Katika Mkataba wa Bomba la Mafuta Hoima -Tanga imeandikwa Refinery itajengwa Tanga.

Katika Mkataba wa Bomba la Mafuta Hoima -Tanga imeandikwa Refinery itajengwa Tanga.

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Watanzania hasa wapenda maendeleo suala la kujenga refinery ya Crude oil ya Uganda limeandikwa kwenye Mkataba siyo suala la Makubaliano na Dangote refinery ya crude oil itajengwa na waofanya drilling ya Total Energy.

Lakini Tujiulize Refinery ya Mombasa itakua inasafisha mafuta gani? labda Kenya nao katika Exploration zao wamegundua Mafuta na wao ndiyo maana Dangote anataka kujenga refinery huko na inaiweka Tanzania katika bomba la mafuta Hoima Tanga kuwa safe

Tumeangalia kwa hype sana ya jina la muwekezaji. Dangote bado ana vita kubwa ya kustabilize uzalishaji, cash flow na madeni ya refinery yake, Pale Nigeria bado kabisa hajafanya jambo la maana ndiyo maana tunahoji kwanini aingie haraka, Afrika Mashariki kabla hajamaliza changamoto za nyumbani kwao?

Tusiwe desperate sana kama Taifa mtu aje achukulie mikopo kwenye makubaliano yetu ili akastabilize deni la refinery yake ya Nigeria. Kwanza apambane na changamoto za uzalishaji na soko lake huko alikotoka. Afrika Mashariki ina maslahi yake ya kimkakati, si sehemu ya bailout ya mtu binafsi.

Kenya wapo desparate na hili Dili sababu wana mkwamo mkali wa mafuta na pili ni karata ya serikali ya Ruto juu ya kampeni za 2027, kwa upande wa Pili sisi tuna SPRP pamoja na Bomba la Mafuta kutoka Uganda lenye makubaliano ya refinery ambayo itajengwa tanga na ipo kwenye mkataba tayari.

Vigogo wakubwa wa Kenya is waliomkwamisha Aliko Dangote Kenya miaka 8 iliyopita alipotaka kujenga Kiwanda cha Cement bado wako kwenye mfumo wa serikali ya Kenya na utofauti wao kwa sasa

Wana utajiri mkubwa na Zaidi wamejiunganisha, hawashikiki na wananguvu zaidi katika kulinda maslahi yao.

Kenya bado haijaweza kumaliza ufisadi Rushwa inaitafuna Kenya na probably kuna watu wamevuta pesa kwa Dangote wanataka kumuingiza chaka kwa Mikataba ambayo ilisha kua Signed bado utekelezaji tuu.
 
Panda shuka, FDI ilipotea hapa ni massive!
$43 Billion si nchezo kwa uchumi wetu!
Tukubali tumepoteza basi!
Maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom