Katika watu wanaojua kutuchonganisha na Mungu ni hawa wanaokuja kuomba hela bar

Hawa wa wachungaji na mashekh hawana lolote ukipata nafasi ya kuwaumbua usisite
 
Kwa sababu hakuna njia rahisi ya kuthibitisha ilo inabidi usaidie tu. Shida ni pale unapoombwa msaada na mtu ambae unaona kabisa hana ulemavu na ana nguvu na akili timamu kuweza kufanya kazi
 
Hivi ndani ya pombe huwa kuna nini? 🙄 ukiinywa tu fyuuuuuu inashuka chini, masikini unashindwa kujua hata minyege imetokea wapi, huwa sielewi hapo tu
Ni suala ambalo linahitaji utafiti wa kisayansi. Wanasayansi wetu wa bongo wamezubaa sana.
 
Nilienda na mchumba restaurant moja, wakati nakula akaja muhudumu akaniambia yule Baba pale anasema umlipie na chakula chake, kuangalia ni mtu ambae simjui alafu ananiambia "mkuu na mimi naendelea hapa"

Sikumjibu nikamwambia Dada mwambie akulipe mwenyewe, jamaa alifikiri kisa niko na mchumba nitashindwa kuweka mikazo
 
😅😅
 
Yaani hapa utake usitake lazima umpe tu hela hata kama ipo nje ya bajeti yako
Umeanza kunywa lini Mkuu..Walevi wote huwa tuna moyo mkuu machoni pa Bwana.
Kuanzia TBL kule mpaka sisi watumiaji...
Tunasaidia sana kwa sana.Waombaji hawawezi kwenda Kanisani wala Msikitini huwa last option..
 
Kungekewa na camera angeonyesha upendo wote
 
Halafu kuna jitu jingajinga tu litaanza kusema walevi hawaendi mbinguni.Bogus kabisa hadi keshokutwa!
Sisi tupo mbele za Bwana toka enzi na enzi.
Mwana wa Mungu alibariki yale maji yakawa matamu na harusi pale kana ikafana.Hakukuwa tu na Tiktok miaka ile..ila ili fana..mpaka Mama Maria akasema Mwanangu umetutendea makuu..
Wafalme wenyewe wanashauriwa kupata mvinyo kidogo hawa walikuwa wanaketi na kuzungumza na Muumba wa ulimwengu..wewe nani?
 
Umeanza kunywa lini Mkuu..Walevi wote huwa tuna moyo mkuu machoni pa Bwana.
Kuanzia TBL kule mpaka sisi watumiaji...
Tunasaidia sana kwa sana.Waombaji hawawezi kwenda Kanisani wala Msikitini huwa last option..
Mkuu mitungi napiga kitambo tangu nipo o-level aza boys. Walevi tuna moyo wa kipekee kwa sababu tupo real. Hatusaidii ili tuonekane wema au kwa kuogopa kutupwa motoni tukifa. Tunasaidia kwa sababu hivyo ndivyo nafsi zetu zinatutuma
 
Ukiwa unawaza laki 6 ni chai , na hauna kilevi chochote kichwani upo sawa kabisa
Mlevi maskini huyo...msamehe ujue hata mimi zamani nikumuona mtu na gari nilihisi anahela sana.

Nilipofanikiwa kupata deals na kubadili magari matatu nikaona kuna watu wanalewa na kunadili magari kila baada ya miezi 6 tena ya kuanzia 95M kwenda mbele nilijitafkari sana.

Niliwahi safiri na Baba mmoja kumbe ni hawa waganga wa jadi,kwa ukarimu yule mzee alitununulia watu lunch ilifika 500k pahala pazito pale Iringa..aisee nikajua maskini ni mimi si kila unayemuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…