Kuwa na mapenzi na nchi kwa mujibu wa Kalamu ni kuwa vipi?. Unaweza kujidanganya kwamba wewe ni mzalendo na ukawa fisadi mwenye kuifilisi nchi kuliko wale mafisadi wenyewe.
Narudia tena kumpa tender DP World ni maamuzi ya CCM yenyewe kabla hata SSH hajateuliwa na Rais JPM awe makamu wake.
Pia ni matakwa ya ushindani wa shoroba [corridor] zilizopo. Tumepewa faida za kijiografia kulinganisha na mataifa mengi ya ukanda huu na tutakuwa wajinga tukikaa tu bila ya sisi kuitumia faida hiyo katika kukuza uchumi wetu.
Jambo ambalo lipo wazi kabisa kati yetu, wewe na mimi ni kwamba wewe maslahi yako yapo DP World, na wala siyo katika ufanisi wa bandari yetu; hili sasa lipo wazi kabisa.
Mimi, sitajali sana, nani anahudumu hapo kwenye bandari yetu na kuleta manufaa makubwa kwa nchi yetu; lakini ningetulia sana moyo wangu kama tungeweza kuwa na viongozi wa kuwasaidia waTanzania wenyewe kuifanikisha kazi hiyo.
Huyu DP World anayekumiliki wewe, alianza shughuli zake mwaka 1999, tu. Siyo muda mrefu sana. Sisi kama nchi, ni lazima nasi tuwe na lengo la kujijengea uwezo wa kufanya mambo ambayo yanaweza kuwa ndani ya uwezo wetu. Kuendesha bandari kwa ufanisi siyo jambo la ajabu sana, kwa nini tutishike kiasi unachofanya wewe tuonekane kutishika.
Na hili silisemei kwa maswala ya bandari peke yake. Tunatakiwa kuchukua hatua za kujijengea uwezo katika kila nyanja ya shughuli zinazofanyika hapa nchini.
Najaribu kunielewa, sihimizi serikali ndiyo ilazimike kuyafanya haya, lakini ni jukumu la serikali kusimamia na kuhimiza uwepo wa hali hii katika jamii yetu.
hatuwezi kuwa nchi ya kutegemea wengine toka nje waje kufanya hata yale tunayoweza kuyafanya sisi.
Uwepo wako hapa jukwaani, tokea mwanzo, ni kupigania DP World tu, na siyo jambo jingine lolote, na wala siyo kampuni nyingine yoyote inayoweza kufanya kazi hapo bandarini kwa ufanisi, hata zaidi ya huyo DP World.
Kwa hiyo nisome vizuri utambue tofauti kubwa sana zilizopo kati yangu na wewe. Kuendelea kwako kuipigania DP World hapa hakutabadili chochote katika utambuzi wangu kwako, kuwa wewe ni mali ya DP World, kwa maslahi unayoyajua mwenyewe.
Kama kweli wewe ni mTanzania, najua utanielewa tu, hata kama hutaweza kubadili msimamo wako.