Wapi Uislam umetukuza majini? Kuna kutajwa ama kubainishwa uwepo wa hao viumbe kwa kuashiria Mungu muumbaji ameumba viumbe wa aina tofauti kwa material tofauti. Kuna ajabu Mungu akitupatia habari kwa baadhi ya viumbe wake aliyowaumba mwenyewe?
Itikadi ya Uislam Mungu ni mmoja, yeye ndiye anayepaswa kukusudiwa kwa haja zote, hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna chochote kilochofanana na yeye. Nguzo za Uislam ni 5, ya kwanza ni shahada ambayo ni ASH-HADU ANLA ILAHA ILLALLAH.
Kwa maana: Nashuhudia ya kwamba hakuna Mungu isipokuwa yeye tu Allah. Bi maana; laa maabuda bi haqqi fil ujuudi illallah! Kwa maana; wah-dahu laa shariika lah! Kwa taafisir ya kuwa Mungu anatosheka na shirika la peke yake. Hahitaji ushirika kwenye kuabudiwa.
Kwenye Qur'an Mungu anasema: "wa annal masaajidalillahi falaa'tad-uu ma-allahi ahadaa"- Na kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu na asiabudiwe yeyote pamoja naye.
Mtume swallallahu alayhi waalihi wasallam anasema; Yeyote atakayekwenda kwa msoma nyota(mganga wa kienyeji) kisha akasadikisha na yanasemwa na msoma nyota (yaani tawile).....Mtume anasema mtu wa namna hiyo swala yake haitokubalika kwa siku 40 na akifa ndani ya hizo siku pasipo kutubu anakufa hali ya kuwa ni Kaafir.
Katika suratul baqara Mungu anasema kumtetea Mtume wake Suleyman baada ya wayahudi kudai Nabii Suleyman amani ya Mungu iwe juu yake alikuwa ni mshirikina. Mungu akajibu kwa kusema kwa kuanza; wama KAFARA Suleymana illa sh-yatwiina yu-allimuuna nnaaasa s-h-r...Hakukufuru Suleymani isipokuwa ni masheytwaani wa kijinni waliyowafundisha watu uchawi. Mungu hakuanza na Nabii Suleyman hakuwa mshirikina bali alianza kwa kusema hakukufuru. Ushirikina ni kufr katika Uislam na ni dhambi kubwa sana!
Kuna aya nyingi na hadithi kadhalika zinazokanusha ya kuwa Uislam haufungamani na ushirikina, za juu ni baadhi. Si jambo jema kulizungumzia suala hauna elimu nalo kisha ukalitolea ufafanuzi na hitimisho, kwani hayo ni makosa.
Rabbuna allahu dhuljalaali
Hasbuna allahu dhulkamaali
Waislam tunayemuabudu ni mmoja tu, ni Allah. Huwa Allah!
Katika vitabu vilivyokuwa na sheria ni Tawrat ya Nabii Musa amani ya Mungu iwe juu yake. Baada ya hapo viumbe vinavyoishi kwenye hii ardhi ya sayari ya dunia walidhani ya kuwa Mungu hatoshusha kitabu kingine chenye sheria kitakachokuwa muongozo kwa viumbe wa Mungu. Majinni nao ni viumbe wa Mungu.
Walipoisikia Quran wakarudi kwa jamii yao na kuwapa habari. Viumbe vyote vipo kwenye miliki ya Mungu. Kwa hili, Mungu akatupatia habari kwenye Quran mazungumzo ya majinni walivyorudi kwenye jamii yao. Na si ajabu kwani ni viumbe wa Mungu. Hii sura ndiyo ikaitwa Suratu jinni. Ndipo majini wakasema kuwaambia jamii yao kwenye mazungumzo yao;
Innaa sami-ina Qur'anan ajaba! Kwa maana; hakika yetu sisi(hao miongoni mwa majini) tumeisikia Quran ya ajabu.
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.
3
4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
4
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.
5
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
6
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
7
Kwenye Quran aya nyengine Mungu anasema; wamaa-khalaqtul jinna wal insi illa liyaabuduun. Kwa maana; Mungu hakuumba Majini na Wanadamu isipokuwa wamuabudu. Kama Malaika wanavyomuabudu na kumtukuza Mungu, nanyi viumbe wengine wajibu wenu ni huo huo. Hivyo, hakuna la kustaajabisha hapo. Na bila shaka kwenye baadhi ya hizo aya jawabu lako limo humo.
Mzee, kwa imani ya kiislam binadamu analindwa na Mungu. Na laiti asingeliuweka ulinzi wake miongoni mwa majini waliyomkufuru Mungu wangelimchezea binadamu kama binadamu anavyochezea mpira.
Umeandika uongo mwingi sana na sijui unapata manufaa gani kwa haya! Mengineyo nitayaweka sawa baadaye kwa sasa nina majukumu.