Dah!
Wakati mwingine unakuwa kama 'robot' tu unavyoandika humu.
CCM kuendela kuwa chama cha siasa na kushika madaraka ya nchi tena ni hapo mafisadi yaliyokivamia chama hicho yatakaposafishwa kabisa toka ndani ya chama.
CCM inayo misingi mizuri sana, lakini imeshikwa na matapeli, kiasi kwamba imepoteza kabisa mwelekeo; na isipokuwa na uangalifu inaweza kujikuta inasambaratika yote kama chama.
Usifikiri kwamba sijui ndani ya chama hicho kuna wazalendo kweli kweli, ambao sasa hivi wanaburuzwa tu na hili genge. Kwa hiyo usitegemee baada ya ujinga huu wa Samia, asiyekuwa na chembe hata ndogo ya mapenzi ya nchi anayoiongoza, viongozi watakaofuata wataendeleza maovu yale yale aliyoyaachia nchi.
Ile IGA ulikuwa ni usaliti kwa nchi yetu, ndiyo maana ilistukiwa na kutupiliwa mbali.