Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Kama unaamini MUNGU yupo inatosha, ila uchawi upo.
Kama ambavyo kuna Elimu ya Mungu duniani, elimu ya uchawi ipo mpaka ngazi ya degree kabisa sio kitu cha kufikirika tena πŸ˜…
 
Swali zuri Sana.

Tuifundishe jamii kwa shuhuda jinsi gani tumepambana na maisha hadi hapa tulipo pasipo kuingiza hofu ya fikra za ushirikina. Kwamba hatujawi tumia bidhaa yoyote ya ushirikina kwa Sababu yoyote ile. Halafu na wengine waseme walikutana nao wapi huo ushirikina Ili tuwasikilize tuwape mawazo mbadala. Maandiko yapo ila sasa mimi nasemea uhalisia, siwezi semea jambo katika Kona kwamba limeandikwa, waliondika wao waliliishi, mimi sijapewa neema ya kuliishi, nimepewa neema ingine, siwezi kulazimisha. Maana silioni wala sijakutana nalo na mapambano ya maisha yanaendelea sambamba na mafanikio bila hizi mambo mambo....
 
Safi Sana. Hizi ni bidhaa tu za matumizi ya kawaida kabisa mfano, vibuyu hivi vipo watu wanawekea maziwa ya ng'ombe huko ukweni kwangu usukumani mbona vyombo tu hivi ni mapambo tu, na hata kwetu iramba singida mbona hivi vibuyu tunachuma shambani .... πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Kwa hiyo ukiona hizi show ndiyo unasema uchawi huu..... Mwe
Ila nimecheka Sana... πŸ˜€ Eti picha kwa msaada wa mtandao
 
Kama unaamini MUNGU yupo inatosha, ila uchawi upo.
Kama ambavyo kuna Elimu ya Mungu duniani, elimu ya uchawi ipo mpaka ngazi ya degree kabisa sio kitu cha kufikirika tena πŸ˜…
Ila haihusiani na maendeleo yoyote ni klabu tu za watu. Tufanye kazi tuendelee tuache kumaliza watu kwa kuagiza viungo halafu wakishikwa wakaenda Polisi ni kilio tu kuanzia mwagizaji hadi mpelekaji. Ndiyo nini sasa kama siyo ujinga kwa herufi kubwa
 
Najua huamini uchawi na pia ni dhana ya imani nikuombe jambo tunaomba vitu vitatu tu bas
1: majina ya mama yako mzazi
2: majina yako matatu
3: naomba na picha yako
Baada ya siku 3 uje na bandikoblingine hapa
 
Mjinga mmoja huyu,ukikaa simiyu mwezi tu utaelewa
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Mimi nimeshakaa huko hakuna lolote jamani tuache Simiyu wafanye maendeleo yao ya haki hizi zingine hadith tu. Hata sasa wako vijana wasomi wanakaa Simiyu wanatumia fursa za maendeleo wanatoka ukiwauliza vipi hizi Hadith wanabaki wanakushangaa kuuliza swali iwapo uko sawa au umeamka na za janaπŸ˜€
 
Ukishiba makande lolote linalokujia unaongea tuπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hata mimi nasisitiza neno UCHAWI lifutwe kwenye dikishenare aka kamusi.
 
Mheshimiwa Dkt. Gwajima

Unaposema wewe si Muumini wa hizi Imani Una maanisha nini

Kama unasema wewe si muumini wa kuamini kwamba ushirikina haupo basi vilevile wewe ni muumini usiyeamini Mungu yupo.

Ndiyo maana yako mheshimiwa?
Serikali haiamini uchawi mkuu.
 
Mheshimiwa,
Kuishi Tanzania na kuijua Tanzania hakumanishi Zambia haipo, maana yangu ni kwamba kutokupitia hali hiyo hakufanyi uchawi usiwepo.
Binafsi sishabikii uchawi wala ushirikina wa aina yeyote na wala haunipi hofu katika kufanya mambo yangu ila haimanishi haupo, maana hata kifo kipo lakini haimanishi niache kupambana kuishi vizuri.

Kuna elimu ya uchawi ngazi ya degree kabisa sio mambo ya kufikirika.

Elimu bora sio kuficha uchawi kwamba haupo ni kuhakikisha watu wanafanya mambo yao bila hofu ya uchawi na kutojiingiza huko kuharibu maendeleo na mambo chanya katika jamii.

Nimewasilisha.
 
Hata mimi nasisitiza neno UCHAWI lifutwe kwenye dikishenare aka kamusi.
Jamii ikielimika ikaamua inawezakana tu. Na elimu siyo ile tu ya darasani Bali elimu ya fikra za kuangalia mambo kwa dimensions sita na zaidi siyo moja tu.

Kule Instagram kuna shuhuda ya mama mmoja aliyekaa na uvimbe tumboni kilo kama tisa na zaidi akisubiri kujifungua mtoto miaka 27 akiambiwa kafanyiwa ushirikina, mwisho wa siku kaenda hospitali ina mtaalamu mzuri kaambiwa liuvimbe tu kama mauvimbe mengine yoyote. Anajuta kukaririshwa dhana potofu
 
Mkuu leo usiku nipo nawewe,, naamini kesho utakuja na uzi mpyaaaaaπŸ˜ŽπŸ€πŸΎπŸ€Όβ€β™€οΈπŸ˜Œ wabishi kama nyie ndo tunawataka.
 
When rational fails we turn to spirituality...., In short ni kutafuta majibu rahisi kwa mambo usiyoyajua na tungeendelea kwa mwendelezo huo huenda leo tungekuwa tunaamini Kupatwa kwa Jua (Eclipse) Ni ghadhabu za Muumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…