Hapana Mkuu! Ni mpaka kifo kiwatenganishe.
Hili la kuthitibika mmoja wao amefanya uzinzi ni katika Uchumba.Katika uchumba mwanamke akifanya Uasherati kabla ya ndoa hata kama ameshatolewa posa Mwanaume ana haki ya kuvunja uchumba na kuomba arudishiwe mahari.Lakini kwa watu ambao tayari wameshaoana na mmoja akafanya uzinzi hapo hakuna kutengana kwa namna yoyote.
Mathayo19:4-7
Mathayo5:30-32
Mathayo 5:31
Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
Mathayo 5:32
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Sio
Hapo hajatajwa Mchumba bali Mke.
Kumbuka kuwa uzinzi sio kuchepuka siku moja.
Uzinzi ni tabia ya kupenda Ngono nje ya ulipo halarishwa kutokana na imani yako.
Mkeo akichepuka na kukuomba msamaha inabidi umsamehe tu ndivyo inavyotakiwa.
Uzinzi ni tendo, mfano la mkeo kuendelekeza Ngono na watu wengine.
Ukienda Magoti ambako wanawake wanajiuza, kuna wake za watu pia tena wamepanga na chumba kabisa na ndio kazi yake anayoipenda.
Huyo ndiyo mzinzi, je mkeo akiamua kufanya hivyo utaendelea kubaki naye ?
Mwingine anahama nyumbani kwako na kwenda kuishi kwa hawala yake. Mbinu zote za kumtoa huko zinashindikana je utabaki bachela miaka yako yote iliyobaki ?
Mwingine unamfumania kila kukicha, leo unamfumania na Ali kwesho na Josefu, keshokutwa na James basi ni mwendo huo huo hata umwonye vipi je utaendelea kumvumilia hadi kifo ?
Ndio maana ukaitwa Uzinzi sio wa kufumania mara moja bali tabia ya Uzinzi.
Mkeo akiwa Mzinzi Biblia imeruhusu kumwacha halikadhalika mwanaume.
Wako wanawake wametelekezwa na waume zao kwa miaka mingi na huko aliko Mume kaoa mke mwingine na ana watoto na hana habari ya kumrudia mkewe tena, hapo Mke anaruhusiwa kuolewa na Mume mwingine.
Kudhibitisha Uzinzi wa mwenza wako lazima upitie hatua za Kibiblia kwa Wakristo.
Mke ana ofisi yake Magoti au kahamia kwa hawala au mume kemtelekeza Mke.
Hatua ya kwanza mwite ili kumwonya.
Akikataa mwitie wazee wa familia kama ndugu zake hasa baba na mama zake.
Akikataa liambie Kanisa juu ya hilo swala.
Akikataa oa mke mwingine.
Huna Hatia.