Katika ukoo wetu mimi ndiye wa kwanza kuwa mwajiriwa wa serikali, jifunze kitu hapa

Katika ukoo wetu mimi ndiye wa kwanza kuwa mwajiriwa wa serikali, jifunze kitu hapa

Kwa hiyo mwanangu unajisifia kuingia utumwani ukiamini mungu Kaku fanyia. Hivi huoni mifumo ya kuajiriwa imekaa kiutumwa?
 
Kulikuwa na minong'ono kuwa ndugu yetu mkubwa ni mchawi na ana roho ya wivu. Mafanikio anataka yawepo ndani kwake tu. Wengine walikuwa mpaka wanakuwa wa kwanza kiwilaya katika mitihani ya dhihaki (mock) darasa la saba.

Ikifika mitihani ya taifa wenzake aliyowaburuza darasani wanapangiwa Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys n.k lakini yeye hata shule ya sekondari ya wilaya hafiki. Akibahatika basi atapata kuchaguliwa shule ya ufundi seremala.

Sometimes mtu anafanya usaili wa kwenda jeshi kila kitu kinakaa sawa, mara mambo yanacease mtu anaendelea kuwa fukara.

Brother wetu mmoja alikubalika sana mpaka aliweza kupewa kuwa kaka mkuu kuanzia la nne mpaka siku anamaliza la saba, kwenye michezo ndiyo alikuwa balaa, kila mchezo anaoshiriki lazima afike mkoani na huko mkoani hakuna wa kushindana naye. Leo hii ni maskini kabisa.

Mimi nikiwa darasa la saba nikampokea Yesu na kuokoka. Kwa mara ya kwanza katika ukoo wetu nachaguliwa kwenda sekondari tena shule ya kitaifa si ya kata au wilaya. Nilihakikishiwa kabisa kuwa sitavuka la saba na kutolewa mifano ya wenzangu, lakini Yesu akavunja mipaka mpaka sasa ni mwajiriwa wa serikali.

Nimesoma mpaka chuo kikuu, ndiyo mtu wa kwanza kuwa na degree katika ukoo wetu na ndiyo mtu wa kwanza kuionja sekondari katika Ukoo wetu, na ndiye mtu wa kwanza katika ukoo wetu kuwa Mkristo.

Yesu ndiye kiboko ya uchawi, laana, mikosi na kila hila. Ukimpokea kwa lengo jema ukiamini kuwa yeye ni njia ya kweli na uzima hatakuacha.

Kuna mambo mengi kanitendea ila napenda kwa leo tuishie hapa.
Hongera sana, hata mimi nimeokoka na ninaona kuna vitu nipo tofauti na wenzangu. Ila mpendwa nimefurahi kusikia umeokoa ila mpendwa kuna vitu inabidi uvifanyie kazi kwani sio vya mtu aliyeokoka kama lugha mbaya zenye ukakasi. Hua huna lugha nzuri hasa upande wa siasa.

Jitahidi mpendwa kua na lugha nzuri ikizingatiwa sisi tuliookoka ni barua ya kusomwa na watu wote na pia neno limetuasa kua wapole na wanyenyekevu. Samahani kwa kuleta hili katika ushuhuda wako ila biblia imetupasa kuonyana na kukumbushana na mwisho wa yote twende mbinguni. Asante
 
Mkuu hongera, umeshajipatia buyu lako la asali ? Maana huko serikalini sasa hivi ni mwendo wa kulamba asali 🐝🍯
 
Na elimu ya kutosha kuhusu hili. Ipo hivi na ieleweke ya kwamba. Waafrika wako masikini sababu maisha yao yapo connected na mizimu, na mizimu haitaki maendeleo thus ukijenga nyumba kijijini unalogwa ukiaga unalogwa, ukisoma haufaulu,ukilima ufanikiwi,nk. Ni hadi uwe maarifa ya kucut off ile connection ndipo utoboe.Talielezea ili jinsi nguvu ya mizimu inavyozuia mtu kufanikiwa.
 
