min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 61,672
- 178,673
Hawa wa wachungaji na mashekh hawana lolote ukipata nafasi ya kuwaumbua usisiteNani aliekwambia wanaoenda msikitini na kanisani wana huruma na upendo? Juzi nimepanda gari moja tumekaa siti moja ya mwisho watu wanne kati ya hao wanne kuna mchungaji kashika biblia mkononi anaelekea kanisani pembeni yake kulikua na Shekhe sijui imamu katupia kanzu na tasbuhi na wahuni wawili yaan mimi na mwenzangu mmoja tunatoka Segerea tunaelekea Mbezi Magufuli Stand njiani Kinyerezi akapamdishwa Bibi ana Stroke yaan kapalalaizi upande mmoja kushika bomba juu hawezi kabisa nilishangaa kuona mchungaji ambae alikua karibu na dirisha alifungua dirisha na kufanya km hajaona kitu huku Shekhe akawa amemkodolea macho tu yule Bibi badala ampishe mimi Muhuni nikaona isiwe kesi nikainuka nikamwambia Bibi njoo ukae kwenye nafasi yangu wote wakabakia wananishangaa nikamwambia wewe Mchungaji uchwara sogea kule mpe nafasi Bibi huyu akae Mchungaji akajifanya km hanisikii nikamwambia mara ya pili watu wote wakageuka nyuma akaona aibu akasogea Bibi akakaa cha ajabu sasa wote walikua wanashuka vituo viwili mbele mpaka nikajiuliza walishindwa nini kusimama pale hawa wakuda, kwa hio usipumbazwe na muonekano au title ya mtu upendo na huruma haina mtu au sehemu kwamba Msikitini au Kanisani ndio utapata watu wenye huruma na upendo sana sio hivyo