Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

Sidhani kama umemuelewa.

Umeambiwa hasara ipo japo haituhusu sisi. Kwa maana hiyo suala la upotevu wa umeme njiani lipo hata kwa hao Ethiopia.

Sasa kama hasara ipo kwa Ethiopia basi hakuna faida ya wataalam wa Tanesco kwenda kujifunza huko Ethiopia kama ulivyopendekeza.
 
Wanatangaza wao, mjadala wanaanzisha wao wenyewe na kujijibu wenyewe tena.
Nchi ina vituko hii
 
Hio ni bei gani kwa Tshs ? 0.077 !!! Na kwanini tunazalisha kwa gharama zaidi wakati tuna vyanzo lukuki na Bwawa likiisha ni kwamba overheads zinapungua hivyo gharama ya uzalishaji kupungua ?

Kuliko kuendelea kununua nje hata zikipanda na kuwa dola 5 kwanini wasiwaze long term kuhakikisha umeme unafika kila kona ya Tanzania kwa gharama nafuu ?

Shida tunawaza leo na sio kesho waliotangulia kila mtu angewaza leo yake sisi tungekuta hio miundombinu ? Hio 0.077 badi ni gharama kubwa na inatoka kwenye Kodi zetu inabidi tuwaze sisi ndio tuanze kupeleka excess huko na kupata hizo 0.077 after all tuna vyanzo vingi kuliko wao...; Leo hii tunanunua LPG ili tupikie kwanini tusitumie huo umeme kwa kupikia kwa walio karibu na grid ili hio excess ya kununua LPG ndio tukanunue huo umeme wa so called bei rahisi ?

Na hii excess ya kwetu tunaiuza kwa kiasi gani ? Hiki Chama kishakuwa Chama cha Madalali
 
Sidhani kama umemuelewa.

Umeambiwa hasara ipo japo haituhusu sisi. Kwa maana hiyo suala la upotevu wa umeme njiani lipo hata kwa hao Ethiopia.
Rudia kusoma nilichoandika

Mtu kuuza kwa loss bidhaa zake kitu cha kawaida ili mtu aambulie chochote

Ethiopia kusafirisha umeme kilomita zote hizo wanapata loss kubwa lakini wako tayari kutuuzia kwa bei nafuu na hiyo loss yao walau wapunguze loss

Ndio maana ufafanuzi wa katibu mkuu Mramba kasema hiyo loss yao haituhusu sisi tunaangalia bei nafuu wanatuuzia

Wewe ndio una kichwa kigumu kuelewa nilichoandika

Rudia kusoma nilichoandika
 
Hii nchi Yaani unaweza ukajikaza kabisa usichangie chochote kwa ajili yako, lkn ukakuta Jambo likakukereketa kweli hahahaa!
 
Kama namwelewa sana KM Mramba. Ufafanuzi usiokuwa na utata wa mhandisi๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Mitambo ni mipya ila nyaya za zamani, nisawa na kununua gari jipya ukalipitisha barabara mbovu, bora ukodi bolt tu
 
Sijui kichwani mwetu ni viazi na ndo maana tunadharaulika kiivo
 
Elimu Elimu Elimu... TANESCO endeleeni kutoa elimu huku tukijaribu kuwaelewa... kabla hatujakata tamaa kuelewa. Topic ngumuuuuu
 
Tunalipa kodi,wao ndiyo wanapanga wazitumiaje.
Tukazane kulipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