Katika umri gani ulifanikisha lengo la kujenga nyumba yako?

Watu wanajenga na bado hayo yote wanafanya
 
Saafi sana.

Ndo ujipange ujenge ingine japo mjini hadi ujenge nyumba ya kueleweka yapasa ujipange hasaa.
Jeuri hiyo ya kuitoa nyumba iliyo kichwani sinaaaa. Yani kodi yenyewe inanifukuza balaaa, uwanja sina hahahaaa😁😁, nacheka kama mzr ila moyon maumivu
 
Daah nimepambanaa kwa jasho na dam nimejenga..ile namalizia kuweka geti tu mke ananipeleka bakwata et tuachane tugawane nyumba daah...na hawa watoto wetu wawili tuwafanyaje?..kumbe alikua kwa maslahi tu sio mapenz
Mungu wangu..pole mkuu, daah...
 
Nakaribia 40 na bado! kila nikiangalia mbele naona kama kuna kama mitatu hivi kabla ya 'kuanza zoezi'. Nikiwaona wa 20's waliofanikisha, nakaribia kukimbia wazimu......najiona nimekosa mipango, lofa, mzembe n.k.
Inawezekana kipndi upo kwenye 20s nyumba haikua kipaumbele chako wala hukuifikiria na ulienjoy maisha yako(Hicho ndio kikubwa)
Na kama kwa sasa nyumba ni jambo la muhimu sana kwako jitahidi ufanikishe achana kabisa na yaliyopita wala kujilinganisha.
 
Mie nilitamani sana niitwe mama mwenye nyumba kabla ya 30 au nikiwa 30. Bado mwaka mmoja nifike umri huo na kiwanja kipo ilikua mwezi huu tuwe tunakimbizana na ujenz mwenzangu kanigeuka hataki tena kujenga na pesa ametunza yeye.
Sina hamu hapa nmekua mpolee mipango yote imeyeyuka.
 
Pole mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…