Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Nawasikitia sana watu ambao wamebaki kuamini kwamba hapa duniani kuna kitu kinachoitwa uchawi na kinafanya kazi. aisee hakuna kitu kama hicho binadamu ni mnyama tu ana limit zake yako miujiza hawezi tu kufanya mfano kupotea na kwenda kutokea sehemu nyingine au eti kujibadilisha umbo..

kuamini uchawi ni ujinga naini uoga uliopitiliza mimi nimeshapita mazingira mengi sana tu kuanzia makaburini, mabaharini, misituni usiku Kwa usiku na sijawahi kuona badiliko lolote nikalihusisha na eti ni mbinu za kishetani. Maisha yapo tu the way yapo magonjwa yapo ya Kuua so hata Ukifa ghafla hujalogwa tunakupima tunajua ulikuwa na ugonjwa gani..

Zamani kweli mambo mengi yalikuwa hayajagunduliwa maswali yasiyo na majibu yalikuwa mengi.. Pressure, kisukari, kifafa na magonjwa ya akili haya kujulikana hivyo watu akili zao ilibidi ziishie kwenye kuamini uchawi kwamba Ukifa na ugonjwa wasioujua basi umelogwa..

Uchawi upo Kwa dhana kwamba una fanywa (Wana upractice Kwa mazoea yao ila hautendi lolote yaani huwezi ukawa tabora eti umuue mtu yupo dar (hakuna outcome yoyote).

Ndo maana mimi daima napenda mtu ninayefanya naye mijadala awe haamini hakuna uchawi nitamkubali sana nitaona kichwa chake kinaweza ku solve mysterious mbalimbali.. mbona simple tu MUNGU YUPO, UKICHAA UPO, MAARIFA YAPO, NGUVU ZIPO ILA UCHAWI HAUPO LABDA UCHAWA.mwingine unakuta eti kisa tu ana kidonda kilichokataa kupona basi wanaelekeza fikra kwamba ni cha kulogwa cha kichawi mbona ishu kama hiyo ni nyepesi kwamba akili yako haitaki kuamini kama kidonda hakiwezi tu kupona Kwa sababu nyingine za afya au mazingira Mpaka utuhumu uchawi?
Una ujinga fulani hivi kichwani mwako.

Soma,

WAEFESO 6:11-12 ; MAMBO YA WALAWI 17:7; KUMBUKUMBU LA TORATI 32:17 ; ISAYA 13:21 ; 1 WAKORINTHO 10:20-21.
 
Kwa hiyo hapo ushahidi wa kuonekana uchawi upo ni kitu gani? Je ni mzee kutokea msijue alikotokea au ni inayosemekana harufu ya jini? Au ni kitendo cha kuambiwa mtupe na muondoke bila kugeuka?
Ndugu yangu ndege JOHN still wewe bado Ni kijana mdogo (your still growing up)

Nakuombea uishi Sana ili uweze kuyashuhudia mengi na mengineyo wewe bado upo upofuni

ASANTE
 
Ndugu yangu ndege JOHN still wewe bado Ni kijana mdogo (your still growing up)

Nakuombea uishi Sana ili uweze kuyashuhudia mengi na mengineyo wewe bado upo upofuni

ASANTE
Miaka 29 ni mTu mdogo? Kwamba nitaanza kuona mauza uza nikiwa 40 au. Anyway nitajie mfano wa uza uza.. Kwamba nifilisike? Niugue figo? Mtoto wangu afe? Kitu gani nipe mfano wake ambacho huenda ikawa nguvu ya uchawi
 
Hajakukuta,kunajamaa alimpa mimba mtoto wa mzee mmja hapa Kigoma,Jamaa hakua na malengoo nae kumuoa yule Binti. Mzee alipombana mwanae Mimba ya Nani akataja ni ya B,Mzee asubuhi paap yupo kwao na B anataka apate maelezo Toka kwa B.

B,akaitwa akasema sihusiki na mambo hizo tena kisela huku akicheka,Mzee akamwambia naomba uwe mkweli B nakuheshimu.B akapinga tena Mzee akamwambia "namwachia Mungu" hahahaha.

Bwana Usiku B amekaa sebuleni na wazazi wake na Mjomba wake aliekuja kuwasalimu Mara paap bonge la panya linakatisha sebuleni kwa speed mdomoni limeuma Mboo na pumbuu,kha! Wanahamaki linakimbilia Juu ya Dali.B kupiga mkono kucheki machine yake loool anakutana na maku🤣🤣alipiga ukeleeee uoooo.Mjomba anauliza vipiii uncle haipooo aaseee mzee mshenzi sana.

Familia nzima walitoka Usiku huohuo kwenda kwa mzee yule mama na Mjomba walilia sana Baba yake alikua safarini Mwamza.Mzee akawaambia mwambie mwanao aseme ukweli ,dogo alikili mimba ni yake mzee akawaambia upo tayari kumuoa B ndio nendeni nae nitakuja Kesho tumalize.Toka hapo B akawa ameoa.

Broo uchawi upo omba yasikukute,ila nivitu si vyakutilia mkazo kuvizingatia,Kuna watu wakijikwaa et kategwa mchawi kashindw mara akipaliwa maji et mchawi kashindwa Hali hii mim naita Ufala/ushamba.
 
Unaelewa kweli unachokisema? Kafatilie mazingaombwe ni nini, yanafanyikaje, na yanahitaji vifaa gani kutekeleza.

Babu yangu alikuwa mwanamazingaombwe aliwahi kunambia ule ni uchawi na hatothubutu kumfundisha mwanae yeyote
Alikuambia hivyo kukuogopesha na kukuaminisha alikua anafanya mambo yasiyowezekana
 
Kasome Machapisho ya Dr. Fr. David Clement Fumbuka, Padri Mzungu aliyefanya extensive research kuhusu jamii ya Wasukuma na mwanzilishi wa Sukuma Museum pale Bujora, Mwanza. Ndo utajua wewe na Fr.Clement nani anaujua ukweli wa haya mambo.
 
Mheshimiwa Dkt. Gwajima

Unaposema wewe si Muumini wa hizi Imani Una maanisha nini

Kama unasema wewe si muumini wa kuamini kwamba ushirikina haupo basi vilevile wewe ni muumini usiyeamini Mungu yupo.

Ndiyo maana yako mheshimiwa?
Swali zuri Sana. Kutokuwa muumini namaanisha kwamba fikra hizo hazinitawali tena maana Mungu alishanipa mamlaka ya kuzipuuza na hazina mamlaka juu yangu tena milele...

Karibu kwa swali la ziada ndiyo kuelimishana kwenyewe huku sisi Kwa sisi. Ahsante Sana kwa mjadala
 
Nikueleweshe Tena uchawi upo Kwa maana ya kufanywa yaani matendo yake mfano

Kukamata mkia wa mnyama kuanza kuzunguka nao mbuyu ukiamini fulani kitatokea au kwenda njiapanda kuoga uchi n. K matendo hayo yanafanyika ila hautendi lolote kama ni hela utazipatia kwenye kazi utalipwa na sio eti uloge uende chumbani ukute mahela yamejaa
Umemaliza kabisa mwenye masikio na asikie na mwenye fahamu na afahamu. Tuache kufarijiana huku tunasababisha majanga tu kwenye jamii na kuulizana bila majibu.
 
Back
Top Bottom