Tatizo la watanzania wengi ni kushangilia ushindi kabla mechi haijaisha. Ajira tu umeshajiona Bill Gates. Inasikitisha sana.
Mtu mwenyewe anytime anaweza akapigwa redundancy alafu anajimwambafai, akipitishiwa panga ataanza kuwalilia waliomkata panga anamsahau Yesu, kweli Africa ndipo ujinga ulipozaliwa na wajinga ni wengi kupita maelezo yaan mtu anamiliki vyeti tu ila kichwani empty
 
Na elimu ya kutosha kuhusu hili. Ipo hivi na ieleweke ya kwamba. Waafrika wako masikini sababu maisha yao yapo connected na mizimu, na mizimu haitaki maendeleo thus ukijenga nyumba kijijini unalogwa ukiaga unalogwa, ukisoma haufaulu,ukilima ufanikiwi,nk. Ni hadi uwe maarifa ya kucut off ile connection ndipo utoboe.Talielezea Ili.
Utaielezea wapi? Na kwanini usielezee hapa? Hauoni km huo ni sehemu ya ujinga ulionao? Kazi na kupata kazi na ajira ni juhudi, mbinu na maarifa ya mtu binafsi plus connection ukikosa vyote utaishia kua kapuku tu acha kumbebesha Yesu mizigo isiyomuhusu
 
Sasa Yesu ameingiaje au Yesu ndio amempa kazi au Yesu ndio amemuajiri? Sometimes acheni upambe na kampeni za kijinga km hizi watu sio wajinga kiasi hicho hata km ni mfia dini huwezi ukaandika ujinga km huu ulioandikwa hapo, wewe eleza ni juhudi na kutokukata tamaa plus connection ndio vimekupa mafanikio ya kufikia malengo yako stop saying Yesu kanipa hiki Yesu kanipa kile huo ni upotoshaji mnafanya kampeni za kuingiza watu wengi kwa wachungaji wapigaji huku wao wanabaki kua masikini,

Km Yesu angekua hivyo kila anaeenda kanisani si angekua anaenda na RR sasa mbon wengine ni makapuku na kila siku wanatoa Sadaka au Yesu yupi mnaemzungumzia? Msitufanye sisi mazuzu
Wote awaendi kanisani kwa lengo moja.Kwenda kanisani,kumjua Mungu na kuwa na maarifa ya kiMungu ni vitu tofauti kabisa.Na si KILA mtu ana interest za kuwa tajiri.
 
Ni shule inahitajiHuwezi kutulia kidogo pia ni mada ambayo inaweza ikapanda yenyewe stay tune. Huwezi ukafanikiwa bila kutengeneza ulimwengu wako wa roho kwanza ndipo utapata hizo connection, kupambana sio kupata bali kupata ni wakati, watu Wana juhudi Sana wanafanya Sana Kazi still awatoboi.
 
Waafrika tunapenda, kuhusudu, na kuhofia sana miujiza miujiza katika kupata mafanikio au kutatua matatizo.

Mungu muumba mwenyewe alimwambia Adam, kuanzia sasa utakula kwa jasho.

Kama hilo tamko lilishatoka lini liligeuzwa?

Yesu mwenyewe alisema asiye fanya kazi na asile. Sasa tuulizane hapa, tunaodhani wamefanikiwa, ilikuwa ni miujiza?

Kuna wanaoonekana kufanikiwa kupitia makanisa wanayoyaongoza sawa, lakini ni kwa kufanyia kazi mipango yao ya kukusanya wanacho kitaka.

Tumwombapo Mungu tumwombe maarifa zaidi tutakayo yafanyia kazi. Jamii zilizofanikiwa zimefanikiwa kwa kuweka maarifa mbele na kufanyia kazi hayo maarifa.

Jifungie chumbani funga sana omba sana kama utapata kapu la fedha humo ndani mwako. Maana huyo umuombaye alisha weka msimamo.
UTAKULA KWA JASHO.
 
Wote awaendi kanisani kwa lengo moja.Kwenda kanisani,kumjua Mungu na kuwa na maarifa ya kiMungu ni vitu tofauti kabisa.Na si KILA mtu ana interest za kuwa tajiri.
Sasa umemuelewa alichokiandika Sandali Ali hapo au unapingana nae kwamba kaandika ujinga? Yeye anasema Yesu kampa kazi kampa ajira, yaan anaamisha wale wote wanaosota makanisani kumuomba Mungu ili wafanikiwe kimaisha na hawafanikiwi kwa lolote huku wakijimaliza kutoa Sadaka za kuchangia kujenga makanisa hawana Yesu au hawapo na Yesu? Ila wakibadiri dini kutoka uislma na kuhamia ukristu na kua na Yesu basi watapata kazi na watapata ajira km sio uzuzu ni nini huo?
 
