasa ya kisiasa (Pro-bono) wanaelewa kinyume na hapo watafia jela maana wadharimu hutumia vyombo kama polisi na mahakama kukandamiza sauti zote kutia hofu ili wengine waogope ajabu kelele ndio zinaongezeka, napenyezewa kuwa mkakati maalumu kwamba huandikishwi pale unapofikishwa na hayo ni maelekezo hivyo utatafutwa miaka huonekani kwenye vitabu vyao, rejea kesi ya Mbowe na walinzi wake wale ex- cdos nchi watu wanajiamulia watakavyo
 
Watanganyika imefika mahali kama tunangoja Malaika ashuke na Panga atupiganie!
Kama mhadhiri anaweza kukamatwa harafu Wahadhiri wengine wakaendelea kufundisha bila kuweka Chaki chini basi.
Sina hakika kama Wahadhiri wa Kenya wangekubali!
Mkuu njaa. Labda tuje na suruhisho ni nini kifanyike ikiwa mrija utakatwa.
 
Sijasoma shule za Kata mimi umri sawa na baba yako Mzazi ninachokumbuka nilichanga 30,000 ili ijengwe kwenye kata ninayoishi
Wewe ni zao la shule ya kata kwasababu hakuna mzee mwenye akili za panzi kama wewe
 
Katibu Mkuu wa UDASA, Dk. Dominicus Makukula, amesema wakati alipomtembelea Dk. Melikisedeki Kaijage, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) anayekabiliwa na kesi ya ugaidi, alitoa ujumbe mmoja muhimu.

Kwa mujibu wa Dk. Makukula, Dk. Kaijage alisema: “Mkipata nafasi, msaidieni mke wangu.”

"Juzi sisi tulipatwa na mkasa hapa kwenye uhuru wa kitaaluma kuna mwalimu alikamatwa kwa kutoa mfano... somo linaendana na kitu kinaitwa governance na maswala ya utawala hapa Tanzania basi akakamatwa akawekwa ndani".

"Mimi mahusiano yangu na huyu ni mwanataaluma mwenzetu na ameingia kwenye matatizo akiwa ni mwanataaluma. Kwa hiyo nimekuja kumuona na kumtia moyo kama mwanataaluma"

"Nawasihi na ninawaomba msizungumze kitu kwa sababu sielewi nini kinaniandaa msizungumze kitu mkipata nafasi naomba mumsaidie mke wangu".

Soma zaidi: Mhadhiri UDOM aliyepewa dhamana na Mahakama, sasa apewa shitaka la ugaidi, ahamishiwa Gereza la Isanga

View attachment 3650487
Hii post imenikumbusha methali ya "Kwa muoga kulienda kicheko na kwa shujaa kulienda kilio"!
 
Tunaishi nyakati ambazo viongozi hawafuati utawala wa sheria, mamlaka warejeshe huduma ya umeme na maji maana hazihusiani na kosa ambalo ameshitakiwa nalo pia ni pre- & postpaid. Lakini pia inasikitisha sana ama mtu ameshitakiwa bado hajathibitika kuwa na kosa kisheria ila ananyanyasika zaidi ya watumwa!
 
Mimi naanza kuwa na fikra mtambuka dhidi ya watu hawa.

Inawezekana kuna watu wamewatangazia waTanzania wenzao vita isiyo wazi. Wanaitumia tu fursa ya u-CCM kutimiza ajenda tofauti kabisa.

Fikra hizi zimeanza kunisumbua sasa akilini mwangu.

Nimeangalia mashahidi wa kesi ya Tundu Lissu; karibu wote wanaangukia upande mmoja. Hii ni kwa bahati mbaya au imetengenezwa kwa maksudi mazima!

Hata humu, mengi ya haya yasiyokuwa na akili,, ukiyafuatilia vizuri, yanaangukia huko huko kwenye kundi moja!

Hii ni hatari sana kama unapigana na adui usiyemjuwa.
Hiyo iko wazi sana,ndo kinachofanyika kwa sasa
 
Hiyo iko wazi sana,ndo kinachofanyika kwa sasa
Sasa kwa nini tusiokubali ujinga huu tusiwe wawazi, tuseme kuwa hapa siyo CCM inayotuvuruga; bali ni hawa waliochukuwa hiyo CCM na kuitumia kutuvuruga.

Tunaficha ugonjwa unaotuua?
 
Back
Top Bottom