Sasa Yesu ameingiaje au Yesu ndio amempa kazi au Yesu ndio amemuajiri? Sometimes acheni upambe na kampeni za kijinga km hizi watu sio wajinga kiasi hicho hata km ni mfia dini huwezi ukaandika ujinga km huu ulioandikwa hapo, wewe eleza ni juhudi na kutokukata tamaa plus connection ndio vimekupa mafanikio ya kufikia malengo yako stop saying Yesu kanipa hiki Yesu kanipa kile huo ni upotoshaji mnafanya kampeni za kuingiza watu wengi kwa wachungaji wapigaji huku wao wanabaki kua masikini,

Km Yesu angekua hivyo kila anaeenda kanisani si angekua anaenda na RR sasa mbon wengine ni makapuku na kila siku wanatoa Sadaka au Yesu yupi mnaemzungumzia? Msitufanye sisi mazuzu
Amejisema mwenyewe,wewe kama huamini anachoamini kama kimyaa,watu kama nyinyi mmejichukulia kama mizani ya dunia yaani Jambo lenu sahihi la wengine sio,kama huamini,puuza sio kujifanya Una jibu la kila kitu cha dunia hii.Amesema Yesu wake wewe unaumia nini
 
Mkuu Saint Anno II njoo umsaidie Sandali Ali huku

Mkuu sijapingana nae ila alichokosea ni kutuaminisha kwamba ukiwa na Yesu then you're successful in each & everything that's rubbish, mimi mkristu tena sio wa mchongo alichokiandika ni ujinga km ingekua ni kwa faida yake binafsi si angebaki nayo kwenye kitabu chake cha kumbukumbu, yeye kaja kuwachota wafuasi humu watoke uislam waende ukristu kwamba ukiwa mkristu utafanikiwa kimaisha hio dhana ni potofu, na hii sio mara yake ya kwanza

Huyu amepotoka kifikra na kiakili inabidi tumuweke kwenye mstari sahihi kwamba mafanikio hayana udini, umenielewa?

Na wewe kabla ya kunivamia na kunikosoa jipime uwezo wako wa kufikiri km fikra zako ni fupi usipimane na mimi
 
Nimekuambia usijifanye wewe ndio mzani wa dunia kuwa majibu yako ndio sahihi,suala la kuamini la mtu binafsi hata wengine watakaovutika ni uelewa wao na Imani yao na vipimo vyao ndio vitakavyowapeleka huko .. kwamba wewe ni wale much know..aaah!Acha vitisho visivyo na hoja
 
Hakuna niliposema mimi ni mzani wa dunia nilichosema aache tabia ya kuaminisha watu kua ukiwa muislamu na hauna Yesu basi haufanikiwi huo ni uongo ninao ndugu zangu ni waislamu na wana ukwasi mzuri tu, acha kuishi na hio mentality kwamba ukiwa muislam haufanikiwi kimaisha sio ukweli
 
Mwanadamu anatawaliwa kiroho na kimwili pia kama walivyowatendaji wa serikali kuanzia mjumbe wa nyumba kumi hadi Raisi kama ngazi ya juu ya mwisho kiutawala katika nchi na ndivyo ilivyo pia katika ulimwengu wa kiroho pia zipo mamlaka zinazotawala watu kiroho pia kuanzia mchawi, gwiji, mzee, wakuu wa vilinge, machief, mizimu, na kuendelea. Hawa watawala wa kiroho upande wa giza, wameseti standard ya maisha ambayo watu wa eneo fulani awatakiwi kuvuka mstari fulani wa maisha waliyopanga wao kupitia maagano yao ya kichawi ambapo mtu yeyeto eneo hilo Akienda kinyume kwa kutaka kuvuka mstari walioset ni lazima yatamkuta mabaya, madhara au mabalaa kwa sababu anakuwa ameenda kinyume na maagano ya miungu yao.

Ni labda tu uwe na elimu ya kutosha au nguvu ya ziada Ili uweze kuuvuka mstari waliouweka. Kwann mizimu haitaki maendeleo jibu rahisi ni kwamba watu wakiendelea wataacha kuabudu mizimu kwa kuingiza tamaduni za kigeni maeneo hayo thus nguvu ya mizimu inawawahi fasta wasivuke mstari walioset thus ukijenga au ukitaka kujenga tu nyumba maeneo hayo unashangaa umefukuzwa kazi, umehamishwa kitengo, biashara imeyumba, mara ajali, msiba nk, umeenda kijijini na gari urudi, nk. Mfano wa standard walizoseti kupitia maagano mfano

1. Mtaa au eneo au kijiji, au ukoo nk huu Hakuna atakaesoma kama ni la saba wote ukoo mzima akijitahidi kufaulu shule dungwa mimba, anaemfadhili kafa, nk.

2. Hakuna vitu vya maendeleo ukijenga nyumba nzuri umeondoaka, huu mfano naouna mpaka wa vijijini vya Tanga na Vya mkoa wa Kilimanjaro hii barabara kuu ya Dar to Arusha. Angalia vijiji vya upande wa Tanga unakuta nyumba za udongo zimechoka, za nyasi hali duni ya maisha lakini chek upande wa pili uingiapo mkoa wa Kilimanjaro unakuta maendeleo yapo nyumba za Bati nyingi tu, nk. Means hivyo vya upande wa Tanga pana nguvu ya ucheif satanist inayotawala hapo inayozuia maendeleo.

3. Vifo vya ukoo au eneo vinavyofanana

4. Hakuna atakaemiliki gari au chombo chochote, nk. Au unakuta eneo zima iwe mtaa, nyumba zote zimeishia kwenye lenta, au Hakuna aliyefaulu kupiga hata plasta, au mtaa mzima hauna taa za nje

5. Watu wote kuwa na tabia zisizopendeza zinazofanana.

6. Magonjwa yanayofanana, hali ya uchumi mnayofanana, nk.
Madhara gani ukupata ukivuka mstari

1. Kifo
2. Mambo yako kuvurugika mfano ulipotaka tu kujenga
3. Migogoro isiyoisha ktk ndoa hili wanandoa inabidi kulichunguza sana, mfano baada ya kuhamia eneo fulani au nyumba fulani ya kupanga, au kiwanja sehemu fulani mlipojenga tu uelewano ndani mfano migogoro ya ndoa, magomvi, magonjwa, kipato kushuka, na mabalaa mengine. Tambua mpo kwenye nyumba au kiwanja kilichopo kwenye umiliki wa uchief satanist yaani kwenye mamlaka ya kiroho inayotawala eneo hilo.

Nini ufanye Ili uweze kuuvuka mstari uliowekwa na mizimu au uchief satanist unaotawala eneo hilo.

1. Simama kwa imani yako.
2. Hama eneo husika, thus wazawa wa eneo husika ni ngumu Sana kufanikiwa.
3. Uwe na nguvu za ziada yaani upigane kweli Ili uweze kuuvuka huo mstari. Kuzishinda nguvu za eneo husika.
4. Unaweza ukafanya maendeleo kupitia kujifichia kwa mgeni wa eneo husika awe kama mmiliki kivuli Ina maana ile nguvu ikitafuta mmiliki inakuta sio wewe.
5. Uwe na elimu ya kutosha kuhusu saikolojia ya ulimwengu usioonekana jinsi unavyotenda Kazi na jinsi ya kwenda nao kinyume nao Ili usiathiri mambo yako.
6. Kata kabisa connection na mizimu, maana unapozaliwa tu tayari upo connected kutokana maagano yaliyofanyika na vizazi vyako vilivyopita.

Shida zote wanazopitia watu mfano umasikini, magonjwa, talaka, usingle, kuzaaa hovyo, ulevi, laana na mikosi mbalimbali chanzo ni connection na mizimu na wengi hawana elimu hii thus wanachapwa na umasikini, magonjwa, talaka, ulevi, uzinzi, uroho, ubinafsi, teswa na wachawi, nk. CUT OFF ILI UWE HURU inatakiwa uyatawale mazingira yako na sio mazingira yakutawale.
CUTT OFF.
 
Shida zote wanazopitia watu mfano umasikini, magonjwa, talaka, usingle, kuzaaa hovyo, ulevi, laana na mikosi mbalimbali chanzo ni connection na mizimu na wengi hawana elimu hii thus wanachapwa na umasikini, magonjwa, talaka,ulevi, uzinzi,uroho, ubinafsi,teswa na wachawi,nk. CUT OFF ILI UWE HURU inatakiwa uyatawale mazingira yako na sio mazingira yakutawale.
CUTT OFF.
Sawa umeeleweka mkuu kwa hio unamaanisha suluhu ya hayo yote ni kutoka uislamu na kuongia ukristu ili Yesu akupe mafanikio si ndio au umemaanisha nini?

Nataka tusitoke kwenye kiini cha mada kwamba ukitoka kwenye uislamu na ukaingia kwenye ukristu na kumpokea Yesu basi wewe tayari umetoboa maisha na una guarantee ya kufanikiwa kwa lolote 100% bila shida yoyote
 
Back
Top Bottom